Kiongozi wa kisheria wa Atabatu Abbasiyya tukufu akutana na balozi wa India nchini Iraq na kujadiliana naye namna ya kuongeza ushirikiano baina yao..

Sehemu ya kikao
Kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya tukufu Sayyid Ahmad Swafi (d.i) amekutana na balozi wa India hapa Iraq katika ukumbi wa utawala wa Ataba tukufu, miongoni mwa mambo waliyo jadiliana ni namna ya kuongeza ushirikiano baina ya Iraq na India.

Kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya tukufu, alimkaribusha Mheshimiwa balozi na ugeni alio fuatana nao, akawaambia kua Iraq ni nchi yao ya pili, Sayyid Swafi (d.i) akaelezea mambo mbalimbali, miongoni mwa mambo hayo ni kufungua ushirikiano katika sekta za elimu na biashara baina ya India na Iraq, bila kusahau sekta ya afya, pamoja na kuweka wepesi katika mambo yatakayo rahisisha ushirikiano huo, kama vile upatikanaji wa viza na mengineyo, na akasisitiza kuendelea kwa ushirikiano baina ya hospitali ya Alkafeel na madaktari wa India, na chuo kikuu cha Ameed kitaendelea kupokea walimu wa utabibu watakao fanya kazi sambamba na wenzao wa hapa Iraq.

Naye balozi wa India, alianza kwa kuwapongeza raia wa Iraq kutokana na ushindi mkubwa waliopata dhidi ya magaidi ya Daesh, akasema kua; toka alipo wasili Bagdad na kuanza majukumu alikua na shauku kubwa ya kutembelea Atabatu Abbasiyya tukufu na kutoa shukrani zake kwao kutokana na kazi kubwa wanayo fanya ya kuwahudumia mazuwaru kutoka kila pembe ya dunia pamoja ya wanaotoka India.

Akaongeza kusema kua: “Nina furaha sana, pia ninashangazwa na ninayo yaona katika sehemu hii tukufu, tumesoma katika vitabu kuhusu sehemu hii takatifu, namshukuru Mwenyezi Mungu aliye niwezesha kuja kupatembelea, tuna mazaru (sehemu takatifu) nyingi nchini India lakini huduma mnazo toa hapa ni za hali ya juu kabisa”.

Mwisho wa mazungumzo yao walisisitiza umuhimu wa kuendelea kwa ushirikiano baina yao katika sekta zote kwa manufaa ya raia wa nchi zao, na umuhimu wa kubadilishana uzoefu katika sekta ya uchumi, mwisho kabisa Atabatu Abbasiyya tukufu ilimpa midani ya Ataba balozi wa India.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: