Tamko la mwisho katika mkutano wa (faharasi ni zana katika jamii ya waarabu kwa kutumia program ya RDA)..

Maoni katika picha
Kutokana na wito mtukufu kutoka kwa kituo cha faharasi na mpangilio wa maalimati chini ya ofisi ya Daru makhtutwati ndani ya uwenyeji wa Abulfadhil Abbasi (a.s) limefanyika mkutano wa pili wa faharasi na usanifu chini ya kauli mbiu isemayo (Faharasi ni zana katika jamii ya waarabu kwa kutumia program ya RDA) siku ya tarehe (16 na 17 mwezi wa pili) na kushiriki jopo la wataalamu na taasisi za kielimu hususana katika mambo ya maktaba pamoja na maeneo matukufu (mazaru) na vituo vya elimu vya ndani na vya kigeni, pembezoni mwa kongamano hili zimefanyika harakati nyingi kama vile:

  1. Maonyesho ya nakala kale kwa kushirikiana na Darul kutubi na vifaa vya kiiraq.
  2. Washiriki kutembelea maktaba ya Atabatu Abbasiyya na kukagua vitu vilivyomo miongoni mwa vitabu na mpangilio wa vifaa.
  3. Kutembelea kituo cha kutengeneza na kukarabati nakala kale, katika muda wa siku mbili washiriki walifundishwa baadhi ya mambo katika vikao vitatu vilivyo shehena vitu vingi, vilivyo pelekea washiriki kutoa mapendekezo yafuatayo:
  4. Mkutano huu ufanywe kua kongamano la kila mwaka na lihusike na mambo ya kitaalamu katika ulimwengu wa elektronik.
  5. Kuchapisha kitabu kitakacho elezea mazingira ya makongamano ya nyuma.
  6. Kunufaika na kipeperushi cha maahadi kupitia kituo cha faharasi na mpangilio wa maalumati chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu kwa kuanzisha utaratibu wa RDA, na kuanzisha mtiririko wa masomo kwa kutumia program ya RDA.
  7. Kuwaalika watu walio bobea katika mambo ya maktaba na kufanya nadwa za kujadili swala la faharasi na changamoto zilizopo katika maktaba za Iraq na za nchi za kiarabu kwa ujumla katika kutekeleza utaratibu mpya wa faharasi.
  8. Kutumia vyuo vikuu katika kusaidia wataalamu wanaosomea fani ya RDA.
  9. Kuthamini uwezo wa mafundi vijana wanao somea mambo ya maktaba na kuongeza juhudi za kuwasaidia ili waweze kugundua program zitakazo wasaidia waweze kutumia kanuni za faharasi ya namba.
  10. Kuongeza masomo na tafiti kuhusu mambo yanayo tatua changamoto za maktaba za ndani ya eneo letu na katika nchi za kiarabu kwa kufuata kanuni zinazo kubalika kimataifa na maelekezo yanayo wekwa na taasisi za kimataifa kuhusu faharasi mpya.
  11. Kuongeza uwezo wa watumishi wa maktaba na vituo vya kutoa maelezo kwa kuwapa kozi za mara kwa mara kuhusu misingi na kanuni za faharasi mpya.
  12. Kuhimiza maktaba na vituo vya kutoa maelezo vya kiiraq kua wazi na kupanua uwanja wa kushirikiana baina yao katika kubadilishana uzoefu na maarifa pamoja na kufungua uhusiano na taasisi za elimu za kimataifa.
  13. Kukiomba kituo cha faharasi na mpangilio wa maalumati cha Atabatu Abbasiyya tukufu kitoe chapisho (kitabu) kitakacho elezea uzoefu wao katika kutumia (RDA) pamoja na kuelezea changamoto walizo pata na namna walivyo zitatua pamoja na kuelezea ubora wa program hii.
  14. Kutoa mialiko kwa watu walio somea mambo ya faharasi na wafanya kazi wa maktaba katika kufanyia kazi maktaba kongwe kwa njia salama na kuwasiliana kwa kutumia mtandao wa www.rdatoolkit.org kwa ajili ya kupata utatuzi wa changamoto zinazo jitokeza.
  15. Kualika taasisi za elimu za kiiraq kuja kufasiri kifungu cha (2030) kilicho pitishwa na umoja wa mataifa chini ya kauli mbiu isemayo (Nafasi ya taasisi za elimu katika maendeleo endelevu) na kuioanisha na program ya maendeleo ya maktaba na vituo vya elimu vya Iraq kwa namna inayo kubaliana na maendeleo ya kimazingira ya sasa.
  16. Kualika wizara ya elimu ya juu na kujadili kielimu vigawanyo vya elimu na maktaba za vyuo vikuu vya Iraq na kuangalia namna ya kunufaika na mradi rasmi wa kuendeleza selebasi za masomo katika vigawanyo vya elimu na maktaba za vyuo vikuu vya dunia nzima, hasa katika nchi za kiarabu.
  17. Kutoa wito kwa watunga sheria kuandaa kanuni na taratibu za maktaba na kuzipatia uwezo wa kiofisi unao hitajika pamoja na kuzisaidia kipesa kadri itakavyo hitajika kwa ajili ya kuziendeleza na kuzibadilisha kua maktaba zinazo tumia vifaa vya elekronik.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: