Ushiriki wa watafiti wa ndani na nje ya Iraq: ufunguzi wa kongamano la kwanza la kimataifa na kitamaduni Ruhu Nubuwwah..

Maoni katika picha
Kongamano la kwanza la wanawake Ruhu Nubuwwah la kitamaduni na kimataifa linalo simamiwa na idra ya shule za Alkafeel za wasichana chini ya kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinadamu cha Atabatu Abbasiyya tukufu chini ya kauli mbiu isemayo: Zaharaa (a.s) ni hazina ya elimu na kilele cha hekima, asubuhi ya siku ya Ijumaa ya tarehe (24 Jamadil Aakhira 1438 h) sawa na (24 Machi 2017 m) wamefungua kikao cha kongamano kikiwa na washiriki wanawake watafiti wa ndani na nje ya Iraq.

Kongamano lilifunguliwa kwa Qur’an tukufu , na lilifanyika katika ukumbi mkuu wa kituo cha Swidiqa Twahira (a.s), lilipata muitikio mkubwa wa watafiti wa kisekula na wadau muhimu, liliongozwa na dokta Nawwaal A’aidi, na tafiti zake zilikua kama zifuatazo:

Utafiti wa kwanza: Wa Ustadhat Zaiba Abdunnabi Khiyami kutoka Baharain, ameandika kwa anuani isemayo: (Maisha ya kiutendaji ya bibi Zaharaa -a.s-) utafiti wake umeelezea maisha ya imamu Ali na bibi Fatuma (a.s) katika kutengeneza familia, kafafanua misingi kumi na nne inayo inua hadhi ya nyumba.

Utafiti wa pili: Wa Dokta Fatuma Karim Rasan kutoka chuo kikuu cha Bagdad utafiti wake umebeba anuani isemayo: (Mwenendo wa kimalezi katika hotuba ya Zaharaa (a.s) ya kuelekeza Umma.. nguvu ya hoja kwa ushahidi wa Qur’an kama mfano) alifafanua uwezo mkubwa alio kua nao bibi Zaharaa (a.s) katika kujenga hoja.

Utafiti wa tatu: Wa Dokta Anwaar Majidi Sarhani kutoka chuo kikuu cha Bagdad, utafiti wake ulihusu (Hotuba za wanawake na athari yake katika jamii.. hotuba ya bibi Fatuma Zaharaa kama mfano), Utafiti ulielezea zaidi vipengele vya hotuba ya bibi Fatuma Zaharaa (a.s) na njia ya uongeaji aliyo tumia pamoja na ufasaha wake wenye athari kubwa kwa wasikilizaji.

Utafiti wa nne: Wa Ustadhat Twayyiba Ibrahim Asadu-llahi, uliokua na anuani isemayo: (Mfano bora wa maisha ya ndoa katika sira ya Fatuma Zaharaa -a.s-) na athari ya maelewano ya wanandoa katika kujenga furaha ya ndoa.

Kisha washiriki walijadili utafiti wa Ustadhat Twayyiba Ibrahim Asadu-llahi, kwa kutoa maoni na maelezo yenye manufaa kwa washiriki na kupata elimu zaidi.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: