Ugeni wa Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya watembelea majaalisi za kuomboleza mashahidi wa kikosi cha Abbasi (a.s) walio pata shahada hivi karibuni katika vita ya kukomboa mji wa Mosul..

Maoni katika picha
Ugeni kutoka katika Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya jana Juma Nne (23 Jamadil Aakhira 1438 h) sawa na (22 Machi 2017 m) walitembelea vikao vya kuomboleza mashahidi wa kikosi cha Abbasi (a.s) walio pata shahada hivi karibuni katika vita inayo endelea ya kukomboa mji wa Mosul katika oporesheni ya (Tunakuja ewe Nainawa), vilivyo fanyika katika mkoa wa Basra, na kutoa rambirambi kwa familia za mashahidi pamoja na kupongeza ushujaa wa watoto wao na namna walivyo jitolea katika kuitikia wito wa Marjaa dini mkuu hadi wakafanikiwa kupanda meli ya Sayyid Shuhadaau imamu Hussein (a.s).

Jaula ilihusisha vikao vya kuomboleza mashahidi watatu, ambao ni; Shahidi Qahtwaan Al-waailiy, Haidari Muslim Al-maalikiy kutoka katika kikosi cha Abbasi (a.s) na Shahidi Karaar Ni’imatul-imaara kutoka katika kikosi cha Ali (a.s) chini ya Atabatu Alawiyya tukufu.

Ugeni uliongozwa na rais wa kitengo cha dini katika Atabatu Abbasiyya tukufu Shekh Swalaah Karbalai ambaye aliuambia mtandao wa Alkafeel kua: “Tupo pamoja na mashahidi, na leo tumekuja kutembelea vikao vya maombolezo vinavyo fanywa na ndugu zao, vya kuwarehemu watukufu hao na kuonyesha kujali namna walivyo jitolea damu zao tukufu kwa ajili ya kulinda aridhi ya Iraq, raia wake na maeneo matukufu, wakiitikia wito wa Marjaa dini mkuu, tumekuja kutoa rambi rambi pamoja na zawadi ndogo zikiwemo za kutabaruku pamoja na pendera ya Abulfadhil Abbasi (a.s), ziara yetu ilianzia kwa Shahidi Qahtwaan Waailiy, ambaye alipigana kwa ushujaa mkubwa sana pamoja na majeraha makubwa aliyo kua nayo, alirejea katika uwanja wa vita na akapigana hadi akapata utukufu wa shahada katika vita ya kukomboa mji wa Badushi na kuungana na ndugu yake shahidi, na mama yake alipo ona mwili wake akaaga dunia na kuungana na mwanaye, Sayyid Ahmad Swafi aliathirika sana na tukio hili, akatutaka tuhudhurie na ugeni mkubwa katika kikao cha maombolezo ya shahidi huyu mtukufu, katika ujio wetu tumefuatana na ndugu zetu watumishi wa Atabatu Husseiniyya tukufu”.

Akaendelea kusema kua: “Kisha tulienda kutembelea kikao cha maombolezo ya shahidi Karaar Ni’imatul-Imarah, aliye kua mpiganaji wa kikosi cha imamu Ali (a.s) kilicho chini ya Atabatu Alawiyya tukufu, na tuliona namna mzazi wa shahidi alivyo pokea bendera ya Abulfadhil Abbasi (a.s) kwa machozi mengi sana ikiwa kama ishara kua mzazi huyu atafufuliwa pamoja naye (a.s) inshallah, matembezi yetu yaliishia katika kikao kilicho fanywa na Shekh Salim Maliki kiongozi wa kikosi cha Habibu bun Mudhahir (a.s) cha kuomboleza mwanawe shahidi Haidari aliye lelewa katika haram tukufu ya Abulfadhil Abbasi (a.s) na alikua anasoma dini, ilipo tolewa fatwa tukufu ya jihadi akaungana na kikosi cha wapiganaji, amepambana hadi kapata shahada (r.a), tunamuomba Mwenyezi Mungu mtukufu awakubalie muhanga wao na awafufue pamoja na Sayyid Shuhadaau imamu Hussein (a.s).

Akamalizia kwa kusema: “Kwa hakika tunapo tembelea familia za mashahidi tunahisi furaha na utukufu, hasa tunapo busu mikono yao, hili ni jambo dogo tunalo weza kufanya kwao, hata kama wakiwa mbali kiasi gani tutaenda kuomboleza na kuwapa pole, huu ni wajibu wetu”.

Ndugu wa mashahidi kwa ujumla walifurahi sana kutembelewa na ugeni huu mtukufu kutoka katika Ataba mbili, na wakasema hili ni jambo kubwa sana kwao, pia waliona ni fahari kwao, watoto wao kupata shahada na kuungana na Sayyid Shuhadaau (a.s).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: