Kituo cha upigaji picha wa nakala kale na uwekaji wa faharasi chaingiza katika maktaba yake nakala kale (250) na chasema kua aina hizo ni nadra..

Sehehu ya utendaji kazi
Kituo cha upigaji picha wa nakala kale na uwekaji wa faharasi chini ya kitengo cha habari na utamaduni katika Atabatu Abbasiyya tukufu, kimefanikiwa kuingiza nakala kale (250) ambazo ni nadra katika hazina yake baada ya kukamilisha kazi ya kuzikarabati.

Kwa mujibu wa maelezo ya mkuu wa kituo Ustadh Swalaah Mahdi Abdulwahaab: “Zimepatikana kutokana na ushirikiano baina ya kituo chetu na maktaba ya imamu Haadi (a.s) ambayo ni miongoni mwa maktaba kubwa katika mji mtukufu wa Mashhadi, nakala kate hizi zinahususha mambo muhimu yanayo hitajika mara kwa mara, kutokana na vifaa vya kisasa vinavyo milikiwa na kituo chetu, tulizipiga picha na kuzifanyia ukarabati kwa kutengeneza nakala mbili kwa kila aina, moja ya maktaba kwa ajili ya kuhifadhi asili na nyingine ya kituo chetu”.

Akaoneza kusema kua: “Lengo la kufanya kazi hii ni kwa ajili ya kuhifadhi turathi zetu na kupanua wigo wa unufaikaji, pamoja na kuziingiza katika uwanja wa kutumika na watu wanao ingia maktaba au katika Intanet, nakala ya asili itatunzwa katika maktaba na kuilinda usiharibike na nakala ya fotokopi ndio itakayo tumika”.

Kumbuka kua kituo cha upigaji picha wa nakala kale na kuweka faharasi chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu, siku za nyuma kilifanya kazi ya kupiga picha na kukarabati nakala kale zingine ambazo ni za nadra katika maktaba za Pakistani na Landan, pamoja na maktaba za Iraq, hii ni sehemu ya utekelezaji wa majukumu iliyo jipangia ya kuzienzi na kuzitunza turathi za kiislamu, na hasa turathi za Ahlulbait (a.s), kuzipiga picha na kuzikarabatu halafu kuziingiza katika uwanja wa wasomaji na wahakiki.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: