UTANGULIZI
Kichwa pamoja na kupigwa na nguzo kiliendelea kua juu, na macho yalitoa machozi yalo changanyika na damu, yakamwagika yakiosha viumbe kutokana na udhalili, na bendera yapepea juu ya mkusanyiko wa watu, na mwezi ung’aao daima, na malalo matakasifu hujengwa na watukufu na hutembelewa na mamilioni, roho za waumoni hupazunguka na kupakumbatia: (Amani iwe kwako ewe mja mwema mtiifu kwa Mwenyezi Mungu na mtume wake na kwa Amirul mu-uminina na Hassan na Hussein).
Mwezi wa bani Hashim, na mwenye kuhami wakina Fatuma, kielelezo miongoni mwa vielelezo vya umma, mtenda wema na mwenye kujitolea na mwenye kisimamia maamuzi yake, jambo lake lipo Dhahiri katika anga, hutembea baina ya watafutaji wa athari za utajo wake, aliweka katika mji wa Karbala maana ya utukufu na kujitolea, na akawa kielelezo cha undugu na ukamilifu, hekima ya Mola ilitaka amfikishe imamu Hussein (a.s) pembezoni mwa mto wa Furat, ili aendelee kubigwa na mawimbi uhai wote na awe na mazaru (sehemu) maalumu yenye kusifiwa, itakayo endelea kushuhudiwa, na kushuhudia dhulma za waovu, na kuendelea kulingania uadilifu na amani karne na karne, kubba ipo juu na minara miwili kama mikono inayopokea mema ya mbinguni na kuyatoa kwa walimwengu.
Anaendelea kuangazia usiku, kama mwezi ung’aao (badri) angani, macho yanakesha yakiuangalia na kuvutia nyoyo za wapenzi, na kuwafurahisha kwa maji yake yenye ladha nzuri.
Abulfadhil Abbasi (a.s) katika historia ya kiislamu amekua mtu muhimu sana, ni kiongozi shujaa ambye ni mara chache kupatikana mtu wa mfano wake katika ubinadamu wake na ujasiri alio kua nao na kila aina ya ukamilifu hakika ni fahari kwa watu wote duniani.
Abulfadhil alionyesha msimamo mkubwa katika tukio la Twafu, na ujasiri wa hali ya juu usio elezeka, alikua na nguvu za jeshi lisilo shindwa, alitia uoga katika jeshi la ibun Ziyad, na akawashinda kimaanawiyya kama alivyo washinda katika uwanja wa vita, hakika ushujaa wa Abulfadhil ni wa hali ya juu kabisa, ulikua na unaendelea kua ni similizi kwa watu za zama zote.
Hakika ushujaa wa Abulfadhil na utukufu alio kua nao kama alivyo sema imamu Swadiq (a.s): “Ammi yetu Abbasi alikua msimamizi makini, mwenye imani kubwa”. Utukufu na fahari kuhusu yeye sio kwa waislamu tu, bali kila mtu mwenye ubinadamu lazima atasifu utukufu wake.
Alikua ni mfano wa sifa njema, alikua mpole, muaminifu, mliwazaji, alimliwaza ndugu yake baba wa watu huru imamu Hussein (a.s) katika siku za mitihani mikubwa, akamlinda na kumuhami, hakika namna alivyo mliwaza ndugu yake hakuna anaye weza kufanya vile isipokua mtu aliye ongoka na mwenye imani kubwa.
Mfano wa mwenendo wa Abulfadhil Abbasi (a.s) na ndugu yake imamu Hussein (a.s) unatufundisha undugu wa kweli katika uislamu, hakuna aina yeyote ya adabu na wema na ihsani isipokua alimfanyia, miongoni mwa jambo linalo onyesha upeo wa mapenzi na namna alivyo kua akimjali ndugu yake ni pale alipo fika katika maji na kuyachota huku akiwa na kiu kali sana, alipo taka kunywa akakumbuka kiu ya ndugu yake imamu Hussein (a.s) na kiu ya watoto wa nyumba ya mtume (s.a.w.w) akaacha kunywa kwa ajili yao na akamwaga maji yaliyokua mkononi mwake, na namna alivyo simama imara katika mazingira haya magumu, wanahistoria wote wameandika habari hizi, je unaweza kupata mtu mwingine wa aina hii?!! Angalieni katika historia za watu wema duniani, kuna wa mfano wake?
Hakika Abulfadhil Abbasi (a.s) alipata shahada kwa ajili ya kutafuta uhuru na utukufu wa mwanadamu, na kueneza upendo na kuhurumiana baina ya watu, alifanya juhudi kubwa ya kuondoa dhulma na ufisadi, na kujenga jamii bora yenye utulivu.
Abulfadhil alibeba bendera ya uhuru na ukarimu, akaongoza msafara wa mashahidi katika viwanja vya utukufu, kunusuru jamii ya waislamu iliyo kua inaishi katika dhulma na uovu.
Abulfadhil alienda katika uwanja wa jihadi kwa ajili ya kuufanya utajo wa Mwenyezi Mungu uwe juu katika aridhi, utajo ambao ndio mwenendo kamili wa maisha wa wanadamu.
Amani ya Mwenyezi Mungu iwe juu yako ewe Abulfadhil, katika uhai wako na shahada yako imekua ni makutano ya amani kwa wanadamu wote, yatosha kua fahari kwako wewe umekua mfano wa mashahidi wote wa Twafu, ambao wamevaa utukufu katika ulimwengu wa waarabu na waislamu.
Abbasi (a.s)
Ni Abbasi bun Amirul Mu-uminina Ali bun Abutwalib bun Abdulmutwalib bun Hashim bun Abdulmanafi bun Quswai bun Kilab bun Murra bun Kaabi bun Luayi bun Ghaalib bun Fihri bun Maalik bun Nadhri bun Kinana bun Khuzaima bun Mudrika bun Ilyaasa bun Mudhiru bun Nizaar bun Ma’adi bun Adnaan.
Tunaishia hapa kuleta majina ya baba zake watukufu ambao wanafika hadi kwa nabii Adam (a.s) baada ya kusoma kauli ya mtume (s.a.w.w) isemayo: “Itakapo fika nasabu yangu kwa Adnaan ishieni hapo”.
Kana kwamba aliangalia ugumu wa kutamka majina, kwani majina yanayo endelea ni magumu katika matamshi ya kiarabu, yanaweza kukosewa badala ya kumaanisha utukufu yakamaanisha jambo baya la kupunguza utukufu wao, wakati wazazi wote wa mtume mtukufu na wasii wake ni watu wema, jambo muhimu hapa ni kufahamu kua wazazi wao hawakua na kasoro yeyote miongoni mwa kasoro za zama za ujinga, hawakuabudu sanamu, jambo hili wanalikubali wanazuoni wote wakweli, wanao waamini manabii na mitume.
Mwenyezi Mungu amewatakasa wazazi wa mtume mtukufu kwa kusema: (Na kugeuka kwako katika wasujudio) wanazuoni wamethibitisha kua wazazi wa mitume walikua na sifa ya kusujudu (unyenyekevu kwa Mwenyezi Mungu), na wala sio kweli kua baba yake nabii Ibrahimu (a.s) alikua ni Aazar, aliyekua anaabudu sanam pamoja na Namrudi, historia inathibitisha baba yake alikua anaitwa Taarikh, Yawezekana Aazar alikua Ammi yake, Ammi (baba mdogo) kumwita baba ni jambo la kawaida, na imekuja ndani ya Qur an tukufu, Mwenyezi Mungu anasema: (Je! Mlikuwapo yalipo mfika Yaaqub mauti, akawaambia wanawe: Mtamuabudu nani baada yangu? Wakasema: Tutamuabudu Mungu wako na Mungu wa baba zako, Ibrahim na Ismail na Is-haka…), Hapo Qur an imemwita Ismail kwa jina la baba, na wala hakua baba wa Yaaqub, alikua ni Ammi yake na imemwita Ibrahim kwa jina la baba wakati alikua ni babu yake.
Hivyo Aazar yawezekana akawa ni babu yake upande wa mama yake, kama wanavyo sema baadhi ya wana historia, na babu wa mama unamwita baba, na miongoni mwa dalili za kwamba alikua sio baba yake mzazi ni aya, ambayo Mwenyezi Mungu anasema (Na kumbuka aliposema Ibrahim kwa baba yake Aazar), akamuainisha kwa jina lake, angekusudiwa baba yake mzazi kusingekua na haja ya kumbainisha kwa jina lake (ingetosha kauli baba yake) lakini kwa kua aliye kusudiwa katika aya hiyo sio baba yake mzazi laziba abainishwe kwa jina lake Aazar.
Mtume mtukufu amesema wazi kuhusu usafi wa wazazi wao kutokana na vitendo vya kikafiri pale alipo sema: “Mwenyezi Mungu alipo taka kutuumba, aliweka nuru katika mgongo wa Adam, nuru hiyo ikawa inaangazia katika matumbo kisha ikahamia katika mgongo wa wasii wake Shith, na ilihusiwa isiingie ispokua katika matumbo ya wakina mama wema, wasia huu uliendelea kufanyiwa kazi, kwa kuhama nuru hiyo kutoka kwa watu wema kwenda kwa watu wema mpaka ikafika katika mgongo wa Abdulmutwalib ikagawika vipande viwili, nusu ikaingia kwa Abdullahi kisha kwa bi Amina na nusu ikaingia kwa Abuutwalib kisha kwa Fatuma bint Asadi”.
Adnaan aliwahi kubashiri katika khutuba zake kuhusu kudhihiri kwa mtume na akasema atatokana na kizazi chake na akahusia watu wamfuate. Mwanaye Muad, alikua hodari wa vita na mtu wa mapangoni, alipambana na Bani Israeel walio pinga tauhidi, yeyote aliye pigana naye alimshinda, alikua ni mtu wa tauhidi katika dini ya nabii Ibrahia (a.s), Mwenyezi Mungu alimuamuru Irmiya ambebe katika buraq ili kumuepusha na vitimbi vya Bakhatansar (kafiri), Mwenyezi Mungu alimuambia Irmiya kua: Mimi nitatoa katika mgongo wake mtume mwema atakaye kua ndio mwisho wa mitume. Irmiya akambeba na kumpeleka katika aridhi za Sham hadi alipo fariki Bahkatansar.
Sababu ya Nizaar kuitwa jina hilo, baba yake aliona nuru ya utume inawaka katika paji la uso wake, akalisha watu chakula kwa ajili yake, na akasema: Hakika nimetoa chakula kwa ajili yako.
Pia tumekatazwa kuwatukana Rabiah na Murrah, kwa sababu ni waumini, miongoni mwa maneno ya Mudhiri anasema kua: Atakaye lima shari atavuna majuto.
Ilyaasa bun Mudhir, alikua ni kiongozi wa watu wake na bwana katika ukoo wake, ilikua halihukumiwi jambo bila yeye, naye ni mtu wa kwanza kutoa zawadi ya shuka katika nyumba tukufu ya Maka (Kaaba) na mtu wa kwanza aliye gundua sehemu ya maqaamu Ibrahim (a.s) baada ya kisa cha maangamizo (gharka) ya nabii Nuhu (a.s), alikua ni muumini mwana tauhidi, limepokewa katazo la kumtukana, alipata heshima na hadhi ya baba zake, alikua na nuru ya mtume Muhammad (s..a.w.w).
“Kinana” Alikua shekh mtukufu mwenye mandari nzuri, waarabu walikua wanaenda kumtembelea kwa ajili ya utukufu wa elimu yake, alikua anawalingania kumuamini Mwenyezi Mungu, kufanya mema na kua na tabia nzuri, akiwahimiza kua; kumfuata Mwenyezi Mungu kutawazidishia utukufu, wala wasikadhibishe haki itokayo kwake, alikua akiwahimiza wanufaike na mafundisho, na alikua anapenda kula peke yake.
“Nadhir” Watoto wa juu yake hawaitwi Makuraishi, watoto wake mfano wa Maaliki na Fihri na wote walio zaliwa na Nadhir ndio Makuraishi, na wasio tokana na kizazi chake sio Makuraishi.
“Fihri” Alipigana na Hassaan bun Abdulkilaab alipokuja kutoka Yemen na jeshi kwa lengo la kuchukua jiwe jeusi katika Kaaba ili ajengee nyumba ya ibada huko Yemen, ndipo Fihri akaenda kupambana nae na akamshinda na kumteka, Hassaan akakaa miaka mitatu akiwa mateka hadi alipo lipa fidia ya mali nyingi ndio akaachiwa huru, wakati anarudi Yemen akafa njiani kati ya Maka na Yemen, waarabu walimuheshimu sana Fihri, hususan ilikua inadhihiri nuru ya utume usoni kwake, alikua na kauli maarufu kutoka kwake isemayo: “Kidogo kilicho mkononi kwako ni bora kuliko kingi usicho kua nacho hata kama ukiambiwa kitakua chako” na alikua mtu wa tauhidi.
Kaabi bun Luai aliendelea kumtaja mtume na kuwafundisha makuraishi kua atatokana na kizazi chake, na kuwataka wamfuate kwa kusema: “Sikieni tambueni na fahamuni, usiku unapo funika na mchana unapo pambazuka na aridhi ni tandiko na milima ni magingi na wa mwanzo na wa mwisho, yote haya yana mazingatio, unganisheni undugu wenu na msuluhishe mambo yenu, je mmesha ona aliye kufa akarudi au maiti ikajenga nyumba? Ipambeni haram yenu (Kaaba) na muitukuze na mshikamane nayo wala msiitenge, itakuleteeni habari kubwa, na atatokea mtume mtukufu, kisha akasoma beti zifuatazo:
Mchana, usiku na kutofautiana kwa matukio…
Sawa iwe imetokea kwetu au kwa wengine…
Yaendelea matukio hadi mwisho…
Na kwa neema ilo ongezwa kwetu na kusitiriwa…
Katika hali ya kughafilika atakuja mtume Muhammad…
Atasema habari zitakazo sadikishwa na wenye kuambiwa..
Kisha akasema:
Laiti ningemshuhudia nikamuitikia wito wake…
Ili familia inayo tafuta haki isisaliti…
Kutokana na utukufu wake na heshima aliyo kua nayo waarabu walianza kuhesabu tarehe kwa kifo chake, kisha baada ya tukio la mwaka wa tembo wakahesabu miaka kwa tukio hilo, kisha walihesabu miaka kwa tukio la kifo cha Abdulmutwalib, naye ndie mtu wa kwanza kuifanya siku ya Ijumaa kua ni siku ya kukusanyika kwa Makuraishi, katika zama za ujinga ilikua inaitwa Al uruba na baada ya kuja uislamu ikaitwa Amdhwaahu.
“Kilabu bun Murrah” Huyu ni babu wa tatu wa mama yake mtume na babu wa nne wa baba yake Abdullahi, alikua maarufu kwa ushujaa na nuru ya utume ilikua inaonekana katika uso wake.
“Kuswai” Ndiye aliye wakusanya watu wake na kuwataka wajenge pembezoni mwa Kaaba na kuishi hapo, na wakajenga milango maalumu katika Kaaba, ambayo ni: mlango wa bani Shaiba na wa bani Jamhu hali kadhalika mlango wa bani Makhzuum na mlango wa bani Saham, na wakaacha nafasi inayo tosha kuzunguka Kaaba. Hawa bani Kuswai (watu wa Kuswai) walijenga nyumba ya nadwa (bunge) kwa ajili ya kujadili mambo mbali mbali yanayo husu jamii yao, makuraishi waliheshimika kutokana na uzuri wa maoni yake, hadi akaitwa (Mujmia) mkusanyaji (kutokana na kuikusanya jamii yake na kua kitu kimoja).
Ulipo fika msimu wa hija aliwaambia makuraishi kua: “Huu ni msimu wa hija, na waarabu wamesikia mnayo fanya na nyie mnaheshima kubwa kwao, sijui utukufu ulio mkubwa zaidi kwa waarabu kushinda kulisha chakula, kila mtu atoe katika mali zake (kwa ajili ya kulisha chakula)”.
Wakakusanya mali nyingi, ulipo fika msimu wa hija, walichinja wanyama katika kila njia inayo ingia Maka mbali na wale walio chinjwa ndani ya Maka, na wakawasha moto katika eneo la Muzdalifa ili kila anaye kuja awaone.
Na wakapika chakula kingi siku za mina, waliendelea kufanya hivyo kila mwaka hadi ulipo kuja uislamu, chakula kinacho pikwa na mfalme siku za mina ni miongoni mwa athari za Quswai, na alikabidhiwa usimamizi wa nyumba tukufu ya Kaaba, baada ya kua madaraka hayo alikua nayo Halil ambaye binti yake alikua ni mama watoto wa Quswai.
Quswai alipata madaraka ya kua msimamizi mkuu wa Kaaba: kutokana na wasia wa Halil moja kwa moja kwake au kupitia mkewe, hivyo akalazimika yeye asimamie mambo ya Alkaaba kutokana na kushindwa kutekelezwa majukumu hayo na mwanamke, au Abuu Ghabshaan Khuzaai ndiye aliye husiwa na Halil awe kiongozi mkuu wa Alkaaba halafu Quswai akayachukua madaraka hayo kwa kulipa fidia ya ngamia.
Na haya ndio mapokezi sahihi kuhusu namna alivyo pata Quswai uongozi wa Alkaaba, na yanakubaliana na akili inayo hukumu utakatifu wa babu zake mtume mtukufu na mwisho wa mitume, tofauti na baadhi za riwaya zinazo dai alitoa fidia ya pombe, wakati pombe ni haramu katika dini zote.
Inawezekana kwa babu wa mtume aipe thamani pombe?!! Wakati anajua kua imekatazwa na anakataza watu wasiitumie?! Imepokewa kua alimuambia mwanae na watu wake kua: “Jiepusheni na pombe, hakika sio nzuri kwa miili na huaribu akili”, mtu kama huyu vipi ataweza kutoa fidia ya pombe? Tena alikua muazi zaidi katika kukaza pombe, katika kauli nyingine anasema: “Atakaye fanya mabaya kwake ni mazuri ataingia katika mabaya na atakaye mkirimu mtu muovu atamshirikisha katika maovu yake na ambaye hatabadilika kwa kufanyiwa ukarimu atabadilika kwa kufanyiwa maovu na atakaye tafuta mambo yaliyo juu ya uwezo wake atastahili kukosa na husuda ni adui aliye jificha”.
Amekusanya ukarimu na utukufu “Abdumunafu” bun Quswai, kutokana na hadhi yake na utukufu wake walikua anaitwa “Mwezi wa Bathaau” alikua msamehevu na mkarimu hadhulumu mali ya yeyote, hadi katika uhai wa baba yake akaitwa “Fayaadhu” pia huitwa Munafu; kwa sababu ya kuwa mtaratibu kwa watu na katika mambo yake hadi akapigiwa mfano wa pande mbili za aridhi, jina lake alikua akiitwa Abdu kisha likaongezwa Munafu, likawa “Abdu Munafu” haya ndio mapokezi sahihi.
Yaliyo andikwa na ibun Dahalani katika Siratu Nabawiyya kua mama yake alimtumikisha katika sanamu lililokua linaitwa Munafu, (ndio akaitwa Abdu Munafu) sio sahihi, hakuna shaka kuhusu utukufu wa mababa wa manabii na mama zao pia katika nyanja zote za uhai wao, kuanzia kuabudia masanamu na mambo mengine machafu, sio kweli kabisa yanayo semwa kua; miongoni mwa wazazi wa mitume kuna waliokua wanaabudu masanamu kwa ushahidi tulio eleza hapo awali.
Naye Buswiri ameashiria jambo hili alipo sema:
Bado utaendelea kua katika nyoyo za watu, wanakuchagua wakina mama na wakina baba. Hakika hakukua na sanamu aliyekua anaitwa Munafu, lakini aliopo ni sanamu aitwae Munatu kwa Taaun.
Kutokana na hili ibun Kalbi katika kitabu cha masanam amesema: “Sijui lilikua wapi hili sanamu? Na lilikua la nani? Na nani aliyelitengeneza”.
Hapa inabainika wazi kua kauli ya Baraqi na Zuberi isemayo kua mama yake alimtumikisha katika kuhudumia sanamu aliye kua anaitwa Munatu na akaitwa Abdu Munatu lakini makuraishi wakambadilisha na kumwita Abdu Munafu sio ya kweli.
Nyumba ya Abdumunafu ilikua ndio nyumba bora zaidi katika miji ya makuraishi, na katika uongozi wake alikua na upinde wa Ismail na bendera ya Nizaar, na miongoni mwa wasia wake uliokutwa umeandikwa katika mawe: aliwahusia makuraishi wamuabudu Mwenyezi Mungu na waunge udugu.
Mwanae Hashim alifata nyayo zake hadi akawashinda makuraishi wote na waarabu wa utukufu, alikua akiwapa chakula mahujaji kama alivyo kua akifanya baba yake, mwaka mmoja Hashim alienda Sham, akanunua unga na keki, akatengeneza mikate na akachinja mnyama, akapika chakula kingi watu walikula hadi wakashiba. Alikua analisha chakula wakati wote, wa dhiki au wa neema, alikua anasaidia wasafiri na anampa amani mwenye hofu, na unapoingia mwezi wa Dhulhijja alikua anasimama na kuegamia Alkaaba kwa mgongo wake na analingania watu kwa kusema:
“Enyi makuraishi; hakika nyie ndio mabwana wa waarabu, wenye muelekeo mzuri na utukufu mkubwa, na wenye nasaba ya kati na kati, hakika nyie ndio majirani wa nyumba ya Mwenyezi Mungu, Mwenyezi Mungu amewakirimu kwa kumtawalisha na amekuteueni kua majirani zake tofauti na wengine katika wana wa Ismail, hakika wanakujieni mazuwaru wa Mwenyezi Mungu na wanaitakasa nyumba yake hakika wao ni wageni wake, na wenye haki ya kuwakirimu wageni wa Mwenyezi Mungu ni nyie, wakirimuni wageni wake na mazuwaru wake, hakika wanakuja kutoka katika kila mji, katika mazingira magumu, naapa kwa mola wa nyumba hii lau kama nikiwa na mali nitaitoa yote, mimi natoa katika mali zangu za halali zisizo kua na hata chembe ndogo ya haramu, zisizo patikana kwa dhulma na hazija changanyika na kitu chochote cha haramu, anayetaka kufanya hivyo na afanye, nakuombeni kwa utukufu wa nyumba hii, mtu yeyote asitoe katika mali zake kwa ajili ya kuwakirimu wageni wa nyumba ya Mwenyezi Mungu isipokua mali safi, isiyo kua ya haramu wala ya unyan’ganyi”.
Walijitahidi sana kutekeleza jambo hili, walikua wanatoa mali zao na kuzitunza katika nyumba ya mikutano (daru nadwa).
Naye ndiye mtu wa kwanza aliye weka utaratibu wa safari mbili za makuraishi; safari ya Yemen na safari ya Sham, akachukua kutoka kwa wafalme wa Roma na Ghasani vitu wanavyo vitegemea, biashara ya makuraishi haikua ya Maka na vitongoji vyake tu walifanya biashara na watu wa nje pia, walikua wakinunua na kuuza, hadi Hashim akawa anasafiri kwenda Sham na akawa anafikia kwa Kaisar (mfalme wa Sham), Kaisar alifurahishwa sana na uzuri wa tabia za Hashim pamoja na ukarimu wake, hakumuwekea kikwazo chochote na akaidhinisha kufanya nae biashara, halafu akampa mkataba wa amani, nyumba ya Hashim ilichanganyika na watu wa aina mbali mbali, alikua wakati wa masika anenda Yemen na wakati wa kiangazi anaenda Sham, wakashiriki pamoja naye katika biashara wakuu wa makabila ya waarabu na wafalme wa Yemen na Sham, akawa anasafiri na ngamia zao akizichanganya katika ngamia zake akiuza mizigo yao pamoja na mizigo yake kisha anawapa faida, akawatosheleza gharama ya safari na wao wakamuhakikishia ulinzi na usalama katika safari zake, jambo hili lilikua na faida kwa wote wawili, aliye bakia nyumbani anapata faida na aliye safari yupo katika amani, makuraishi wakaishi katika hali hiyo, wakapata heri na baraka nyingi kutokana na utukufu wa Hashim, na hii ndio maana ya mazowea ya safari (ilaafi) yaliyotajwa ndani ya Qur’an tukufu.
Katika khutuba zake alikua anasema: “Enyi watu sisi ni Aali Ibrahim, na familia ya Ismail, ni wana wa Nadhri bun Kinana, wana wa Quswai bun Kilabi na ndio viongozi wa Maka, wakazi wa haram tuna uongozi na maamuzi, tuna haki ya kusikilizwa na kutiiwa, isipokua mtu atakapo amrisha mabaya au kuvunja undugu.
Enyi wana wa Quswai nyie ni sawa na tawi la mti yeyote atakae likata mwenye mti lazima atahuzunika, na jambia ambalo halitunzwi isipokua katika hara lake, na mlengaji mshale anaye chomwa na mshale wake na wenye kutulia katika wema na kujitoa katika uovu.
“Enyi watu, upole ni utukufu na mwenye kusubiri hupata, wema ni hazina, ukarimu ni hakiba, ujinga ni ukosefu wa akili, siku zinazunguka, na muda unaenda, mtu hunasibishwa na vitendo vyake, na huchukuliwa kutokana na anayo yafanya, fanyeni mambo mema mtapata sifa nzuri, achene maovu mtasalimika na waovu, wakirimuni mnao kaa nao mtadumisha vikao vyenu, wahamini watu mnao ishi nao watapenda kua jirani zenu, zitakaseni nafsi zenu mta aminiwa, shikamaneni na tabia njema humuinua mtu, jiepusheni na tabia mbaya huvunja utukufu na hubomoa ukarimu, hakika kelele ya mjinga ni nyepesi kuliko ujinga wake, kichwa cha familia hubeba mizigo yake, nafasi ya mtu mwema ni kutoa nasaha kwa watakao nufaika nazo”.
Nuru ya utume ilionekana usoni kwake, uso wake ulikua unatoa nuru katika usiku wa giza, hakupita katika jiwe wala mti ispokua ulisema: tunakubashiria ewe Hashim atapatikana kutokana na kizazi chako mmbora wa viumbe wa Mwenyezi Mungu ambaye ni Muhammad mwisho wa mitume.
Baba yake –Abdumanafi- alimuhusia kama alivyo muhusia baba yake Quswai: asiweke nuru ya utume ispokua katika matumbo ya wanawake wema na akakubali kutekeleza usia huo.
Tulisema kua nuru hiyo walirithi kutoka kwa nabii Adam (a.s), kutokana na utukufu wake wafalme wa Roma na Farsi walitaka kumuozesha Hashim lakini alikataa, hadi alipo ambiwa katika ndoto kua: “kamuoe Salma bint Amru bun Labid bun Hadath bun Zaid bun Aamir bun Ghanam bun Maazin katika ukoo wa Bani Najaar, hakika huyo ni mwanamke mtakasifu na ametokana na watu watakasifu, hafanani na mwanamke yeyote, kamlipie mahari kubwa hakika utapata kutoka kwake mtoto atakae zaa mtume”. Hashim pamoja na ndugu yake Mutwalib na watoto wa ammi yake wakaenda Madina kuitafuta familia huyo, huku wamebeba bendera ya Nizaar na wamevaa nguo za kifahari na ngao.
Walipo fika kwa watu walio wafuata Mutwalib bun Abdulmanafi akasema: “Sisi ni wageni kutoka katika nyumba ya Mwenyezi Mungu mtukufu, na maeneo matakatifu, watu hutembea kuja kwetu, na nyie mnafahamu utukufu wetu, Mwenyezi Mungu ametuteua kwa nuru yake ing’aayo, na sisi ni wana wa Luai bun Ghaalib, nuru hii ilihamia kwa Abdumanafi kisha ikahamia kwa ndugu yetu Hashim, nuru hii imeanzia tangu kwa Adam (a.s), Mwenyezi Mungu ameielekeza kwenu, tumekuja kumposa binti yenu”.
Amru (Abuu Salma) akakubali posa yao, na wakalipa mahali kama walivyo panga na kijiandaa.
Hashim alipo muoa bibi Salma akapata mimba na kumzaa Abdulmutwalib, ile nuru ya utume ikahamia kwa Abdulmutwalib, na aliendelea kuona bishara za kuzaliwa kwa mmbora wa viumbe ambazo zilikua zikimshangaza, Hashim akamfahamisha kuhusu swala la kuzaliwa kwa mtume kutokana na wao.
Alipo zaliwa Abdulmutwalib watu walikua wanamwita (Shaibatul Hamdu) kutokana na watu kumsifu sana, alikua ni kimbilio la makuraishi katika shida zao na walirejea kwake katika mambo yao, alikua mtukufu katika watu wake na mbora wao kwa ukamilifu na hadhi naye ni katika viongozi wakuu kabisa wa makuraishi.
Alianzisha vitu ambavyo vimepasishwa na uislamu:
- Aliharamisha watoto wa kiume kuwarithi (kuwaoa) wake wa baba zao.
- Akaweka sheria ya kutoa asilimia tano katika mali ya kuokota, au inayo patikana aridhini.
- Aliweka fidia ya kuua kua ngamia mia moja.
- Makuraishi hawakua na idadi maalumu ya kutufu, yeye akaweka sheria ya kutufu mara saba.
- Aliweka sheria ya kukata mkono wa mwizi.
- Akaharamisha pombe na uzinifu.
- Akaharamisha kutufu ukiwa uchi.
- Akakataza kuapia kwa mizimu.
- Akakataza kula mnyama aliyechinjwa kinyume na sheria.
Miongoni mwa maneno yake ya hekima ni: “Mtu mwenye kufanya dhulma hatoki hapa Duniani hadi yamfike mabaya aliyo fanya, hakika baada ya nyumba hii kuna nyumba ambayo mtu mwema hulipwa kwa wema wake na muovu hulipwa kwa maovu yake, iwapo mtu mwenye kufanya dhulma hatalipwa hapa Duniani basi ajue adhabu yake imeandaliwa akhera”.
Alikua anaitwa “Fayaadh” kutokana na wingi wa ukarimu wake, alikua anakula na kila mtu hadi wapita njia, na baada ya hapo alikua anapeleka chakula chake hadi katika mlima wa Abuu Qubais ili wapate kula ndege na wadudu.
Kutokana na utukufu mkubwa alio kuanao, alikua analala katika Kaaba, na hakuna mtu yeyote aliye wahi kulala humo zaidi yake, alikua hakai na yeyote ndani ya Kaaba isipokua mtume mtukufu, walikua baba zake wadogo wakitaka kumtoa mzee Abdulmutwalib anawakemea sana na kuwaambia: “Hakika huyu anajambo lenye ufalme mkubwa”.
Hakuna ajabu katika hili, hakika alikua ni wasii miongoni mwa mawasii na msomi mkubwa wa vitabu vya Mwenyezi Mungu, Abuutwalib aliwahi kumuambia mtume (s.a.w.w) kua: “Baba yangu alikua anasoma vitabu vyote”. Na alisema: “Hakika katika kizazi changu kuna mtume, ninatamani kufika zama atakazo dhihiri niwe miongoni mwa waumini wake, atakaye mdiriki katika watoto wangu amuamini”.
Amirul mu-uminina (a.s) anasema: “Wallahi hakuwahi kuabudu sanamu baba yangu wala babu yangu Abdulmutwalib, Abdulmanafi wala Hashim, hakika walikua wanamuabudu Mwenyezi Mungu, waliswali kwa mujibu wa dini ya Ibramimu na walishikamana nayo”.
Abuutalib alikua ni bwana wa waarabu alifanana na baba yake Shaibatul hamdu, mjuzi wa mafunzo ya mitume, na alikua mjuzi wa habari za uma zilizo pita kwa sababu alikua ni miongoni mwa mawasii, na muaminifu wa usia wa mitume hadi alipo ufikisha kwa mtume (s.a.w.w). inaendelea..
KUZALIWA NA MALEZI YAKE
Hakuna nasaba (ukoo) mzuri hapa duniani kama nasaba yake, anatokana na familia ya Alawiyya, ambayo ni familia bora na tukufu zaidi kwa pande (nyanja) zote, familia inayo julikana kwa kujitolea katika mambo ya kheri, na imeangazia uhai wa watu wote kwa imani na uchamungu, na hizi ni sifa chache miongoni mwa sifa alizo nazo mwezi wa Bani-hashimu (Abulfadhili Abbasi).
KUZALIWA NA MALEZI YAKE
Hakuna nasaba (ukoo) mzuri hapa duniani kama nasaba yake, anatokana na familia ya Alawiyya, ambayo ni familia bora na tukufu zaidi kwa pande (nyanja) zote, familia inayo julikana kwa kujitolea katika mambo ya kheri, na imeangazia uhai wa watu wote kwa imani na uchamungu, na hizi ni sifa chache miongoni mwa sifa alizo nazo mwezi wa Bani-hashimu (Abulfadhili Abbasi).
Sifa zake
Ni miongoni mwa hekima ya Mwenyezi Mungu mtukufu kwa walii wake, asili ya ukhalifa, mbora wa mawasii kumpatia sifa ya nguvu na ushujaa na moyo wa kujitolea na utukufu, na uzuri wa maumbile, ukarimu na upole, kuwahurumia wanyonge, mtazamo wenye bashasha, mwanga katika uhai wake, uso mzuri na katika paji lake kuna nuru ya imani.
Zilipo kusanyika kwake sifa za uzuri wa sura na tabia ndipo akaitwa “Mwezi wa bani Hashim” alikua mzuri kushinda wazuri wote, anapendeza machoni mwa kila mtu, kanakwamba malaika katika ulimwengu wa binadamu, alikua mtu wa pekee duniani, kama nuru ya mwezi inavyo shinda kila nyota, na haya ndio maelezo ya wapokezi:
“Abbasi alikua mtu mwenye umbo kubwa na mzuri, anapopanda farasi miguu yake hukanyaga chini, alikua akiitwa: Mwezi wa bani Hashim”.
Riwaya ya mahkiyya katika kitabu cha Maqaatil Twalibina imemsifu kua: “Baina ya macho yake kuna athari ya kusujudu”.
Madaaini anasema: “Alinisimulia Abuu Ghassani Haruna bun Saadi, kutoka kwa Kassim bun Asbagh bun Nabata, alisema: Niliona mtu ana uso mweusi katika bani Abaan bun Daaram, na nilikua namfahamu kua ni mzuri na mweupe sana, nikamuambia: Nilitaka kukupotea? Akasema: Mimi niliua mtu mwenye nywele nzuri na baina ya macho yake kuna athari ya sijda aliye kua pamoja na Hussein, tangu nimuue kila nikilala huniijia na kunikokota hadi katika moto wa jahannamu na hunitupa humo, mimi hupiga kelele hadi kila aliye hai husikia kelele zangu. Akasema: Aliye uawa ni Abbasi bun Ali (a.s)”.
Kuna riwaya ya Sibtu bun Jauzi kutoka kwa Hisham bun Muhammad kutoka kwa Qassim bun Asbagh Almujashii anasema: “Wakati vichwa vilipo letwa Kufa, kulikua na mpanda farasi ameweka katika kichwa cha farasi yake kichwa chenye sura nzuri, kama vile mwezi ung’aao, huku farasi akifurahia kubeba kichwa hicho, anapo tingisha kichwa chake kichwa cha mwanadamu kinagusa aridhini, nikauliza: Hiki ni kichwa cha nani? Nikajibiwa: Kichwa cha Abbasi bun Ali (a.s), na wewe ni nani? Akasema: Mimi ni Harmala bun Kaahil Asadiy.
Akasema: nikakaa siku kadha nikamkuta Harmala uso wake umekua mweusi kushinda mkaa, nikasema: Siku niliyo kuona umebeba kile kichwa hakuna muarabu aliyekua na uso mweupe zaidi yako, lakini leo hii hakuna mtu mwenyesura mbaya na mweusi zaidi yako, akalia (Harmala) na akasema: Wallahi toka nibebe kichwa kile hadi leo kila unapo ingia usiku hunijia watu wawili na kunipeleka hadi katika moto mkali na hunitupia humo ndio unaona nimekua hivi nilivyo. Na alikufa akiwa katika hali mbaya sana”.
Riwaya mbili zote zinaonyesha aliye uawa alikua ni Abbasi bun Ali (a.s) kwa kumtaja kwa sifa ya kijana mwenye sura nzuri, siku anauawa alikua na miaka thelathini na nne, na hakuna kijana aliye kua na sura nzuri zaidi yake, wala historia haijasema kama alikua sawa na Qais bun Saadi bun Abada aliye kua na nyele nyingi hadi usoni kwake.
Katika kitabu cha Daru salaam cha Allama Nuriy juzu ya kwanza ukurasa wa 114 na kitabu cha Kibriti Ahmaru juzu ya tatu ukurasa wa 52 vinashuhudia swala hili, huku kitabu cha Qamaru bani Hashim ukurasa wa 126 kinasema kilikua kichwa cha Abbasi mdogo bila kutaja ushahidi, halafu kikatilia shaka kuhudhuria kwake Twafu na kuuawa katika aridhi hiyo, hii ni sawa na alivyo kadiria kua aliye uawa ni ndugu wa Abbasi, aitwaye Othmani wakati siku ya kuuawa kwake alikua na miaka ishirini na moja, au Muhammad bun Abbasi aliye uawa kwa mujibu wa riwaya ya ibun Shahari Aashubu, hizo zote ni ijtihadi tu.
Pengine mtazamo sahihi unaweza ukawa ule alio pokea Swaduuq kutoka katika riwaya ya ibun Jariri Twabari inayo sema kua aliye uawa ni Habibu bun Mudhahiri.
Swaduuq anasema: “Kwa isnadi hii kutoka kwa Omari bun Said, kutoka kwa Qassim bun Asbagh bun Nabata, anasema: alitujia mtu kutoka kwa bani Abaan bun Daaram miongoni mwa walio shuhudia mauaji ya Imamu Hussein (a.s), alikua mtu mzuri mweupe sana, nikamuambia: Nilitaka kukupotea kwa namna rangi yako ilivyo haribika, akasema: Niliua mtu miongoni mwa wafuasi wa Hussen, baina ya macho yake kuna athari ya sajda na nikabeba kichwa chake.
Qassim akasema: Nilimuona akiwa katika farasi yake huku ametungika kichwa juu ya shingo ya farasi na kambana farasi kwa miguu, akasema: Ewe mwanangu yaliyo mtokea ni makubwa, alinihadithia kua: “toka nimuue mtu yule kila nikilala ananijia usingizini, ananishika begani na kuondoka pamoja na mimi hadi katika moto wa jahanam, ananitupa ndani ya moto huo kisha napiga kelele, akasema: jirani yake alisema, usiku hatupati usingizi hata kidogo kutokana na kelele zake, tukawauliza vijana wa mtaani kwake na wao akaenda kumuuliza mke wake, akasema: mmesema kweli hakika bwana huyu ameidhuru nafsi yake”.
Riwaya zote tatu kutoka kwa Qassim bun Asbagh bun Nabata zunathibitisha mambo yaliyo tokea kutokana na kichwa hicho kitakatifu.
Riwaya ya Swaduuq inathibitisha kua aliye uawa ni mtu mzima na sio kijana mdogo, na ni miongoni mwa watu wa Imamu Hussein (a.s) hakuna shaka juu ya hilo, ikiwa tutakubaliana na ibun Jariri kua kichwa kilicho tungikwa juu ni cha Habib bun Mudhahir – wakati wanahistoria hawaja taja tukio hilo zaidi yake- tunaweza kusema kuna utata baina ya riwaya mbili, hususan zinapo kua zinaondoa uwezekano wa kunasibishwa kichwa kile na Abbasi, inakua vigumu kupata usahihi bila kutumia kielelezo cha wazi.
Ibun Jariri anasema katika jz6 uk252 katika kitabu chake cha historia: “Walipigana vita kali, mtu mmoja katika bani tamim akampiga (Abbasi) panga la kichwa akamuua, mtu huyo anaitwa Badil bun Swarim katika bani Aqfaan, kisha mtu mwingine katika bani Tamim akamchoma, (Abbasi) akaanguka, alipo taka kuinuka; Haswim bun Tamim akampiga panga la kichwani, akaanguka, Tamimy akamuendea na akatikisa kichwa chake, Haswin akamuambia, mimi nimeshiriki katika kumuua! Mwingine akasema: Wallahi hakuna aliye muua zaidi yangu, Haswin akasema: Nipeni kichwa chake nikibebe juu ya farasi yangu ili watu wajue kua nimeshiriki katika kumuua, kisha utakichukua wewe na kukipeleka kwa ibun Ziyadi, mimi sina haja na malipo ya kumuua utakayo pewa, akamkatalia, watu wakaingilia kati kuwasuluhisha, akampa kichwa cha Habib bun Mudhahir, akazunguka nacho kwa wapiganaji kikiwa juu ya shingo la farasi wake, kisha akamrejeshea. Walipo rudu Kufa kichwa cha Habib bun Mudhahir kikabebwa na mtu mwingine akakiweka katika shingo la farasi wake, wakaenda kwa ibun Ziyadi, ndipo Qassim ibun Habib akakiona, akaanza kufuata farasi inako elekea, ikiingia katika Qasri la ibun Ziyadi na yeye anaingia, ikitoka na yeye anatoka, mpanda farasi akawa na wasiwasi, akamuuliza! Una nini ewe kijana mbona unanifuata fuata? Akajibu yule kijana, sina kitu! Mpanda farasi akasea: hapana lazima uniambie kwa nini unanifuata fuata? Yule kujana akasema: Hiki kichwa ulicho beba ni cha baba yangu je unaweza kunipa nikamzike? Mpanda farasi akasema: Ewe kijana mfalme hata kubali kizikwe, na mimi natarajia malipo makubwa kutoka kwa mfalme ya kumuua huyu. Yule kijana akasema: Lakini Mwenyezi Mungu hatakulipa kwa jambo hilo ispokua adhabu kali, hakika kumuua kwako ni heri kwake, kisha akaanza kulia.
Kijana akakaa muda mrefu akimfuatilia muuaji wa baba yake na akitafuta mtu anaye weza kulipiza kisasi cha kuuliwa baba yake, zilipo fika zama za Mus’abu bun Zubair, akajiunga na jeshi la Mus’abu, walipo kwenda vitani mara akamuona muuaji wa baba yake, akaanza kumnyatia hadi akamsogelea ndipo akampiga panga na kumuua..”.
Katika riwaya ya Swaduuq, Qassim anamuuliza baba yake kuhusu mpanda farasi aliye beba kichwa, riwaya inasema: “Nikamuambia baba: Kama angeinua kichwa… hadi mwisho”.
Inamaanisha Asbagh alikua hai siku hiyo, pia haiko wazi kuhusu kuhudhuria kwake au kuto hudhuria katika tukio zima, pamoja na kua alikua mpenzi mkubwa wa Ahlulbait (a.s) na mfuasi mzuri wa Amirulmu-uminina na watoto wake watakasifu (a.s), pili kushuhudia kwake tukio hili inamaanisha hakufungwa na ibun Ziyadi kama walivyo fungwa wenzake, na dalili za wazi zinaonyesha kua mtu huyo aliuawa kabla ya tukio hilo.
Hivyo ile sentensi isemayo: “Nikamuambia baba” haijulikani imetoka wapi. Inawezekana imeongezwa baada ya kuzushiwa tuhuma, kama ilivyo kuja katika kitabu cha Laaiy Masnuuah jz1 uk213, baada ya kutaja hadithi ya Asbagh bun Nabata kutoka kwa Abuu Ayubu Answariy “Kua wao waliamrisha kuwaua walivunja ahadi, waovu na waliojitoa kwa Ali”. Akasema: hadithi sio sahihi Asbagh aliachwa kwa sababu sio shujaa.
Katika kitabu hichohicho ukurasa wa 195 ametaja hadithi kutoka kwa ibun Abbasi isemayo: “Mashujaa siku ya kiama ni mtume Swaleh na Hamza na Ali”, watu wa hadithi wamesema sio sahihi kukusanya kitu kisijo julikana na kitu kinacho julikana.
Wamezushiwa kila aina ya tuhuma kwa sababu tu ya kua kwao wafuasi wa imamu Ali (a.s) (Shia), yaliyo andikwa katika vitabu vyao yanashuhudia jambo hilo, katika muhtasari huu hatuwezi kuandika habari zote, yatosha kurejea aliyo andika Sayyid Alamah Muhammad bun Abuu Aqiil katika kitabu cha: “mambo mema ya Ahli jarhi wa ta’adil” ukurasa wa 40 mlango wa pili, ameelezea wafuasi wa Ahlulbait ambao wametukanwa kwa sababu tu ya kumtawalisha kwao Amirulmu-uminina Ali na watoto wake (a.s).
Kaka zake
Hakika kuna haja kubwa ya kuijua historia ya Abulfadhil (a.s) na kuwatambua kaka zake watukufu, hakika miongoni mwao kuna alio karibu nao zaidi mbali na kuunganishwa kwa undugu, nao ni maimamu wawili wa umma wakiwa wamesimama au wamekaa.
Pamoja na kwamba wote wamezaliwa na Kiongozi wa waumini wana utukufu mwingi zaidi, utukufu wao hauelezeki, kama inavyo onekana katika maneno yake (a.s) siku ya kikao cha shura: “Nakuulizeni kwa jina la Mwenyezi Mungu mtukufu, hivi miongoni mwenu kuna mwenye wajukuu mfano wa wajukuu wangu Hassan na Hussein watoto wa Mtume wa Mwenyezi Mungu na mabwana wa vijana wa peponi (yupo mwenye nao) zaidi yangu”? wakasema: hakuna.
Pia Imamu Ali (a.s) alijifaharisha kwa Muawiya kupitia watoto hao wawili pindi Muawiya alipo muandikia akijisifu kua: “Baba yangu alikua mtu mtukufu katika zama za ujinga, na mimi nimekua mfalme katika uislamu, mkwe wa Mtume wa Mwenyezi Mungu, Mjomba wa waumini na muandishi wa wahyi”.
Kiongozi wa waumini (a.s) akamuandikia beti saba, akaeleza kua yeye ni mkwe wa Mtume (s.a.w.w), Ammi yake ni bwana wa mashahidi, ndugu yake aliruka pamoja na Malaika kwenda peponi, alimtangulia katika uislamu, alipewa kiapo cha utii (siku ya Ghadiir) na kwamba watoto wake ni wajukuu wa Mtume (s.a.w.w).
Hivyo undugu wa Abbasi kwao ni bora zaidi kabla ya kuangalia utukufu mwingine, ukiongeza na namna alivyo nufaika nao, kwa kusoma kwao na kupata maarifa makubwa kuhusu Mola.
Na miongoni mwao kuna ambao walikua pamoja zaidi, waliokua pamoja zaidi katika watoto wa kiongozi wa waumini (a.s) ni Maimamu wawili, Abbasi, Muhammad bun Hanafiyya na Omari Atwiraf.
Miongoni mwao wapo walio shiriki katika harakati ya Twafu. Na wapo ambao anaukaribu nao zaidi katika upande wa mama, na wapo ambao wamefanana nae majina.
Jumla ya watoto wa kiume wa Kiongozi wa waumini ni kumi na sita, ambao ni:
Hassan, Hussein na Muhsin, mama yao ni mbora wa wanawake wa duniani (Bibi Fatuma a.s).
Abbasi, Abdullahi, Jafari na Othmani, mama yao ni Ummul-Banina.
Omari Atwiraf na Abbasi mdogo (Asghar), mama yao ni Swahbaau.
Muhammad mdogo (Asghar), mama yake ni Umaamah bint Abu-Aaswi.
Yahya na Aun, mama yao ni Asmaa bint Umais.
Abdullahi na Abubakar, mama yao ni Laila bint Masud.
Muhammad wa kati (Ausat), mama yake ni Ummu Walad.
Maimamu wawili ni vizuri kutiririka katika kuelezea utukufu wao na utakatifu walio pewa, uweledi wao katika elimu ulikua wa hali ya juu kabisa.
Amma! Muhsin, Mtume (s.a.w.w) ndiye aliye mpa jina hilo, akiwa bado tumboni kwa mama yake, baada ya kufariki (Mtume), ujauzito wa bibi Fatuma (a.s) uliharibika ukiwa na miezi sita, kuna riwaya nyingi zinazo elezea tukio hilo zimeandikwa na Ibun Twausi katika kitabu cha (Twaraf) na katika vitabu vingine pia.

Abbasi (a.s) upande wa baba yake alikua na dada kumi na nane, wapo waliokufa wakati wa uhai wa baba yake, kama vile Zainabu mdogo (sughura), Jumana, Umaama, Ummu Salama na Ramla mdogo (sughura). Na wengine historia haijataja kuolewa kwao.
Walio tajwa kuolewa kwao ni: Aqilah Zainabu mkubwa (kubra), aliolewa na Abdullahi bun Jafari Twayaar, akamzaa Jafari mkubwa (akbaru), Abbasi, Ali maarufu kwa jina la Zainabiyyu na Aun mkubwa (akbaru) aliye uawa Karbala wakati familia ya Abutwalib ilipoingia katika uwanja wa vita.
Na Ummu Kulthum, aliye ozeshwa na Hussein kwa mtoto wa Ammi yake Qassim bun Muhammad Twayaar.
Na Ruqayya akaozeshwa kwa mtoto wa Ammi yake Shahidi Muslim bun Aqiil, na alimzaa Abdullahi, Ali na Muhammad.
Katika cha Umda kinasema Muslim alimuoa Ummu Kulthum mtoto wa Ali (a.s) akamzaa Hamida, aliye olewa na mwanachuoni mtukufu Abdullahi bun Muhammad bun Aqiil bun Abutwalib, au mwanae Muhammad alioa ndugu wawili. Na hili halifanyiki ispokua baada ya kufa mmoja wao; kwani hairuhusiwi kukusanya ndugu wawili.
Fatuma aliolewa na Abuu Saidi bun Aqiil, akamzaa Hamida. Na Khadija akaolewa na Abdurahmaan bun Aqiil na akamzaa Saidi. Na Ummu Haani akaolewa na Abdullahi mkubwa bun Aqiil, akamzaa Abdurahmaan na Muhamad.
Ummu Hassan akaenda kwa Ju’uda bun Habirah Makhzumiy, Na umaamah akaenda kwa Swalbi bun Abdullahi bun Nufail bun Haarith bun Abdulmutwalib, akamzaa Nafisah.
Baba zake
Karibu ndugu msomaji tuangalie kwa ufupi kuhusu uhai wa baba wadogo wa Abulfadhil (a.s), ambao ndio matawi ya mti wenye mizizi madhubuti na matiwi marefu hadi mbinguni, hakika baba wadogo wana vinasaba ambavyo humuathiri mtoto, imepokewa katika hadithi kua: “Kama jinsi mtoto hufanana na wajomba zake vilevile hufanana na baba zake”.
Kabla ya kueleza vipawa walivyo tunikiwa na Mwenyezi Mungu, tumuangalie kwa ufupi Ammi yake Mtume (s.a.w.w) aliye kua akijifahari naye Mtume (s.a.w.w) katika maeneo mbalimbali, naye ni Hamza bun Abdulmutwalib.
Nani atakaye kujuza ni nani Hamza? Hivi unajua kitu gani alicho maanisha mtume pale alipo mwita kwa jina la sifa “Simba wa Allah na sima wa Mtume wake”? je! Alikusudia nguvu na ujasiri peke yake?
Hapana; Hakika Mtume (s.a.w.w) ni mfaswaha zaidi katika kutamka dhwadi (mfaswaha zaidi wa lugha), maneno yake yako juu ya kiwango cha ujuzi wa wataalamu, lau kama angekusudia maana ya ushujaa ingetosha kutumia neno la “Simba” bila kuongeza neno Allah (s.w.t) na neno Mtume wa Mwenyezi Mungu.
Kwakua Mtume ameongeza dhati ya Allah lazima kuwe na kusudio lingine, nalo ni msisitizo wa kua ushujaa na nguvu zake zinatumika kunusuru ujumbe wa Mwenyezi Mungu mtukufu na ulinganiaji wa bwana Mtume (s.a.w.w), na hilo ndio jambo kubwa zaidi kuliko yote, hivyo alikua nguzo muhimu ya dini na kinara wa uongofu, ndio akapata heshima kubwa aliyo pewa na Mwenyezi Mungu mtukufu, heshima ambayo hataipata shahidi mwingine yeyote, hii inatokana na ukamilifu wa imani yake tukufu.
Haya yako wazi katika kitabu cha “Twaraf” kilicho andikwa na Sayyid bun Twausi: Mtume wa Mwenyezi Mungu alimuambia Hamza usiku ambao kesho yake aliuliwa: “Hakika wewe utatoweka sana (utakufa), utasema nini kama Mwenyezi Mungu akikuuliza kuhusu sheria za uislamu na mashariti ya imani”?
Hamza akalia na akasema: Nielekeze na unifahamishe.
Mtume akasema: “Ushuhudie kua Mwenyezi Mungu ni mmoja, na Muhammad ni Mtume wake, na Ali ni Walii wake, na maimamu watatokana na kizazi cha Hussein, na Fatuma ni mbora wa wanawake wa ulimwenguni, na hakika Jafari mtoto wa ndugu yako ataruka pamoja na Malaika, na kwamba Muhammad na watu wa nyumbani kwake ni viumbe bora”.
Hamza akasema: “Nimeamini na nimesadikisha”.
Kisha Mtume akasema: “Na ushuhudie kua wewe ni Bwana wa Mashahidi, na simba wa Mwenyezi Mungu na mtume wake”.
Hamza alipo sikia hivyo, akashtuka na akaanguka chini kisha akamkumbatia Mtume na akabusu macho yake na akasema: Nashahadia kwako mambo haya na nitashahadia kwa Mwenyezi Mungu, na Mwenyezi Mungu atoshwa kua shahidi.
Tukichambua hadithi hiyo, tutaona nafasi kubwa aliyo nayo Hamza katika dini na imani, kama si hivyo itakua hakuna faida ya shahada hii wakati amesha itamka tangu akiwa Maka, alipo muamini Mwenyezi Mungu mmoja na Mtume wake, lakini Mtume (s.a.w.w) alitaka kuonyesha utukufu wake na ukamilifu wa imani yake, nako ni kukubali uongozi wa kiongozi wa waumini (Ali buna Abutwalib) na kwamba watoto wake watakasifu (a.s) ni makhalifa wa babu yao Mtume (s.a.w.w).
Pia ananafasi nyingine ambayo hakuna anaye weza kuifikia, nayo ni kukiri kua Hamza ni Bwana wa Mashshidi, na kwamba yeye ni simba wa Mwenyezi Mungu na Mtume wake, na mtoto wa ndugu yake ataruka pamoja na Malaika kwenda peponi, jambo hili hawajalazimishwa waja zaidi ya kutambua utakasifu wa watu wa nyumba ya Mtume, hakika lilifanyika kwake tu kama sehemu ya kuonyesha utukufu wake na kufunguliwa na kupewa yakini.
Tukiangalia namna maimamu wanavyo mchukulia, na wao wanatambua zaidi watu, walikua wanamtumia kama hoja kwao mbele ya maadui zao namna alivyo uawa kishahidi kwa ajili ya dini, kama walivyo kua wakitumia hoja ya ukaribu wao na bwana Mtume (s.a.w.w), pamoja na kwamba kuna watu waliojitolea na wakapigana kwa ajili ya kutafuta radhi za Mwenyezi Mungu mtukufu, Amirulmu-Uminina anasema : “Hakika watu wetu waliuawa kishahidi katika njia ya Mwenyezi Mungu miongoni mwa muhajirina, na kila mtu ni mtukufu, ilifikia wakati wanapo uawa mashahidi wawili panasemwa Bwana wa Mashahidi, ni yeye peke yake (Hamza) ndiye aliye somewa takbira sabini na Mtume (s.a.w.w) wakati wa kuswaliwa kwake”.
Katika siku ya Shura (Imamu Ali alimtumia kama hoja kwake) pale alipo seama: “Namshuhudia Mwenyezi Mungu kwenu, hivi katika nyie kuna mtu mwenye ammi sawa na Hamza! Simba wa Mwenyezi Mungu na mtume wake”?
Imamu Mujtaba (a.s) anasema katika baadhi ya hutuba zake kua: “Miongoni mwa waliomuamini Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w) ni Ammi yake Hamza na mtoto wa Ammi yake Jafari, mashahidi wawili hao walipigana vita vingi pamoja na maswahaba wengine wa Mtume, Hamza akafanywa kua Bwana wa Mashahidi”.
Naye Bwana wa Mashahidi Abu Abdillah katika siku ya Twafu alisema: “Hakua Hamza Bwana wa Mashahidi ni Ammi wa baba yangu”?
Zimepokewa riwaya nyingi zinazo elezea utukufu wake, hata Mtume wa Mwenyezi Mungu aliendelea kusema utukufu wake, na kuwajulisha muhajirina na answari upekee wa Simba wa Mwenyezi Mungu na Mtume wake, ili asipatikane muislamu atakaye tilia shaka utukufu alio pewa na Mwenyezi Mungu, Mtume (s.a.w.w) anasema: “Enyi Answari, enyi bani Hashim, enyi bani Abdulmutwalib, mimi ni Muhammad mjumbe wa Mwenyezi Mungu, tambueni mimi nimeumbwa kwa udongo ulio rehemewa, tukiwa wanne katika nyuma (familia) yangu: mimi, Ali, Hamza na Jafari”.
Lengo la Mtume katika maneno hayo ni kuonyesha utukufu wa Ammi yake na mtoto wa Ammi yake, ndio maana hajaendelea kutaja uumbwaji wa maimamu wala wafuasi wao walio umbwa kutokana na mabaki ya udongo wao (kama ilivyo kuja katika kitabu cha Swahihul- Aathaar), amejitaja mwenyewe na wasii wake kwa sababu wao ni miongoni mwa misingi ya uislamu na imani.
Kiongozi wa Waumini siku ya kufunguliwa kwa mji wa Basra alielezea utukufu wa watu saba miongoni mwa watoto wa Abdulmutwalib, akasema: “Hakuna atakaye kataa utukufu wao ispokua kafiri, na hakuna asiye wajua ispokua mpumbavu, nao ni: Mtume Muhammad, wasii wake, wajukuu wake wawili, Mahdi, Bwana wa mashahidi Hamza, na Jafari aliye ruka kwenda peponi”, kubwa alilokusudia ni kuelezea utukufu wa Ammi yake na ndugu yake, akaowanisha shahada yao na wale walio jitolea katika kutetea ujumbe wa Mwenyezi Mungu na ambao ndio nguzo za uislamu na imani.
Lau kama Bwana wa Mashahidi Hamza na mtoto wa Ammi yake Jafari Twayaar (mrukaji) wasingekua na utukufu wowote zaidi ya shahada na kukubali ujumbe wa Mtume wasinge unganishwa na watu wema.
Abu Abdillahi Swadiq (a.s) anasema: “Itakapo fika siku ya kiyama na Mwenyezi Mungu (s.w.t) akikusanya viumbe wake, Nabii Nuhu atakua wakwanza kuitwa na kuulizwa: Je ulifikisha? Atajibu: Ndio. Ataulizwa tena: Nani atakaye kutolea ushahidi? Atasema: Muhammad bun Abdillahi (s.a.w.w).
Akasema: Nuhu (a.s) atatoka na kupita katikati ya makundi ya watu hadi afike kwa Muhammad (s.aw.w), atamkuta sehemu inayo nukia miski akiwa pamoja na Ali (a.s), na ndio maana ya kauli ya Mwenyezi Mungu isemayo: (Watakapo iona karibu (adhabu) nyuso za waliokufuru zitahuzunika..), Nuhu atamuambia Muhammad (s.a.w.w): Ewe Muhammad, Mwenyezi Mungu (s.w.t) ameniuliza, Je! Ulifikisha? Nikajibu, Ndio. Akasema: Nani atakaye kutolea ushahidi? Nikajibu: Muhammad. Mtume atasema: Ewe Jafari na ewe Hamza nendeni mkamtolee ushahidi kua alifikisha.
Abu Abdillahi (a.s) akasema: Hamza na Jafari ndio watakao watolea ushahidi manabii siku ya Kiyama.
Mpokeaji (wa riwaya) akahoji, iko wapi nafasi ya Ali (a.s)?
Akasema: Yeye ana nafasi kubwa zaidi ya hiyo,
Na huo ushuhuda lazime uwe wa kweli, kwa maana kwamba ujengeke katika kuifahamu dini ya Nuhu (a.s) na dini za manabii wengine watakao watolea ushahidi kwa mujibu wa hadithi hii, hivyo ushahidi utajengeka katika kuielewa dini (sheria), matukio na maeneo yaliko tokea matukio hayo, hayo yakikosekana ushahidi hauwezi kufaa. Hiyo ndio maana inayo julikana tunapo sema ushahidi katika hali ya kawaida, sio ushahidi wa kielimu tu, kwamba unajua kua mitume ni maasumu na kwamba walitekeleza majukumu yao, kama ingekua hivyo tu wasinge ambiwa walete mashahidi, kwa sababu aliye wafanya kua maasumu anafahamu zaidi uaminifu wao, lakini Mwenyezi Mungu mtukufu anataka kuendesha mambo kwa hekima na kufuata misingi ya utoaji wa hukumu siku ya Kiyama.
Kisha hiyo shahada sio ya ziada, kwamba wanashuhudia kumuwakilisha mtume tu, kinacho takiwa ni ushahidi kamili wa yaliyo fanyika.
Kwa maana hiyo, hakika Hamza na Jafari wamepewa elimu kubwa sana ya kutambua sheria za dini zote zitokanazo na Mwenyezi Mungu, na wanaitambua vizuri haki, wanaweza kuielezea kesho akhera, katika ulimwengu wa ushahidi, haiwezekani baada ya elimu yote hiyo wasijue sheria za uislamu.
Twalib
Watafiti wa kiislamu wamethibitisha kua Twalibu bun Abu Twalib alisilimu mwanzoni mwa uislamu, hakika mtu mwenye mazingatio akimuangalia Abu Twalib, aliwakusanya watoto wake wote pamoja na Mtume (s.a.w.w) hawakuachana naye katika mazingira yote, pamoja na waliyo shuhudia kwake (s.a.w.w), miongoni mwa miujiza na dalili za wazi, hawakuwahi kutilia shaka ujumbe wake, mshairi anasema:
Ukiulizwa nani mbora wa walimwengu… kikabila na mbora wa familia.
Utakimbilia kwa Abdulmanafi baba… na mwanaye Hashim mtukufu.
Hakika wamepata utukufu bani Hashim… wao ndo mahala neema imeenea.
Na mbora wa bani Hashim ni Ahmad… Mtume wa Mwenyezi Mungu.
Katika hadithi ya Jaabir Answaariy inaonyesha daraja kubwa kuanzia mwanzoni mwa uislamu, anasema: nilimuambia Mtume wa Mwenyezi Mungu: Hakika watu wengi wanasema Abu Twalib alikufa kafiri?
Akasema: Ewe Jaabir Mola wako anafahamu zaidi yaliyofichikana, hakika siku niliyo pelekwa mbinguni nikafika hadi katika Arshi, niliona nuru nne, nikasema: Ewe Mola wangu! Hizi ni nuru gani? Akasema: Ewe Muhammad, huyu ni Abbulmutwalib na huyu ni Abu Twalib na huyu ni baba yako Abdullahi na huyu ni ndugu yako Twalib.
Nikasema: Ewe Mola wangu! Kwa nini wamepata utukufu huu?
Akasema: Kuficha kwao imani na kuvumilia katika hilo hadi wakafa.
Imepokewa kwa Kuleiniy katika kitabu cha Raudha Kafi kutoka kwa Swadiq (a.s) “Twalibu alikua ni muislamu kabla ya vita ya Badri, hakika makuraishi walimchukua kwa nguvu, akaingia msafara wao kwa lazima, Twalibu alitenzwa nguvu:
Ewe Mola imma wakapigane na Twalib… katika upatanisho na jambo hili.
Katika upatanisho mazungumzo yameelemewa… yamemfanya kua mwenye kunyang’anywa haki na sio aliye nyang’anya.
Naye Muhammad bun Muthanah Hadharamiy amepokea kua: Hakika Mtume (s.a.w.w) alikutana na Abu Raafii mfanya kazi wa Abbasi bun Abdulmutwalib katika siku ya Badri, akamuuliza kuhusu watu wake, akamuambia kua Makuraishi wamewachukua kwa lazima.
Haya yanathibitishwa na yaliyo pokewa na ibun Jariri, kua Mtume (s.a.w.w) katika siku ya Badri alisema: “Mimi nafahamu watu katika bani Hashim na wengineo wameletwa kwa nguvu, hawakua na haja ya kupigana na sisi, yeyote atakae kutana nao asiwauwe, na atakaye kutana na Abbasi bun Abdulmutwalib asimuue, hakika amekuja kwa kulazimishwa”.
Wanahistoria wametofautiana kuhusu kifo cha Twalibu, kuna wanao sema: Alipo toka kwenda katika vita ya Badri alipotea na habari zake hazijulikani tena, wengine wanasema: Farasi wake alimzamisha katika bahari akafa kwa maji. Kuna uwezekano mkubwa Makuraishi walimuua baada ya kufahamu uislamu wake, na kutambua kua hayuko pamoja nao.
Aqiil
Aqiil bun Abu Twalib ni moja ya matawi ya mti mwema, naye ni miongoni mwa walioridhiwa na Mtume (s.a.w.w), historia inasema kua aliingia katika uislamu mwanzoni mwa uislamu, alikua kielelezo cha kumpenda mtume, alikamilisha masharti yote ya utiifu: ukomavu wa imani ulionekana katika vitendo vyake, kufanya kheri ilikua sifa yake, utiifu ulijaa katika mambo yake, alipambika na ukweli katika kauli zake. Mtume mtukufu anasema kumuambia Aqiil: “Mimi nakupenda mapenzi ya aina mbili: nakupenda wewe kama wewe, na nina kupenda kwa kukupenda Abu Twalib”. Hivyo alikua na utukufu wa aina mbili kwa Mtume, haiingii akilini kwamba mapenzi yake yalikua yanalenga sifa za duniani.
Yatosha kwa Aqiil kua na utukufu huu mkubwa, nguvu ya imani yake ilimuwezesha kupambana na maadui wa ndugu yake kiongozi wa waumini kwa kutumia ulimi wake, kwa kutoa hoja na dalili za wazi, zilizo onyesha kupotea kwao na kushindwa njama zao katika uhai wake wote.
Hakika kupendwa kwake na Abu Twalib hakutokani na amri ya Mtume, na wala sio kwa sababu ni mwanae mkubwa, wala hakua shujaa zaidi au mwanae wa pekee, hakika alikua na watoto wengine kama, kiongozi wa waumini (Ali), na baba wa masikini Jafari Twayaar (mrukaji), naye ni mkubwa kwao kwa umri, alikua “Mzee wa Abtwah” ilitokea kupendwa zaidi yeye pamoja na kuwepo kwa watoto wengine kama vile (Imamu) na ndugu yake Twayaar kutokana na kukusanya kwake utukufu mwingi wa kurithi na wa kujifunza.
Ukijua kua Abu Twalib alikua hojja katika zama zake, na alikua ni miongoni mwa mawasii, utajua kua mapenzi yake kwa mtu sio jambo la mchezo, hivyo atakaye pata nafasi hiyo ni yule ambaye anastahiki kuipata.
Vilevile Aqiil hakua nje ya mstari wa Ahlulbait katika imani ya kumpwekesha Mwenyezi Mungu (s.w.t), vipi awe tofauti wakati wote wamelelewa katika nyumba moja, na Abu Twalib ndio mlezi wao, hakumfukuza yeyote katika darasa lake, wala katika mji wake wala hakuwahi kumdharau yeyote.
Vipi ataonyesha mapenzi yake kwake kama hana uhakika na imani yake, na uhakika wa uislamu wake, pamoja na kwamba alikua msiri wake, kama alivyo kua baba yake na kaka yake Twalib? Pamoja na kwamba hatushakii kutofautiana kwa imani baina yake na ndugu zake Twayaar na kiongozi wa waumini (a.s).
Aqiil hakua na hadhi kubwa katika uislamu kama ndugu zake hao wawili, yeye ni miongoni mwa waislamu wa mwanzo.
Kama alivyo ukubali mwito wa uislamu dada yao Ummu Hani, akawa miongoni mwa watu wa mwanzo kuingia katika uislamu, kama ilivyo pokelewa katika riwaya, na katika nyumba yake ndipo alipo shukia Mtume wakati alipo rudi kutoka mbinguni (Miraji) mwaka wa tatu wa utume, akamuambia kuhusu utume kabla ya kuutangaza kwa watu, naye alimuamini moja kwa moja, alihofia makuraishi kua watamkadhibisha, yanayo semwa kuhu yeye kua alisilimu katika fat-hu Makka, mwaka wa nane hayana ukweli.
Na ni makubwa yanayo semwa na wasemaji kuhusu mama yao, Fatuma bint Asadi mke wa Shekh Abtwaha baada ya kuthibitishwa na Mtume kua alikua mwanamke mtakatifu na muumini katika uhai wake wote. Jambo la kushangaza! Kuna wanao badilisha ukweli huo, na wanadai kua miongoni mwa utukufu wa bwana wa mawasii kwamba: Fatuma bint Asadi, aliingia katika nyumba tukufu (Kaaba) akiwa na ujauzito wa Ali (a.s) akataka kumsujudia Hubal (sanamu) Ali akamzuia akiwa ndani ya tumbo lake. Hakika sifa hiyo inamdhalilisha mwana mama mtukufu aliye takasika na uchafu wa kijinga na shiriki.
Vipi inawezekana kiumbe bora baada ya Mtume ahifadhiwe katika tumbo la mwanamke kafiri na muovu?
Pia wamemtenga kabisa na mafundisho ya Mwenyezi Mungu, wakati alikua anasikia darasa za Mtume asubuhi na jioni kila siku, pamoja na hadhi kubwa aliyo pewa na Mwenyezi Mungu ya kumfanya mwanaye kua wasii na kiongozi wa waumini, na hili likawa ni maalumu kwa mwanaye tu na wala sio kwa yeyote katika maimamu, pamoja na kwamba (Ali) ametokana na nuru moja na udongo mmoja na Mtume (s.a.w.w). Imamu Swadiq (a.s) alikua anamkasirikia kiongozi anaye jiita, kionozi wa waumini (Amirulmu-uminina), anasema: “Jina hilo halifai kuitwa mtu yeyote ispokua babu yangu (Ali) kiongozi wa waumini (Amirulmu-uminina”.
Imepokewa kua Mtume (s.a.w.w) alisimama katika kaburi lake (Fatuma bint Asadi) akasema: “Mwanao Ali, sio Jarari wala Aqiil” alipo ulizwa kwa nini amesema hivyo, akajibu: “Malaika wamemuuliza kiongozi wako nani baada ya Mtume, akaona haya kusema mwanangu”
Hivi kweli inaingia akilini mwanamke mtukufu kama huyu, aliye mbeba kiumbe bora zaidi baada ya Mtume kutojua mafundisho ya dini? Je! Kuna haya katika dini?
Ndio, walitaka kushusha heshima yake lakini hawakufanikiwa, hakika riwaya sahihi zinasema kua, pindi Mtume alipo ingia katika kaburi lake alimwita kwa sauti ya juu: “Ewe Fatuma mimi ni Muhammad bwana wa binadamu na wala sijifakharishi, watakapo kujia Munkari na Nakiri wakakuuliza nani Mungu wako? Waambie Allah ndiye Mungu wangu, na Muhammad ni Mtume wangu, na Uislamu ni dini yangu, na Qur’an kitabu changu, na mwanangu ni Imamu wangu na kiongozi wangu, kisha akatoka ndani ya kaburi halafu wakamfukia kwa udongo”.
Yawezekana hili lilikua rasmi kwa ajili yake na kwa watu watakatifu kama yeye, wakati wa uhai wa mtume haikua lazima katika talakini kumtaja kiongozi wa baada ya mtume, kama ilivyo kua maalumu kwake tu kusomewa takbira arubaini wakati takbira ya swala ya maiti ni tano.
Pamoja na watu waliotaka kushusha heshima yake katika uislamu, Mtume ameudhihirishia umma nafasi yake katika dini, na kwama yupo chini ya usimamizi wa Mwenyezi Mungu pale alipo amua kumvisha sanda kwa kutumia kanzu yake, ili awe na vazi siku ambayo viumbe watafufuliwa bila mavazi, na alimlaza katika kaburi baada ya kumuelezea hali ya kaburini na kuridhika.
Kwa ufupi: Hakika nyumba ya Abu Twalib ni nyumba ya tauhidi, imani na uongofu, watu wote katika nyumba hiyo, wanaume kwa wanawake waliukubali uislamu mwanzoni mwa daawah, miongoni mwao kuna walio dhihirisha imani yao na kuna walio ficha.
Kuoa na kuzaa
Kiongozi wa waumini (a.s) alimuowa Fatuma bint Hizam Al-Amiriyya baada ya kufariki kwa Swidiqa mmbora wa wanawake kwa mujibu wa baadhi ya wana historia, na wengine wanasema ilikua baada ya kumuoa Umama bint Zainabu bint Rasulu Llah, na hiyo ilikua baada ya kufariki Zaharaa (a.s) kwa sababu Mwenyezi Mungu aliharamisha wanawake kwa Ali wakati wa uhai wa bibi Fatuma.
Akazaa naye watoto wanne wakiume, ambao ni: Abbasi, Abdullahi, Jafari na Othman, baada ya kufariki (Imamu Ali) aliishi muda mrefu na hakuolewa na mwanaume mwingine, pia Umama, Asmaa bint Umais na Lailah Nahshaliyya hawakuolewa baada yake, Imamu alikufa akiwa na hao wake wanne.
Mughira bun Naufal alimchumbia Umama, kisha akachumbiwa na Abu Hayaaj bun Abu Sufiyan bun Harith, akawakataa. Imepokewa hadithi kutoka kwa Ali (a.s) inasema: Hakika wake wa Mtume na wake wa Wasii hawaolewi na mwanaume mwingine baada yao, kwa hivyo hawakuolewa kutokana na kufanyia kazi hadithi hiyo.
Ummu Banina alikua ni miongoni mwa wanawake watukufu, akitambua vizuri haki za Ahlulbait (a.s), alikua na ikhlasi kwao, aliwapenda kwa dhati, naye alikua na heshima kubwa kwao, baada ya kurudi Madina bibi Zainabu kubra (mkubwa) alienda kumpa pole kwa kufiwa na wanae wanne, na alikua anamtembelea kila siku ya sherehe.
Imepokewa kuhusu ukubwa wa uwelewa wake kuhusu hadhi ya Ahlulbait (a.s) kwamba: alipo ingia kwa kiongozi wa waumini –Hassan na Hussein walikua wanaumwa- akazungumza nao kwa upole maneno mazuri yanayo tuliza roho, aliishi nao kwa mapenzi makubwa sawa na mama kwa mwanaye kipenzi.
Hakuna shaka juu ya hilo kwani yeye ni mke wa mtu mwenye imani kubwa, ameangaziwa na nuru yake (ya mme wake) na amenufaika na elimu yake na amepambika na tabia zake.
Kuzaliwa
Dunia iliangaziwa kwa kuzaliwa mwezi wa bani Hashim, siku ambayo iliangaza nuru yake angani, akanyonya ziwa la ushujaa, na kulelewa kwenye miguu ya ukhalifa, akalelewa katika mazingira matukufu na kuipa nyongo dunia, hakupata kushuhudiwa mahala popote ispokua nafsi yake ilikua na imani thabiti, na matarajio chanya, moyo tulivu na elimu yenye manufaa.
Aliendelea kufuata tabia za mjukuu Shahidi -Hussein- (a.s) aliye umbwa kwa ajili yake, akajengeka kuendana naye katika sifa za utukufu na ushujaa, na kusimama pomoja naye katika hatari. Akitembea (a.s) basi anaende kwenye jambo tukufu na akiongea husema maneno mema yenye uongofu, akipigana ni kwa ajili ya haki na akiacha basi hua ni batili, na akiangamia basi ni kwa ajili ya dini.
Abulfadhil (baba wa utukufu) amekusanya kila aina ya utukufu; kwa sababu alinufaika na nuru ya jua la uimamu (Hussein ni elimu, ushujaa na islahi), hivyo yeye na ndugu yake Shahidi (a.s) walikua sawa na kauli ya Mwenyezi Mungu isemayo: (Naapa kwa jua na mwanga wake* Na mwezi unapo angaza) halikupita neno lolote (la Imamu) ispokua alinufaika nalo, wala kitendo ispokua naye alikifanya, hadi mambo ya kihisia pia aliathirika nayo, alikua sawa na kopi yake.
Alimfuata Imamu katika kila kitu hadi kuzaliwa kwake, Imamu Hussein alizaliwa mwezi tatu Shabani na Abulfadhil Abbasi akazaliwa mwezi nne Shabani mwaka wa ishirini na sita hijiriyya.
Miongoni mwa mambo yasiyo kua na shaka ni kwamba, pindi Kiongozi wa waislamu (a.s) alipo letewa mwanae kipenzi ili amfanyine taratibu za sunna ambazo hufanyia mtoto anapo zaliwa, alimuangalia mwanaye ambaye kiongozi wa waumini alimchagua mama yake kutoka katika familia ya waarabu shujaa zaidi, ili amzalie mtoto shujaa atakaye mnusuru mjukuu wa Mtume siku atakapo zungukwa na maadui, Imamu alipo muangalia mtoto huyo aliona yatakayo jiri kwake, akawa anamshika katika kila kiungo kitakacho pigwa panga, na akawa anamgeuza geuza mikono yake, itakayo katwa katika vita ya kumnusuru imamu wa zama zake huku macho yake yanabubujika machozi.
Akiangalia kufua chake kwa elimu ya yakini anaona mkuki umechoma kifuani, yanaongezeka majonzi yake, na akiangalia kichwa chake anatambua kua kitapigwa na chuma na kuvunja nguvu zake, pia akimuangalia anaona atakavyo mnywesha maji ndugu yake, wala hakuna atakaye mfikia katika utukufu wa kunywesha maji watu wa nyumba ya Mtume, atawabebea maji wakati yeye mwenyewe anakiu kali, na ataacha kunywa maji baada ya kukumbuka kiu ya ndugu yake, atabobea katika kuwaliwaza, na atahakikisha anakua msaada kwao, ataonyesha mapenzi ya undugu wa dhati, atakua sambamba na watu wema, (kiongozi wa waumini) akakithirisha kusema: “Nina nini mimi na huyu Yadidi”, aliona matukio yote yatakayo wasibu wanae.
Mtoto huyu alikua kipenzi mkubwa kwa wazazi wake, walimuonesha bishara nzuri na utukufu, walitambua mabalaa yatakayo msibu ya majeraha makali, kiu na kuuawa kikatili.
Hili ni jambo la kawaida kwa watu wema wenye utukufu japo kidogo, vipi (isiwezekane) kwa kiongozi wa waumini (a.s), mtu bora zaidi kwa baba na mama.
Hivyo! Itakuaje kwake kuhusu huyu mwanadamu mkamilifu (Abulfadhil) ambae hakuna yeyote wa kufananishwa naye katika utukufu, kama tulivyo eleza kwa ufupi kuhusu kudhulumiwa kwake na mapambano yake.
Ameeleza muandishi wa kitabu cha “Bani Hashim” katika ukurasa wa 21 kua: Ummu Banina alimuona kiongozi wa waumini (a.s) anamkalisha Abulfadhil (a.s) miguuni kwake kisha anambusu katika mikono yake miwili na analia, akashtushwa na hali hiyo; kwa sababu alikua hamtambui mtoto wake kwa undani kama anavyo mtambua baba yake, na alishangaa kumuona analia bila sababu ya wazi, kiongozi wa waumini alipo muelezea yatakayo mkuta mtoto wao ikiwa ni pamoja na kukatwa mikono yote miwili kwa sababu ya kumnusuru ndugu yake Hussein (a.s), na yeye pia akalia, na wote walio kuwepo ndani wakalia, pia kiongozi wa waumini alimuelezea mkewe cheo kikubwa alicho nacho mwanae mbele ya Mwenyezi Mungu mtukufu, na kwamba baada ya kukatwa mikono yake atapewa mbawa na kuruka pamoja na malaika kwenda peponi, kama alivyo fanyiwa ammi yake Jafari bun Abu Twalib, hiyo ni bishara njema ya milele na utukufu wa kudum.
Abbasi katika mtazamo wa Maimamu (a.s).
Hatudhani kua msomaji wetu unahitajia zaidi kuhusu mada hii, baada ya kutaja wasifu wa Abulfadhil Abbasi (a.s), wa elimu na uchamungu, na nafasi kubwa aliyo nayo katika kujitolea kwenye nyia ya haki, hakika maimamu wa Ahlulbait (a.s) humpa heshima kubwa mtu asiye kua na wasifu kama hizo, vipi kwa mtu mwenye wasifu tukufu kama hizi, tena anatokana na wao!? Imamu Sajaad (a.s) anasema: daraja kubwa aliyo nayo (Abulfadhil Abbasi –a.s-) tofauti na mashahidi wengine pale alipo mfananisha na ammi yake Twayaar, akasema (a.s).
Mwenyezi Mungu amrehemu ammi yangu Abbasi bun Ali, alipata matatizo mengi, hakika alimuhami ndugu yake kwa kutumia nafsi yake hadi akakatwa mikono yake, Mwenyezi Mungu akampa mbaya mbili akaruka pamoja na Malaika kwenda peponi, kama alivyo fanya kwa Jafari bun Abu Twalib, hakika Abbasi anahadhi kubwa mbele ya Mwenyezi Mungu, mashahidi wote watatamani hadhi yake siku ya kiyama.
Neno “wote” linamjumuisha Hamza na Jafari, mashahidi wawili watakao watolea mitume ushuhuda wa kutekeleza ujumbe wao, Allamah Muhakiki Mutabahhar katika kitabu cha Kibriti Ahmar ukurasa wa 47 juzuu la 3 amekanusha habari hiyo.
Huenda kilicho andikwa katika ziara ya Shuhadaa kinadhibitisha pale inapo sema: “Amani iwe juu yenu enyi Rabaniyyuun, nyie mlitutangulia, na sisi ni wafuasi na answaru, nyie ni mabwana wa mashahidi duniani na akhera”.
Hali kadhalika kauli yake (a.s) isemayo: Hakika hakuna atakaye washinda wala kuwafikia (katika utukufu). Imethibiti kua wao ndio bora kushinda mashahidi wote, hakuna shahidi atakaye washinda wala kuwafikia katika ubora, Abulfadhil Abbasi (a.s) yupo pamoja nao katika ubora huo, na anaupekee wake kama alivyo thibitisha Imamu Sajaad (a.s) anautukufu wa aina yake ambao hakuna mwingine mwenye utukufu kama huo.
Kutokana na utukufu wake pamoja na heshima kubwa aliyo nayo, utakuta Ahlulbait (maasumina) (a.s) walikua wanamshirikisha katika mambo ambayo hawamshirikishi mtu wa kawaida, kwa mfano ndiye aliye shirikiana na ndugu yake Imamu Hussein katika kumuosha ndugu yao Imamu Hassan (a.s).
Baada ya kutambua nafasi ya Imamu, na kwamba jambo la Imamu halifanywi ispokua na Imamu mfano wake, inakua wazi kwako kua mtu atakaye toa huduma yeyote katika kumuosha Imamu, kama vile kusogeza maji na mengineyo, atakua na utukufu mkubwa duniani baada ya maimamu, hakika mwili wa Maasumu anapo kufa, hausogelewi au kuangaliwa na asiye kua maasumu, kwani kipindi hicho hua karibu zaidi na Mola wake, kipindi ambacho kipenzi wa Mola wa walimwengu hua yupo naye.
Hivyo ndio walivyo makhalifa wa mtume (s.a.w.w), wanafanana naye katika mambo yote ispokua Utume na ruhsa ya kua na wake wengi.
Miongoni mwa utukufu wa Ibun Abbasi bun Abdulmutwalib, alikua anabeba maji ya kumuogeshea Mtume (s.a.w.w) akimsaidia kiongozi wa waumini (a.s) wakati wa kumuosha, lakini alifumba macho yake kwa kuogopa asiwe kipofu kwa kuangalia mwili mtakasifu.
Na mfano wake ni habari zilizo ripotiwa kuhusu utukufu wa kaburi la Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w), watu walikua wanajitahadharisha kuliangalia, jambo hilo lilikua wazi wka watu wa Madina, ilikua kitu kinapo dondokea juu ya kaburi wanamtuma mtoto akakitoe na wanamfunga macho yake.
Siri hizi fikra za mwanadamu wa kawaida hawezi kuzielewa, lakini pia hatuna cha kufanya zaidi ya kukubali, haifai kukataa kwa sababu tu akili zetu zinashindwa kuelewa swala hilo, hususan baada ya kutambua kua Mtume na Maimamu (a.s) baada ya kufa kwao hua kuna mambo ya maajabu yanatokea, ambayo hayapatikani kwa waja wote, kama vile miili yao kutoliwa na udongo, au miili yao kupaa mbunguni, na kuonana wao kwa wao, au kufufuka wafu miongoni mwao wakiwa katika miili ya asili, mambo ambayo akili haikatai kutokea kutokana na kuwepo kwa ushahidi mwingi wa matukio hayo, na kuthibitishwa na watu wengi (1), hivyo watu wa kawaida hawawezi kuvumilia kuona maajabu ya watakasifu, hususan wakati roho zao zinapo toka ispokua nafsi za maasumina wao kwa wao, hata kama mtu atakua na uchamungu na unyenyekevu wa hali ya juu.
Lakini (Maarifa ya Abbasi) aliyo tunukiwa na Imamu katika ziara ni makubwa sana, ni nafasi waliyo fikia Mitume na Muqarabuna ambayo ni: “Mja mwema, aliye weza kufikia kiwango hicho cha utukufu, akashirikiana na mjukuu Shahidi, Mtume Mtukufuna wasii wake pamoja na jopo la malaika katika kumuosha Imamu Hassan Mujtaba mjukuu wa Mtume (s.a.w.w).
Hiyo ni nafasi ya juu kabisa ambayo haifikiwi ispokua na watakasifu miongoni mwa maasumina, Abulfadhil Abbasi alikua sawa na wasadikishaji, Mashahidi na waja wema.
Tukisoma kauli ya Imamu Hussein aliyo muambia Abulfadhil Abbasi (a.s) pindi maadui wapipo vamia hema zao jioni ya mwezi tisa Muharam, alimwambia: “Wafuate kwa ajili yangu ewe ndugu yangu, uwaulize wanataka nini? Abbasi akawafuata akiwa na wapanda farasi ishirini, miongoni mwao Habibu na Zuhairu, akaenda kuwauliza, wakasema: Hakika mtawala anasema mnatakiwa kuwa chini ya utawala wake au tupigane vita. Akarudi kumwambia Hussein, Hussein akamwambia rudi ukawaombe wasubiri hadi kesho.
Hakika unaona namna alivyo kua akiona mbali, na anaweza kutekeleza jukumu la kumlinda Imamu, naye ndio mtu wa kwanza kukutana na maadui, Mwenyezi Mungu alifungua mapambano kupitia nyie na atayafunga kupitia nyie.
Ndio, tumefahamu utukufu mkubwa alio kua nao, kisha tunakumbuka maneno ya dhahabu yasemayo (wala hakuna wanaojua utukufu islpokua watu watukufu).
Wala usidhani –ewe msomaji- kua hakuna umuhimu wa maneno hayo, baada ya kuona kauli katika ziaratu Shuhadaa na ziaratu Waarithah: “Kwa utukufu wa baba yangu nyie na mama yangu, mmetukuka na imetukuka ardhi mliyo zikwa”.
Katika ziara hii Imamu alikua hawazungumzishi, lakini (a.s) alikua anamfundisha Swafwaan atakapo kwenda kuwazuru (kuwatembelea) aseme maneno hayo, hakika riwaya hii imekuja kama ilivyo pokelewa katika kitabu cha Misbaahul-Mujtahidi cha Shekh Tusi, kua Swafwaan alimuomba ruhusa Imamu Swadiq (a.s) ya kwenda kumzuru Imamu Hussein (a.s) na akamuomba amfundishe cha kufanya.
Imamu akamuambia: “Ewe Swafwaan, funga siku tatu kabla ya kuondoka kwako.. hadi akasema, utakapo fika katika jengo useme: Allahu Akbaru Kabira, kisha endelea na ziara hadi akasema: kisha tokea mlango ambao inaelekea kiguu ya Ali bun Hassan, na uwasalimie mashahidi kwa kusema (Amani iwe juu yenu enyi mawalii wa Mwenyezi Mungu..” hadi mwisho.
Imamu Swadiq (a.s) alikua anamfundisha Swafwaan aseme maneno hayo kuwaambia mashahidi, riwaya hii haionyeshi Imamu Swadiq (a.s) husema nini anapo taka huwasalimia mashahidi.
Kuna jambo lingine linalo onyesha utukufu wa Abbasi kwa bwana wa Mashahidi, pale Imamu Shahidi alipo taka kukutana na Omari bun Saadi usiku katikati ya majeshi mawili, na kumuongoza katika njia ya haki na kumuelewesha upotevu wa ibn Maisuun, pamoja na kumkumbusha maneno ya Mtume (s.a.w.w) kuhusu utukufu wake, Imamu Hussein (a.s) aliamrisha watu wote waondoke na abakie na Abbasi pamoja na mwanaye Ali, na ibun Saad pia akafanya hivyo hivyo, alibakia na mwanaye pamoja na kijana wake.
Unafahamu tofauti ya Abulfadhil Abbasi na maswahaba wengine, pamoja na utukufu mkubwa walio nao familia ya Mtume, ambao Imamu Hussein amewashuhudia kwa yakini, ukweli, nia yadhati na kujitolea, Imamu alitaka kuonyesha utukufu wa Abulfadhil Abbasi na Ali Akbaru, hakika watu hao sifa zao hazielezeki.
Ndipo tunaona ilipo fika siku ya kumi ya Muharam, vilio vya wanawake na watoto vilipo sikika katika masikio ya Hussein (a.s) akiwa amesimama mbele ya wapiganaji, alimuambia ndugu yake Abbasi aende akawanyamanzishe, kwa ajili ya kuhofia maadui wasipate moyo baada ya kusikia vilio hivyo, na vikawachochea kwenda kuvamia haram ya watu wa nyumba ya Mtume, pia sauti zao zisisikike wa wanaume maharim.
Tukitaka kufafanua msimamo wa Abbasi (a.s) na kuchelewa kwake kupata shahada, wakati yeye ni mtukufu na mwenye msimamo imara wa kutetea dini na kuinusuru familia ya Mtume (s.a.w.w), vipi aliweza kusubiri wakati anaona ndugu zake wanavyo pigana na watoto wa ammi zake na marafiki wake, huku anasikia vilio vya watoto, wakiwa wamezungukwa na maadui kila upande, huku akiwa ni mwenye mapenzi makubwa sana kwa ndugu zake, mazingira yote yalikua yanamlazimisha aingie katika uwanja wa mapambano dhidi ya maadui wa Mwenyezi Mungu na wafuasi wa Yazidi.
Lakini ilikua ni amri ya ndugu yake mjukuu wa Mtume, ndiye aliye taka asiingie mapema katika uwanja wa vita, hakika bwana wa mashahidi (a.s) alichukulia kuchelewa kwake kuingia vitani ni sehemu muhimu ya kuubakiza Uimamu, na kifo chake kitavunja nguvu ya watu wake, anasema (a.s) “Ukiondoka wapiganaji wangu watasambaratika”. Hata wakati wa mwisho hakumruhusu ispokua baada ya kukosa njia kabisa.
Hakika hadithi ya (uwashaji moto) ya Sayyid Muhammad Ali Shaha Abdul-Adhim, inatuonyesha nafasi aliyo kua nayo (Abbasi) ni sawa na nafasi ya maasumina, pindi Sajjaad (a.s) alipo enda kuzika mashahidi wa Karbala, aliwapa nafasi bani Asadi ya kumsaidia katika kuwazika, ispokua mwili wa Imamu Hussein na wa ammi yake Abbasi (a.s), aliwazika yeye peke yake, akawaambia: “ninaye anaye nisaidia”.
Kuhusu Imamu jambo hili lipo wazi; kwani kawaida Imamu ashughulikiwi ispokua na Imamu mwenzake, lakini jambo la kujiuliza ni kwa ammi yake Abbasi kwa nini amfanyie kama alivyo mfanyia baba yake, bila saha ni kwa sababu alikua mtakatifu zaidi, hivyo mwili wake haukupaswa kushikwa ispokua na mtu mtakatifu zaidi, katika muda ambao yupo karibu zaidi na Mola wake.
Bado utukufu wake unaenziwa na watu wa nyumba ya Mtume (a.s) duniani na akhera, hata bibi Zahara (a.s) atakapo toa malalamiko yake ataanza na lalamiko la kukatwa mikono ya Abulfadhil Abbasi (a.s), kama ilivyo andikwa katika kitabu cha Asraar ukurasa wa 325 na kitabu cha Jawaahir Iqaan ukurasa wa 194, na swala hili ni miongoni mwa mambo muhimu katika sababu za kupata uombezi siku ya kiyama.
Abbasi (a.s) awanywesha maji Ahlulbait (a.s).
Kunywesha maji, ni miongoni mwa ibada kubwa sana katika sheria ya kiislamu, kwa sababu ni kuipa uhai nafsi na kuilinda isiangamie.. haya ndio aliyo bainisha Mtume (s.a.w.w) pale alipo sema: (Ibada tukufu zaidi mbele ya Mwenyezi Mungu ni kupoza moyo kutokana na joto hata ikiwa kwa maji, hakika kufanya huvyo huporomosha dhambi kama vile majani yanavyo dondoka kutoka mtini, Mwenyezi Mungu atamlipa mja kwa kila tone la maji nyumba peponi, na atamnyesha kutoka katika mto wa Rahiqin Makhtum na pindi aridhi itakapo tandikwa atakunywa katika hodhi tukufu pamoja na Mtume..).
Mtume (s.a.w.w) aliulizwa ibada gani itakayo muingiza mtu peponi, akasema: (Nunua chombo cha kunywea (maji) ukitumie kunyweshea watu utakua umefanya ibada ya kukuingiza peponi).
Na katika hadithi iliyo pokewa na Imamu Swadiq (a.s) anasema: (Atakaye nywesha maji katika eneo lenye maji ataandikiwa thawabu sawa na kumuacha huru mtumwa, na atakaye nywesha maji katika eneo lisilokua na maji ataandikiwa thawabu sawa na aliye ipa uhai nafsi na mwenye kuipa uhai nafsi moja na sawa na mwenye kuwapa uhai watu wote..).
Hakika maji yana umuhimu mkubwa sana katika uhai wa walimwengu, Imamu Swadiq (a.s) amethibitisha hilo pale alipo ulizwa ladha ya maji, akasema (a.s): (Ladha yake ni uhai).
Sio ajabu tukisema kua sifa ya kunywesha watu ya Mwezi wa bani Hashim (a.s) mnyweshaji wenye kiu Karbala kairithi kutoka kwa babu zake watukufu, kuanzia kwa Kuswai, Abdulmanafi, Hashim hadi kwa Abdulmutwalib na baba yake kiongozi wa waumini Ali bun Abu Twalib (a.s).
Historia ya kiislamu inatuambia kuhusu kunyweshelezwa mahujaji na bani Hashim… pamoja na kwamba kiongozi wa waumini (a.s) alinywesha waislamu katika vita ya Badri, pale waislamu walipo ogopa kwenda kuchota maji, akaenda Imamu Ali bun Abu Twalib (a.s) bila khofu wala uoga akawaletea maji, akampa Mtume (s.a.w.w) na waislamu wote baada ya kua na kiu kali, hivyo Imamu (a.s) akawaokoa waislamu hao kutokana na kiu.
Alicho kifanya Abulfadhil Abbasi (a.s) siku ile katika viwanja vya Twafu sio jambo geni kwake, alipigana vita kali hadi akafanikiwa kupasua ngome ya maelfu ya maadui, huku jambo kubwa likiwa ni kumuokoa mjukuu wa Mteme na watu watukufu wa familia ya Alawiyya kwa kuwapelekea maji, pia nafsi yake ilikataa kuonja hata tone la maji kabwa ya kunywa ndugu yake Imamu Hussein na watu wa nyumbani kwake (a.s)…
Kama riwaya zinavyo sema, siku ya mwezi saba Muharam, Abulfadhil Abbasi (a.s) aliumia sana alipo ona watoto wa ndugu yake na watu wa nyumbani kwake wanalia kutokana na kiu kali, akaamua kwenda kuwaletea maji kwa nguvu, aliondoka na wapanda farasi thelathini na watu ishirini watembea kwa miguu wakiwa na viriba ishirini, wote kwa pamoja wakaenda kuuvamia mto wa Furat, upande wa Imamu Hussein akatangulia Naafii bun Hilali Almuraadi, na upande wa maadui walikua wakiongozwa na Omari bun Hajjaaji Zubaidi, ambaye ni miongoni mwa watu waovu katika vita ya Karbala ndiye aliye kua anasimamia ulinzi wa mto wa Furat, akauliza: (Umekuja kufanya nini?)
Akajibiwa: Nimekuja kunywa maji uliyo tuzuilia..
Akamwambia: Kunywa.
Akamjibu: Ninywe wakati Hussein ana kiu, pamoja na maswahaba zake?
Akasema: Hauna ruhusa ya kuwapa maji ya kunywa watu hao, sisi tumewekwa hapa kuwazuia wasipate maji…
Majemedari wa Imamu Hussein hawakutishwa na maneno hayo, walivamia mto wa Furat wakajaza viriba vyao maji, Omari bun Hajjaaj na jeshi lake likataka kuwashambulia, ndipo kamanda wa Karbala Abulfadhil Abbasi (a.s) na Naafii bun Hilali wakaingia vitani, wakapigana vita kali sana lakini pande zote mbili hakuna aliye kufa, maswahaba wa Imamu wakarudi wakiwa wamejaza vyombo vyao maji chini ya uongozi wa Abulfadhil Abbasi (a.s).
Abulfadhil Abbasi (a.s) akafanikiwa kuwapa maji ya kunywa watu wa nyumba ya Mtume (a.s) na akawaokoa kutokana na kiu kali waliyo kua nayo, kuanzia siku hiyo akapewa jina la Mnyweshaji (Saqaa) nalo ni miongoni mwa majina yake mashuhuri zaidi, na linajulikana sana kwa watu pia ni jina tukufu zaidi kwake.
Msimamo wake alipokua Twafu
Maneno hayatoshi kueleza utukufu kutokana na wingi wake, yawezekana uwazi ukafuatiwa na usiri, hakika miongoni mwa sifa kubwa ya bani Hashim ni ushujaa, hususan kizazi cha Abu Twalib, kuhusu swala hili kuna hadithi ya mtume isemayo: “Lau kila mtu angezaliwa na Abu Twalib wote wangekua mashujaa”.
Hivi unadhani mtoto wa Abu Twalib kiongozi wa waumini (a.s) muuaji wa Amru bun Abdul-Udi, jemedari aogopwae, aliyefungua mlango wa Khaibari, alimrithisha mwanae ushujaa wote? alimfundisha kuongoza misafara, alikua pamoja naye kipindi cha vita kali, alishuhudia ushujaa mkubwa wa ammi zake. Waarabu walikua wanasema (Fulani mkuu wa farasi) atakapokua shujaa vitani, lengo kuu la kiongozi wa waumini (a.s) kumuoa Ummul-Banina lilikua kwa ajili ya kumzalia jemedari huyu, alifanikiwa lengo lake wala mshale wake haukukosea shabaha.
Abulfadhil alikua alama ya ushujaa, nguvu zake zilionekana usoni kwake, hakuogopa kifo wala kukimbia vita, aliogopwa na maadui wakubwa, aliwauwa majemedari wakubwa wa makariri vitani.
Anafanana na baba yake Karraar katika maamuzi yake … bali katika maana ya utukufu na sifa zake.
Haukua mkono wa Mwenyezi Mungu ispokua ni baba yake … na uwezo wa Mwenyezi Mungu ulikua kwake.
Alikua mkono wa Mwenyezi Mungu na yeye pingili ya mkono wake … yakutosha kuangalia uthabiti wake.
Ni shujaa pale anapo wasili … kama sio kupita mipaka ningesema: umetukuka uwezo wake.
Je inawezekana kwa mshairi kwenda kinyume na maneno yake, au inawezekana kwa muandishi kuandika ushujaa wa Haidariyya, anajipambanua mwenyewe, yuko wazi mbele ya mtafiti, yatosho kumtambua kupitia yaliyo tokea katika vita ya Twafu.
Unapo elezea ushujaa wa Karbala hauwezi kuacha kumzungumza, alikua kilele cha ushujaa na ujasiri tangu zamani, hakutishika na wingi wa adui, alikua muhudumu wa msafara wa Imamu Hussein (a.s) kwa kuwapa chakula na maji ya kunywa, aidha aliweza kusimama katikati ya majeshi mawili.
Wanahistoria wanataja ushujaa uliokuwepo katika zama za ujinga kama katika kisa cha Rabiah bun Mukadam, kisemacho: Rabiah bun Muqadam bun Aamir bun Harthaan katika bani Maalik alikua mmoja wa mashujaa wakubwa, alitoka akiwa na mama yake Ummu Sanaan katika bani Ashjaa bun Aamir bun Laisa bun Bakru bun Kinana, na dada yake Ummu Uzzah, na kaka yake Abu Quráh, akamuona Duridi bun Swamah, akamuambia mtu aliye kua nae; mtu huyu amekusudia kukushambulia, jihami. Alikua hamjui, Rabiah alipo jua kua yule mtu anamfuata, alikaza mkanda wa ngamia na akapigana nae hadi akamuua, Duridi akatuma mtu mwingine, Rabiah akamuua. Akatuma mtu wa tatu Rabiah akamuua halafu mkuki wake ukavunjika, alipo enda kuangalia, akakuta watu watatu wameuwawa na mkuki wa Rabiah umekatika, alipo mkaribia Duridi akaona maiti tatu na mkiki ukiwa umevunjika akasema: ewe kijana mfano wako hauwawi, jamaa wa watu hawa watachukua kisasi dhidi yako, wala hauna mkuki, chukua mkuki wangu utumie kujihami, akampa mkuki wake na akarudi kwa watu wake, akawaambia kua yule mtu ameua watu watatu na amempa mkuki wake ajihami, msiwe na matumaini naye.
Haya ndio yaliyo andikwa na historia kuhusu Rabiah bun Mukadam ambaye alipigana hadi mkuki wake ukavunjika, lakini yuko wapi ukilinganisha na (mlinzi wa msafara) siku aliyo pigana na maelfu ya watu, akawashinda na akayafikia maji akachota na kujaza kiriba mbele ya macho ya maadui?!
Yuko wapi Rabiah ukilinganisha na ujasiri mkubwa aliokua nao Abulfadhil Abbasi, hakuelekeza ispokua katika utukufu, alipambana wakati ambao majemedari wapo katika sakaratil-mauti (mahutihuti).
Mjukuu wa Mtume Mtukufu anaukurasa mwingine wa ujemedari, alipambana baina wa kundi la maadui huku uso wako ukiwakawaka kwa utukufu, watu wa nyumba ya Mtume wanahistoria nderu ya kulinda mafundisho ya Dini takatifu.
Kuna mifano mingi ya ushujaa wake katika vita kali, inatosha kukuonyesha ujasiri na ushujaa wake pamoja na utulivu aliokua nao wakati wa matatizo makubwa.
Kwanza: Mwezi saba Muharam bwana wa mashahidi pamoja na wafuasi wake waliokua pamoja nae, walizungukwa na maadui, wakazuwiwa kuchota maji, na wakaishiwa maji waliyo kua nayo, kila mmoja akaanza kuhisi ukali wa kiu, wakaanza kulia na kuomba maji, yote hayo yanafanyika mbele ya macho ya Abu Ali, na majemedari wa familia yake pamoja na wafuasi wake watukufu, huku wakiwa wametenganishwa baina yao na maji (mto) kwa mikuki na mishale mikali chini ya jeshi kubwa linalo ongozwa na Amru bun Hajjaaj, lakini myweshaji wenye kiu (Saaqi Atwaasha) hakuweza kuvumilia hali ile:
Familia ya Fatuma kulia kiu mbele yake… huku mbele ya macho yake maji ya mto Furaat yanapita.
Hatakama kuufikia mto kunamgharimu damu… au ni mbali sana hawezi kurizika hadi ayafikie.
Hata kama kungekua na ukuta wa Dhuqarnaini… angeuparamia kwa nguvu zote hadi auvuke.
Katika mkono wa kushoto akashika chombo cha kuchotea maji… na mkono wa kulia akashika siraha ya kujilinda.
Alikwenda kama wingu kwa ajili ya kunusuru familia ya Fatuma… akapambana kwa ujasiri na maadui akawashinda.
Imamu Hussein akampa jukumu la kwenda kuchota maji ndugu yake Abbasi, huku nafsi yake tukufu ikiona uzito kumruhusu, yalikua ni maamuzi magumu, akamuamuru aende kuleta maji, japokua hilo ni jambo gumu linalo weza kumwaga damu, akampa wapanda farasi thelathini na watembea kwa miguu ishirini wakiwa na viriba (vyombo vya kuchotea maji) ishirini, akatangulia mbele yao Naafii bun Hilali Aljamaliy, wakaenda bila uoga, kila mmoja akizingatia sheria; kwa sababu wametumwa na mbora wa watu wa nyumba ya Mtume Muhammad, Amru bun Hajjaaji akauliza kwa sauti ya juu: Nani wewe? Una shida gani?
Naafii akajibu: Nimekuja kunywa maji mliyo tuharamishia.
Akamuambia: Karibu kunywa.
Naafii akasema: Hapana, Wallahi siwezi kunywa tone moja la maji huku Hussein na watu wa nyumba yake pamoja na wafuasi wake wakiwa na kiu.
Amru akasema: Hakuna njia ya kuwapa maji watu hao, tumewekwa hapa kuzuwia wasipate maji, Naafii akawaambia watu wake: Jazeni viriba vyenu maji, jeshi la bun Hajjaaj likawavamia, ikawa baadhi yao wanachota maji na wengine wanapigana wakiwa pamoja na jemedari wao, aliye lelewa na miguu ya ushujaa wa Haidariyya (Abulfadhil Abbasi), wakarudi na maji wote wakiwa salama, watu wakaweza kunywa na kupoza kiu kali waliyo kua nayo.
Usisahau kua kiasi hicho cha maji kilikua ni kidogo, hakitoshi kwa kundi la watu zaidi ya mia moja na hamsini, wanaume, wanawake na watoto, kwa mujibu wa baadhi ya riwaya zinasema walikua karibu watu mia mbili, ni wazi kua kila mmoja alikunywa mara moja tu, tena walikunywa kidogo sawa na kuonja, hivyo kiu ilirudi haraka, hawakuwa na wakumshtakia zaidi ya Mwenyezi Mungu.
Pili: Wafuasi wa Imamu Hussein (a.s) baada ya shambulio la kwanza ambalo watu hamsini waliuawa kishahidi, walianza kutoka kwenda kupigana wawili au watatu au wane, kila mmoja alikua anapigana kumlinda mwenzake asiuawe, akatoka Jaabiri na mwenzake wakapigana hadi wakauawa, akatoka Ghifaar na mwenzake wakapigana hadi wakauawa, Huru Riyahi pamoja na Zuhair bun Qain wakaingia katika uwanja wa vita huku kila mmoja akimhami mwenzake wakapigana sana lakini hatimae Huru akauawa.
Katika kitabu cha Tarikh Twabari jz6 uk255 kuna habari inayo sema: “Hakika Amru bun Khalid Swaidawi, Saadi, Jaabir bun Haarith Salmani na Mujmaa bun Abdillahi Al-Aaidhiy wote kwa pamoja waliwavamia watu wa Kufa, walipo anza kupigana walizungukwa na maadui kila upande, Hussein akamtuma ndugu yake Abbasi akaenda kuwaokoa, wakiwa wote wamejeruhiwa, wakati wanarudi wakavamiwa tena na maadui, wakapigana kwa ujasiri mkubwa pamoja na majeraha waliyo nayo, hatimae wakauawa wote kwa pamoja, wakafaulu kupata utukufu wa milele”.
Msimamo wake kabla ya Twafu
Baadhi ya waandishi wameandika kuhusu msimamo wake kabla ya Twafu, katika kitabu cha Muntakhab kinasema: alikua kama jabali kubwa, na moyo wake kama nguzo imara, alikua jemedari shupavu mbele ya makarifi.
Muandishi wa kitabu cha Kibriti Ahmaru juzuu ya 3 ukurasa wa 24 amenukuu kutoka kwenye vitabu vikubwa kua: Hakika yeye –Abbasi- (a.s) alikua nguzo muhimu kwa ndugu yake Hussein katika siku aliyo vamia mto wa Furaat na kusambaratisha jeshi la umawiyya lililokua linalinda maji.
Amesema kua: katika siku za vita ya Swifin, alitoka kijana katika jeshi la kiongozi wa waumini (a.s) akiwa amevaa nikabu usoni kwake, anaonekana mwenye haiba na ushujaa mkubwa aliyekua anakadiriwa kuwa na umri wa miaka kumi na saba, akaomba kuingia katika uwanja wa mapigano, akazungukwa na watu, Muawiya akamtumia Abu Shaáshaai, akasema: watu wa sham hunilinganisha mimi na watu elfu moja waliopanda farasi, namtumia mmoja wa watoto wangu (alikua na watoto saba), kila mtoto aliye mtuma kwake aliuwawa, ndipo akaenda yeye mwenyewe akiwa amekasirika sana, alipo pigana na yeye pia akauwawa, maadui wakakimbia hakuna aliyethubutu kupigana naye, wafuasi wa kiongozi wa waumini (a.s) wakashangazwa na ujasiri huo, lakini hawakumtambua kwa kua alikua amevaa nikabu, alipo rudi baba yake kiongozi wa waumini (a.s) akamwita, ndipo akatoa nikabu yake, akaonekana wazi kua ni “mwezi wa bani Hashim” ni mwanae Abbasi (a.s).
Muandishi wa kitabu cha Kibriti baada ya kusimulia kisa hiki akasema: Habari hii ni sahihi kwa sababu wakati wa vita hiyo alikua na umri wa miaka kumi na saba, na Khawarzami amesema kua, alikua mkamilifu.
Ameandika hivi katika kitabu cha Manaaqib ukurasa wa 147: “Katika jeshi la Muawiya alitoka mtu anaye itwa: Karibu, alikua shujaa sana, alikua anaweza kuchukua dirham na akaisugua kwa mikono yake hadi maandishi yakafutika, akaita mpiganaji katika jeshi la Ali ajitokeze kwenda kupambana naye, akatoka Murtafiu bun Wadhwaahu Azzubaidi akauliwa, kisha akaenda Sharhabiil bun Bikru akauliwa, akaenda Harthi bun Halaaji Shaibani akauliwa pia, jambo hilo likamhuzunisha kiongozi wa waumini (a.s) ndio akamwita mwanae Abbasi (a.s), alikua kijana shupavu, akamtaka ashuke kwenye farasi wake na avue nguo zake, kiongozi wa waumini (a.s) akavaa nguo za mwanae na akamvisha nguo zake na akampandisha kwenye ngamia yake, ili Karibu asidharau kupigana naye (ajuwe kua anapigana na kiongozi wa waumini na sio mwanaye) alipo kwenda kupigana naye akamkumbusha siku ya kiyama na akamtahadharisha na hasira za Mwenyezi Mungu juu yake.
Karibu akasema: Upanga wangu umesha uwa watu wengi kama wewe, kisha wakaanza kupigana, akampiga kichwani kwake na kukipasua vipande viwili, akarudi na akamwambia Muhammad bun Hanafiyya: Simama mahala alipo fia Kalibu hadi jamaa zake watakapo kuja, Muhammad akasimama sehemu ile, akaja mmoja na watoto wa Ammi yake akauliza nani aliye muua Karibu? Muhammad akasema: mimi, akapigana nae hadi Muhammad akamuua, akaja mwingine akapigna naye hadi akamuua akaendelea kupigana nao hadi mtu wa saba miongoni mwao.
Katika ukurasa wa 105 kuna hadithi iliyo pokelewa na Abbasi bun Haarith bun Abdulmutwalib: Alipigana nao Othumani bun Waaili Alhamiri Abbasi kamuua, akapigana na ndugu yake Hamza, alikua shujaa mkubwa, kiongozi wa waumini (a.s) akamkataza asipigane nao, akamuambia: vua nguo zako na unipe siraha yako halafu usimame hapohapo, mimi naenda kupigana nao, akaenda pekeyake kiongozi wa waumini (a.s) akampiga kichwani kwake na kumpasua vipande viwili, wayemen wakashangazwa na ushujaa huo wakamkimbilia Abbasi bun Haarith.
Haya ndio yaliyo tokea katika sifa zake, kuna vita mbili alizo pigana kiongozi wa waumini (a.s) pamoja na mwanae Abbasi.
Shekhe wetu mtukufu Nuri kukataa kwake kuhusu kuwepo kwa Abbasi katika vita ya Swifiin, amechanganikiwa na baadhi ya mapokezi ya Abbasi bun Haarith mahala pasipokua kwake, hoja za habari sio kamili, kwa sababu wapokezi wa nyumba hii ni watukufu, ikipokewa kutoka kwa mmoja wao jambo linalo husu ushujaa hua sio uzushi, hata kama taarifa ikiwa haijakidhi vigezo.
Qassim bun Hassan mjukuu wa Mtume (s.a.w.w) atimiza ndoto kwenye vita ya Twafu, alionyesha ujasiri mkubwa, hakika ni ujasiri wa kurithi, alipigana kishujaa hadi akafanikiwa kuua askari thelathini wapanda farasi, pamoja na umri mdogo aliokua nao, hakika watu wa nyumba ya Mtume wote wako sawa, mdogo ni sawa na mkubwa, hawakuweza kumpiga hadi pale alipo shughulika na kutengeneza kiatu chake, kawaida vita hupimwa kwa kupigana kwa usawa, ndipo mshairi akasema:
Aliinama kufunga kiatu chake… huku vita ikiendelea
Hawakuweza kumpiga… hadi aliposhughulishwa na kiatu chake
Alirithi ushujaa mkubwa… kutoka kwa wazazi wake
Usishangae uwezo wake… tawi huchukua asili ya shina lake
Mawingu hupeperuka…. na ushujaa huongezeka kwa wenye nao
Huonyesha kuchanua kwake… kupitia maajabu ya vitendo vyake.
Huyu hapa Abdullahi bun Muslim bun Aqiil bun Abuu Twalib katika vita ya Twafu anapigana na maelfu ya wanajeshi pamoja na udogo wa umri wake, kwa mujibu wa riwaya ya Muhammad alifanikiwa kuuwa maadui tisini na tatu kwa mashambulizi matatu.
Na Muhammad bun Hanafiyya anamatukio makubwa katika vita ya Ngamia na Naharawani, alikua mshika bendera, akapata mtihani mkubwa ulio ripotiwa na historia na kupongezwa na uislamu, wakati huo alikua na umri mdogo, kama ilivyo ripotiwa na Tadhkiratul-Khawaas na Ibun Kathiir katika Bidaayah juzuu 9 ukurasa wa 38, wameandika kua alifariki mwaka 81h akiwa na miaka hamsini na sita, kua alizaliwa mwaka wa 16h, wakati wa vita hizo -zilizo piganwa mwaka wa 36h- alikua na miaka 20.
Hakuna ajabu kwa Abulfdhil Abbasi kutokana na ushujaa wake hususan baada ya kuangalia ushujaa wa watoto wa Abu Twalib.
Ndugu yake Imamu Almujtaba alikufa yeye akiwa na miaka ishirini na nne, muandishi wa kitabu cha “Qamaru bani Haashim” katika ukurasa wa 84 ameandika kua; alipo ona jeneza la bwana wa vijana wa peponi likishambuliwa mikuki, hakuweza kuvumilia alitoa panga lake akataka kwenda kupigana, kama sio kuzuwiwa na bwana wa vijana wa peponi kutokana na usia wa ndugu yake usemao “Nitakapo kufa msimwage damu kwa ajili yangu” vita ingetokea, Abulfdhil Abbsi akavumilia pamoja na machungu makubwa aliyo kua nayo, akasubiri ahadi ya Mwenyezi Mungu, ilipo fika alipambana kishujaa na kupata utukufu mara mbili.
Kifo chake
Bado mwezi wa bani hashim unapambana kunusuru haki kwa nguvu zote na kulinda hukumu za Dini, tangu aliponyonya maziwa ya ushujaa, na kulelewa kwenye miguu ya uimamu, akakua katika malezi ambayo ni ya kupigiwa mfano katika ushujaa na kujitolea kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, kwa kupambana na majemedari wakubwa wa makafiri, imma kupata ushindi au shahada, ilikua vigumu kwake kukubali dhulma, aliona kifo ni bora kuliko kuishi na madhalimu, hakuona thamani ya maisha kama Imamu wa haki atauwawa na watu wa nyumba ya Mtume wanapewa kila aina ya manyanyaso.
Alikua (a.s) ni mtu muhimu sana kwa mjukuu wa Mtume (a.s), na mlinzi wake mkubwa, watu wa nyumba ya Mtume walipata utulivu kwa kuwepo kwake, kupitia upanga wake mkali na bendera iliyo mkononi mwake pamoja na ushujaa wake, Imamu hakumruhusu kwenda kupigana ispokua wakati wa mwisho wa mapambano hayo matukufu, Hussein hakutaka kumruhusu wala familia haikua tayali kubaki bila yeye, mazingira yalimlazimisha afuate nyayo za baba yake za kupambana na waovu.
Hivi ndio alivyo kua Abulfadhil Abbasi (a.s) baina ya ushujaa mkubwa mbele ya maadui na utaratibu na upole mbele ya familia ya Mtume (s.a.w.w), alichelewa kuingia katika uwanja wa vita kutokana na kumtii Imamu wake (a.s) hadi ulipo fika wakati wake, pindi vilio vya kiu vilipokua vingi katika haram tukufu, nafsi yake haikuweza kuvumilia.
Hapo mbeba bendera alimfuata Imamu na kumuomba ruhusa, Abu Abdillahi hakuona chaguo lingine zaidi ya kumruhusu, kwani hakuweza kuvumilia hali ile bila kufanya kitu, alimuambia Hussein kua kila anapo angalia bendera anawaona maadui wapo karibu wanaelekea kuwafikia, na watu wa nyumba ya Mtume (a.s) wanapata utulivu kwa uwepo wake, Imamu akamuambia: “Wewe ni mbeba bendera wangu”, lakini nenda kawatafutie hawa watoto japo maji kidogo.
Abbasi (a.s) akaenda kwa maadui akawahutubia na kuwatahadharisha na hasira za Mwenyezi Mungu, hutuba na nasaha zake havikusaidia kitu, akarudi kwa ndugu wake, akasikia sauti za watoto wanalia kiu, akaondoka kwa uchungu, akachukua chombo (kiriba) na akapanda farasi wake na kuelekea kwenye mto Furaat, wingi wa maadui haukumzuwia kuyafikia maji, alipigana kishujaa kama alivyo kua baba yake na kuwasambaratisha wote, alipo yashika maji alikumbuka kiu ya Imamu Hussein (a.s), akaona hatakiwi kunywa maji, kwa sababu Imamu na familia yake wanakiu zaidi, alimwaga maji yaliyokua mkononi mwake na akajaza chambo (kiriba) maji huku anasema:
Ewe nafsi nani utamtumikia baada ya Hussein … baada yake haufai kuendelea kuishi.
Hussein yupo katika kiu kali … unataka kunywa maji baridi.
Tallahi hili sio tendo la Dini yangu.
Wakati anatoka mtoni akazungukwa na maadui wengi sana, lakini hakujali, akaanza kupigana nao huku anasema:
Siogopi kifo kinapo wadia … hata nikiuwawa katika vita kali.
Mimi ni Abbasi nataka kugawa maji ya kunywa … wala sikimbii kifo siku ya kukutana nacho.
Akashambuliwa na Zaidu bun Riqaad Jahniy pamoja na Hakim bun Tufaili Sambasi, akakatwa mkono wa kulia, akashika jambia kwa mkono wa kushoto akaendelea kupigana huku anasema:
Wallahi mkikata mkono wangu wa kulia … mimi taendelea kuhami Dini yangu milele.
Na kumuhami Imamu wa kweli … mtoto wa mtume mtukufu.
Hakim bun Tufail aliyekua amejificha nyuma ya mtende akampiga kwenye mkono wa kushoto kwa kuvizia, akaukata, akaikumbatia bendera kifuani kwake.
Hapo wakaanza kumshambulia kwa wingi kutoka kila upande, wakammiminia mishale kama mvua ikatoboa (chombo) kiriba cha maji, huku mkuki mwingine ukimchoma kifuani na mwingine jichoni, mtu mwingine akampiga kwa chuma kichwani.
Akaanguka pembeni ya mto Alqami, akaita kwa sauti ya juu:
Amani iwe juu yako ewe Abu Abdillahi, Hussein (a.s) akaondoka haraka kuelekea aliko ndugu yake kipenzi.
Ndio, Husseiu aliwasiri akamkuta ndugu yake anapumua pumzi za mwisho akiwa amelala kwenye dimbwi la damu, amechoshwa na mishale hawezi kujihami kwa chochote, hawezi kuinua mkono wala kuongea anagalagala kwenye damu.
Ni kweli Hussein atavumilia hali hiyo? Hapana hakua katika hali ya kawaida baada ya kuuwawa Abulfadhil Abbasi, anaeleza jambo hili kwa kusema kua:
“Mgongo wangu umevunjika, nguvu zimeniisha na maadui wangu wamefurahi”.
Kulionekana wazi kuisha kwa nguvu zake … milima ikaitikia kilio chake.
Mhudumu wa familia yake na mnyweshaji wa watu wake … na mbebaji wa bendera yake kauwawa.
Kwa nini isiwe hivyo wakati alikua pambo lake, alimliwaza na kumuhami.
Akarudi kwenye hema akiwa mnyonge aliyejaa huzuni huku analia, anafuta machozi kwa kipande cha nguo yake ili wanawake wasione anavyo lia, maiti za wanaume zikiwa zimejaa ndani ya hema, akaita kwa sauti ya juu: wako wapi wa kutusaidia waje kutusaidia? Wako wapi wenye kutafuta haki waje kutunusuru? Wako wapi wanao ogopa moto watuhurumie?
Maneno hayo yalikua ni kutimiza hoja, ili asipatikane wa kujitetea siku ya kiyama.
Sakina alipomuona baba yake anakuja, alimuuliza: Yuko wapi Ammi yangu Abbasi, amechelewa kuleta maji? Akamuambia: Ammi yako kauwawa, Zainabu akasikia akasema: Ewe kaka yangu! Ewe Abbasi wangu! Msiba ulioje baada yako! Wanawake wakalia sana na Imamu Hussein akalia pamoja nao: huku wakisema msiba ulioje baada yako ewe Abulfadhil.