Kikosi cha Abbasi (a.s) cha wapiganaji chaaga nyota miongoni mwa nyota zake anaye ingia miongoni mwa mashahidi wanao hami Iraqi na maeneo yake matukufu na roho ya mama yakataa kutengana na roho ya mwanawe..

Maoni katika picha
Ndani ya ukumbi mtukufu wa malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) kikosi cha Abulfadhil Abbasi (a.s) cha wapiganaji kimesindikiza mwili wa Said (Qahtwaan Dakhil Waailiy) aliye pata shahada akiwa analinda maeneo matukufu na dini, akiitikia wito wa kiimani na fatwa ya Marjaa dini mkuu ya kulinda maeneo matakatifu.

Shahidi Said alipata utukufu wa shahada katika lango la upande wa kulia (wa Mosul) katika oporeshen ya (Tunakuja ewe Nainawa) ambayo wanapigana majemedari wa kikosi cha Abbasi (a.s) bega kwa bega na jeshi la Iraq.

Kwa sababu ya subira yake ndiyo ilimuwezesha mwanawe kupambana na kupta shahada.. mama wa shahidi (Qahtaan Waailiy) mara tu baada ya kupata taarifa ya kufariki kwa mwanawe kipenzi roho yake ilitengana na uhai, akafariki. Kanakwamba alikataa mtoto wake asiende pekeyake, bali afuatane naye na aone jinsi mwanawe anavyo ungana na msafara wa imamu Hussein (a.s) pamoja na mashahidi wema.

Hajjat mama wa Shahidi Qahtwaan baina ya utukufu wa milele, roho yake ilitoka baada ya kupata habari ya kufariki kwa mwanawe, kana kwamba ameenda kumpa pole mama Wahabi (r.a) katika tukio la Twafu.

Marehemu hawa wamepata usindikizwaji mkubwa sana, kwanza wamefanyiwa ziara ya Sayyid Shuhadaau (a.s) na swala ya jeneza katika ukumbi wa haram ya Husseiniyya tukufu, kisha miili yao ikapelekwa katika malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) kupitia uwanja wa katikati ya haram mbili tukufu, huku sauti za wasindikizaji zikiita (Labbaika yaa Hussein) na (Uwe mbali kwetu udhalili), halafu ilisomwa ziara ya Abulfadhil Abbasi (a.s) na ziara ya imamu Ridha (a.s) pamoja na ziara ya imamu Hujjah Swaahibu Asri wa Zamaan (a.f) kwa niaba ya shahidi Said na mama yake kisha wakapelekwa katika nyumba zao za mwisho.

Mwenyezi Mungu amrehemu mama wa shahidi na amrehemu shahidi wetu na awaweke mahala pema peponi, sote ni wa Mwenyezi Mungu na sote tutarejea kwake.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: