Kwa kushirikiana na idara ya afya ya Karbala: kitengo cha mipango na maendeleo ya binadamu chafanya nadwa ya wakina mama..

Sehemu ya nadwa
Kitengo cha mipango na maendeleo ya binadamu katika Atabatu Abbasiyya tukufu kwa kushirikiana na idara ya afya ya mji wa Karbala tukufu, wamefanya nadwa ya aina yake kuhusu vifo vya wakina mama, na kujadili sababu za vifo hivyo na namna ya kujilinda, katika nadwa hii wameshiriki wakina mama wenye fani tofauti, na imefanyika katika ukumbi wa Qassim bun Hassan (a.s) ndani ya Atabatu Abbasiyya tukufu.

Dokta Nadhaal Hassan kutoka katika kitengo cha uboreshaji wa afya katika khutuba yake alisema kua: “Nadwa hii ni miongoni mwa nadwa nyingi ambazo zimefanywa katika mji wa Karbala tukufu, zinazo lenga kujenga uelewa katika mambo ya afya kwa wakina mama na kupunguza idadi ya vifo vya wakina mama kadri itavyo wezekana, kutokana na makadirio ya shirika la afya la kimataifa, na kutokana na program ya afya ya kupambana na swala hili”.

Tunapenda kukumbusha kua; kitengo cha mipango na maendeleo ya binadamu cha Atabatu Abbasiyya tukufu ni miongoni mwa vitengo hai, hufanya nadwa na kozi za kimaendeleo katika mambo mbali mbali.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: