Kundi la waumini wahuisha kumbukumbu ya kuuawa kishahidi kwa Amirulmu-uminina (a.s) mbele ya malalo yake matukufu..

Maoni katika picha
Nyoyo zilizo jaa huzuni na macho yanayo bubujika machozi, mji mtukufu wa Najafu umefurika mamilioni ya mazuwaru waliokuja katika malalo ya imamu Ali bun Abuutwalib (a.s) kuhuisha kumbukumbu ya kuuawa kwake kishahidi kutoka ndani na nje ya Iraq, ambayo ilisadifiana na siku ya jana Ijumaa ya tarehe 20 Ramadhani 1438 hijiriya sawa na tarehe 16 Juni 2017 miladiya, na kuhuisha ahadi ya uaminifu na baiyya ya milele kwake na kufuata mwenendo wake mtukufu, njia zinazo elekea katika malalo yake tukufu zilijaa makundi ya watu na vituo vya Husseiniyya vinavyo toa huduma ya futari na daku pamoja na mambo mengine kwa mazuwaru (watu wanaokuja kufanya ziara), hali kadhalika kuna uwepo wa vikundi vya maombolezo ndani na nje ya mkoa wa Najafu, pia vyombo vya ulinzi na usalama pamoja na watumishi na wana habari wamefanya kila wawezalo katika kuhudumia mazuwaru watukufu.

Mkuu wa mkoa wa Najafu Luaiy Yasiriy amesema kua zaidi ya wairaq milioni tatu na wageni kutoka nchi za kiarabu na kiajemi laki moja na nusu wamekuja kumzuru imamu Ali (a.s).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: