Muungano wa wasambazaji wa vitabu wa Misri wapongeza mafanikio yaliyo fikiwa katika maonyesho ya vitabu ya kimataifa katika mji wa Karbala na waombo kuto zuwiwa kushiriki kituo chochote cha usambazaji kutoka Misri katika maonyesho hayo..

Maoni katika picha
Rais wa muungano wa wasambazaji wa vitabu wa Misri Ustadhi Aadil Misriy amesifu mafanikio yaliyo fikiwa na maonyesho ya vitabu ya kimataifa yaliyo fanyika miaka ya nyuma ambayo hupata mafanikio mazuri kila mwaka upande wa taasisi zinazo shiriki na upande wa vitabu vinavyo onyeshwa ambavyo hubeba maudhui mbalimbali na mitazamo tofauti.

Hayo yalisemwa katika kikao alicho fanya mkuu wa maonyesho ya vitabu ya kimataifa katika mji wa Karbala Sayyid Muyassir Hakim katika mji mkuu wa Misri Kairo aliko enda kwa ajili ya kutoa mualiko rasmi wa kuwataka washiriki katika maonyesho ya kumi na tatu yatakayo fanyika mwanzoni mwa mwezi wa Shabani ujao 1438h, sambamba na kongamano la Rabii shahada la kimataifa na kitamaduni ambalo huandaliwa na kusimamiwa na Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya kama sehemu ya kusherehekea kuzaliwa kwa wajukuu wa mtume (s.a.w.w).

Sayyid Muyassir Hakim alifafanua kua: “Hakika muungano wa wasambazaji wa vitabu wa Misri wameshajihisha vituo vya usambazaji vya Misri kushiriki maonyesho haya ampapo ni muendelezo wa ushiriki wao katika miaka ya nyuma waliyo pata mafanikio na muitikio mkubwa kwa sababu waandishi wa Misri wanapendwa sana na wasomaji wa kiiraq, na mualiko huu tunaotoa kwenu unaonyesha wazi namna idara ya maonyesho haya inavyo thamini ushiriki wenu, pia tulijadiliana kuhusu namna ya ushiriki wa vituo vya usambazaji vya Misri na mambo ambayo tunaweza kuwarahisishia kama idara ya maonyesho haya, pia yalitolewa maeleza kuhusu malengo ya kufanyika kwa maonyesho hayo kila mwaka,na maelezo kuhusu kongamano la Rabii shahada la kimataifa na kitamaduni ambali maonyesho haya ni miongoni mwa ratiba za kongamano hilo”.

Akaendelea kusema kua: “Hakika muungano wa wasambazaji wa vitabu wanaona maonyesho ya vitabua ya kimataifa katika mji wa Karbara ni jambo zuri sana, ukizingatia kua yanafanyika Iraq pamoja na matatizo yote yanayo ikumba nchi hiyo, hii ni dalili kua watu wa Iraq wanajitambua na wanakiwango cha juu kabisa cha maadili mema.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: