Idara ya intanet katika Atabatu Abbasiyya tukufu yazindua program katika simu za kisasa (smart phone)..

Maoni katika picha
Miongoni mwa mfululizo wa program za simu za kisasa (smart phon) na katika kuhakikisha tunanufaika na teknolojia ya kisasa na kuitumia katika njia sahihi, idara ya intanet chini ya kitengo cha habari na utamaduni katika Atabatu Abbasiyya tukufu imezindua program mpya kwa jina la (Faraaidh) inayo lenga kupangilia namna ya kulipa swala za faradhi, program hii itapatikana katika simu za kisasa (smart phone), imeundwa na kusanifiwa kwa njia ya (Android) na inafanya kazi kwa njia hiyo hiyo.

Program inasehemu nyingi na njia mpya za kuitumia, miongoni mwa sehemu zake ni:

  • 1- Nyakati za swala, kuna ishara itakayo kukumbusha kuingia kwa wakati wa swala.
  • 2- Mtumiaji anaweza kutambua muda wa swala kutokana na mahala alipo.
  • 3- Kujua idadi ya swala anazotakiwa kuswali kila siku.
  • 4- Kila siku itakupa ujumbe unao kujulisha idadi ya swala ulizo swali.
  • 5- Unaweza kupakua (download) moja kwa moja.
  • 6- Upakuaji wake ni rahisi wala hauingiliani na program zingine.
  • 7- Inachukua nafasi ndogo, haitumii nafasi kubwa katika simu yako.

Program hii kwa sasa inapatikana katika (Google Play) unaweza kupakua (download) sasa hivi kwa anuani ifuatayo:

https://play.google.com/store/apps/details?id=alkafeel.net.sallat
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: