Kongamano la Alkafeel la kimataifa kuhusu makumbusho litakua na washiriki wa kitaifa na kimataifa..

Maoni katika picha
Kamati ya maandalizi ya kongamano la Alkafeel la kimataifa litakalo endeshwa na makumbusho ya Atabatu Abbasiyya tukufu mwezi ujao imesema kua, kongamano hilo litakua na ushiriki mkubwa wa kitaifa na kimataifa, watoa mada watakua ni watafiti walio bobea katika maswala ya makubusho, hivyo litakua na hadhi ya kimataifa, pia mialiko imetolewa kwa watu muhimu na wamedhibitisha ushiriki wao.

Rais wa makumbusho ya Alkafeel ya vifaa na nakala kale katika Atabatu Abbasuyya tukufu na mjumbe wa kamati ya maandalizi ya kongamano hili, Ustadh Swadiq Lazim aliongeza kusema kua: “Kongamano litaanza sambamba na mitihani ya awamu ya pili ya wanafunzi wa chuo, litafunguliwa tarehe saba ya mwezi wa tisa na litachukua siku mbili chini ya kauli mbiu isemayo (Makumbusho ni mazingira na uchumi), kamati ya elimu yenye jukumu la kuandaa mada inaendelea kuandaa vielelezo muhimu vya mada zao kwa mujibu wa masharti na kanuni zilizo wekwa”.

Akasisitiza kua: “Kongamano hili litakua tofauti na yaliyo tangulia kwa sababu watashiriki watalamu kutoka nchi za kiarabu na kiajemi (zisizokua za kiarabu) litakua na wahadhiri kutoka Misri, Ujerumani, Japan, Iran pamoja na wairaq kutoka vyuo tofauti vya Iraq”.

Kumbuka kua kongamano hili ni miongoni mwa makongamano na harakati nyingi zinazo fanywa na Ataba tukufu kwa ajili ya kufungua miliango ya mawasiliano na kubadilishana uzoefu katika ulimwengu wa elimu za kisasa, ndio maana watashiriki wataalamu walio bobea katika mambo ya makumbusho wa ndani na nje ya Iraq, kongamano hili linalenga mambo yafuatayo:

Kwanza: Kuhifadhi urithi wa kimazingira na kiuchumi.

Pili: Kusaidia taasisi za kidini kuanzisha vituo vya makumbuso na kuendeleza kazi za maswala ya makumbusho.

Tatu: Kufungua mlango wa kusaidiana baina ya taasisi za makumbusho za kitaifa na kimataifa na kuziendeleza.

Nne: Kuongeza uwelewa kuhusu makumbusho kutakako changia kuzitambua na kuongezeka uchumi wake.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: