Kamati ya maandalizi ya kongamano la pili la fatwa ya kujilinda yatangaza mashindano ya watoto ya kuandika ushujaa wa jeshi la serikali na Hashdi Sha’abi..

Maoni katika picha
Kamati ya maandalizi ya kongamano la pili kuhusu fatwa ya kujilinda linalo lenga kuwazowesha watoto kushiriki katika mashindano ya kitaifa, ambalo huwataka watoto waandike kuhusu ushujaa wa wapiganaji wa jeshi letu tukufu na Hashdi Sha’abi pamoja na visa vya kujitolea na vya kuipenda nchi yao, imetangaza mashindano ambayo yatafanyika katika kongamano litakalo simamiwa na kitengo cha habari na utamaduni cha Atabatu Abbasiyya tukufu kwa ajili ya kuhuisha kumbukumbu ya fatwa tukufu ya kujilinda chini ya kauli mbiu isemayo (Fatwa…ni chemchem ya ushindi na miski ya shahada).

Kamati imeweka taratibu na kanuni zifuatazo:-

  • 1- Kisa kiandikwe kwa kufuata misingi ya kielimu na kimaadili.
  • 2- Kisa kielezee ujasiri wa jeshi la Iraq na Hashdi Sha’abi kwa picha ya jumla (bila kumlenga mtu) katika kulinda nchi, maeneo matukufu, misingi ya kibinadamu na kimazingira.
  • 3- Kisiwe kimesha wahi kutolewa, imma kwenye kitabu au mitandaoni au kimesha wahi kutolewa katika mashindano mengine.
  • 4- Kiandikwe na kuhifadhiwa katika CD kwa program ya word na kiwasilishwe katika kitengo cha Habari na Utamaduni cha Atabatu Abbasiyya tukufu pamoja na wasifu (CV) wa muandishi, au tuma kwenye email ifuatayo, (info@holyfatwa.com).
  • 5- Mwisho wa kupokea ni 05/05/ 2017 m.
  • 6- Nakala tano zitakazo shinda zitachapishwa kwa gharama ya Atabatu Abbasiyya pamoja na kutolewa zawadi maalumu kwa wahusika.

Kuna zawadi tano zimeandaliwa kwa visa vitano vitakavyo shinda, kila kimoja kitapewa laki mbili (200,000) dinari za Iraq.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: