Uwekaji lami katika njia za nyumba za makazi za Abbasi (a.s)..

Maoni katika picha
Mafundi na wahandisi wanao tekeleza mradi wa ujenzi wa nyumba za makazi za Abbasi (a.s) chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu ambazo zimejengwa kwa ajili ya makazi ya watumishi wake, wameendelea na uwekaji wa lami katika njia za nyumba hizo, nayo ni miongoni mwa hatua za mwisho katika mradi huu kwa mujibu wa maelezo ya rais wa kitengo cha miradi ya kihandisi katika Atabatu Abbasiyya tukufu, Muhandisi Dhiyaau Maajid Swaaigh ambaye alisema kua: “Mradi wa ujenzi umefikia ukingoni, sasa hivi tupo katika hatua za mwisho na hii ni miongini mwa hatua za mwisho”.

Akasema kua: “Tunafanya uwekaji wa lami katika njia hizi kwa kutumia kifaa cha kisasa zaidi katika uchanganyaji wa lami, kifaa hicho kinaendana kabisa na hadhi ya mradi huu, pia uwekaji wa lami hii unaendana na ramani ya mradi inayo onyesha maeneo makuu manne katika barabara 50 kila moja inaupana wa mita 10 kwa barabara ndogo huku barabara kubwa ikiwa na upana wa mita 30 na urefu wa kilometa 12”.

Akafafanua kua: “Kazi ya uwekaji lami imepitia hatua nyingi, baada ya kumaliza ujenzi wa nyuma, ilitengenezwa mitaro ya maji ya mvua pamoja na njia za maji taka ikiwa pamoja na kuangalia utakavyo kua muinuko wa barabara, ambapo mambo yafuatayo yalifanyika:

  • 1- Upasuaji wa barabara na kuziwekea vipimo vya muinuko na muinamo wake.
  • 2- Kuweka tabaka la udongo msafi pamoja na kutengeneza tabaka la udongo utakao linda mabomba yanayo pita chini ya barabara.
  • 3- Kuweka tabaka la changarawe.
  • 4- Kushindilia na kusawazisha barabara zote.
  • 5- Kuweka ujazo mwingine baada ya kushindilia.
  • 6- Kuweka ujazo wa sentimita 5 wa lami mchanganyiko.
  • 7- Kushindilia na kusawazisha tena.
  • 8- Kuweka tabaka nyingine ya ujazo wa sentimita 5 wa lami.
  • 9- Kufanya ushindiliaji na usawazishaji wa mwisho.
  • 10- Kuweka lami ya mwisho kwa viwango na wasifu uliopangwa”.

Akaendelea kusema kua: “Hakika kazi hii inaenda haraka na kwa ustadi mkubwa ili ikamilike ikiwa katika ubora mzuri na imara”.

Tunapenda kusema kua; lengo la mradi huu ni kuonyesha thamani ya juhudi kubwa zinazo fanywa na watumishi wa Atabatu Abbasiyya tukufu katika kuwahudumia watu wanao kuja kumzuru Abulfadhil Abbasi (a.s) na kwa ajili ya kuwapatia makazi bora yanayo endana na maendeleo ya nyumba za kisasa, nyuma hizi zitagawiwa kwao kwa bei ya punguzo.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: