Kukamilka kwa maandalizi ya uzinduzi wa mradi wa upanuzi wa haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s) upande wa upauaji wa uwanja wa haram tukufu na watumishi wake watoa zawadi kwa kipenzi wao Zaharaa (a.s) katika kumbukumbu ya kuzaliwa kwake..

Jukwaa la hafla
Kamati iliyo pewa jukumu la kuandaa sherehe za uzinduzi wa mradi wa upanizi wa haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s) upande wa upauaji, imekamilisha maandalizi ya sherehe za uzinduzi huo, utakao fanyika leo siku ya Juma Mosi (19 Jamadil Aakhira 1438 h) sawa na (18 Machi 2017 m) baada ya swala ya Isha, kama sehemu ya kuadhimisha siku ya kuzaliwa kwa bibi Fatuma Zaharaa (a.s), hivyo mradi huu mkubwa utakua sawa na zawadi ya watumishi wa Abufadhil Abbasi (a.s) kwa kila anaye mpenda katika usiku huu mtukufu, pia kamati ya maandalizi ilitangaza kua sherehe hizo zitafanyika eneo la mkabala na mlango wa Qibla ndani ya uwanja wa haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s), kwa kua sehemu hiyo inauwezo wa kuingiza watu wengi zaidi, ratiba ya sherehe itakua kama ifuatavyo:

Kwanza: Kisomo cha Qur’an tukufu.

Pili: Ataongea kiongozi wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya tukufu Muheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi.

Tatu: Ataongea kiongozi wa wakfu Shia Muheshimiwa Sayyid Alaa Mussawiy.

Nne: Qaswida ya kimashairi itakayo somwa na naibu katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu Ustadh Ali Swafaar.

Tano: Ujumbe wa kitengo cha miradi ya kihandisi katika Atabatu Abbasiyya tukufu utakao wasiliswa na Muhandisi Dhiyaa-u Majidi Swaaigh.

Sita: Ujumbe wa watekelezaji wa mradi ambao ni shirika la Aridhi tukufu la ujenzi utakao wasilishwa na kiongozi mtendaji Muhandisi Hamidi Majidi.

Saba: Qawida ya kishairi.

Nane: Itaonyeshwa filamu inayo elezea hatua zilizo pitiwa katika ujenzi, iliyo andaliwa na ofisi ya wapiga picha na waandaaji wa vipindi wa Atabatu Abbasiyya tukufu.

Tisa: Wahudhuriaji watanawirisha macho yao kwa kutolewa pazia katika mradi huu na kuanza kwa enzi za jengo jipya la Atabatu Abbasiyya tukufu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: