Watumishi wa Abulfadhil Abbasi (a.s) waweka mandhari nzuri ya Iddul-Ghadiir..

Maoni katika picha
Katika kuonyesha furaha yao kwenye mnasaba wa sikukuu ya Iddul-Gadiir, ambayo ni siku tukufu sana katika uislamu, nayo ni sikukuu ya tatu baada ya Iddul-Fitri na Adhha, watumishi wa Abulfadhil Abbasi (a.s) wameweka mandari nzuri katika haram tukufu.

Massayyid wanaofanya kazi katika Atabatu Abbasiyya wamesimama kila pembe ya haram tukufu wakiwa na mavazi rasmi huku wameshika maua kama ishara ya amani na upendo, vilevile ni ishara ya utii na mapenzi makubwa kwa kiongozi wa waumini Ali bun Abutwalib (a.s).

Tendo hili hufanywa na masayyid wanaofanya kazi katika Atabatu Abbasiyya kila mwaka, pamoja na kuonekana kama jambo dogo lakini ni kitendo cha kuonyesha utii na upendo wa hali ya juu kwa watu wa nyuma ya Mtume (a.s), pamoja na kufungamana nao kiroho, hakika wao ndio njia iliyo nyooka ambao Mtume (s.a.w.w) ametuhusia kushikamana nao, pia tendo hilo linaingiza furaha katika nyoyo za watu wanaokuja kufanya ziara.

Katika upande mwingine, watumishi wa shamba boy wa Alkafeel chini ya kitengo cha utumishi katika Atabatu Abbasiyya tukufu wameweka maua mazuri ya kupendeza katika milango ya Ataba tukufu ndani na nje, pia wamepamba eneo lote la haram kwa kuweka maua mazuri kuanzia kwenye uwanja wa katikati ya haram mbili (Husseiniyya na Abbasiyya) tukufu hadi ndani ya uwanja wa haram tukufu ya Abulfadhil Abbasi (a.s), na wameweka mabango mbalimbali baadhi yakiwa yamedariziwa na kuandikwa ujumbe wa kutoa mkono wa pongezi kwa mnasaba huu mtukufu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: