Miongoni mwa ratiba ya kongamono la kimataifa la Ameed: mada za kitafiti zaendelea kuwasilishwa na watafiti wa ndani na nje ya Iraq kuhusu amani na utamaduni katika uwelewa na utekelezaji..

Maoni katika picha
Katika kongamano la kimataifa la Ameed lililo anza siku ya Alkhamisi, zimekua zikiwasilishwa mada za kitafiti, kutoka kwa watafiti wa ndani na nje ya Iraq, zinazo husu amani na utamaduni katika uwelewa na utendaji, kongamano lina vipindi viwili, cha kwanza kiliongozwa na dokta Aniisah Abuu Qaasim kutoka Iran pamoja na dokta Najmu Abdullahi Mussawiy kutoka Iraq, kikao kilifanyika katika ukumbi wa Imamu Hassan (a.s), ziliwasilishwa tafiti tano kama ifuatavyo:

  • 1- Utafiti wa dokta Khalid Muharam kutoka Lebanon kuhusu (Amani na utamaduni na mahitaji ya uhakiki wake).
  • 2- Utafiti wa Ustadh Hussein Alawiy Nasir kutoka Iraq kuhusu (Amani na utamaduni ni msingi muhimu wa kupatikana kwa amani ya mwanadamu).
  • 3- Utafiti wa Ustadh Ibtisaam Saadun Nuriy kutoka Iraq kuhusu (Mwelekeo wa wanafunzi wa shule za msingi kuhusu jihadi na wapiganaji wa Hashdi Sha’abi na jeshi la serikali).
  • 4- Utafiti wa dokta Wisaam Hussein Jaasim na dokta Ahmad Jaasim Muslim kutoka Iraq kuhusu (Amani na utamaduni wa sasa katika mtazamo wa thaura (mapambano) ya imamu Hussein a.s).
  • 5- Utafiti wa dokta Falaah Hassan Abbasi kuhusu (Athari za utandawazi katika kuharibu mahusiano na utulivu wa kiutamaduni).

Kikao cha pili kilifanyika katika ukumbi wa imamu Qassim (a.s) na kilihusisha tafiti zilizo wasilishwa kwa lugha ya kiengereza, jumla ya watafiti tisa kutoka Iraq, Uingereza, na Kanada waliwasilisha tafiti zao, mjumbe wa kamati ya maandalizi na msimamizi mkuu wa vikao vinavyo endeshwa kwa kiengereza alisema kua: “Amani na utamaduni vina mahusiano ya moja kwa moja na jamii zote pamoja na kutofautiana kwa tamaduni zao, kwani vimejikita katika misingi inayo kubalika kwa kila mtu na kwenye kila jamii, jumla ya tafiti zilizo wasilishwa kwa kiengereza zilikua (26) zikiwa na maudhui mbalimbali, ikiwepo moja yenye maudhui ya usalama wa kiteknolojia ambayo walishirikiana watafiti wawili kutoka Wingereza katika kuiwasilisha”.

Akaendelea kusema kua: “Tafiti za kilugha zilihusisha mpangolio wa hotuba za baadhi ya viongozi wa nchi na baadhi ya hotuba za kisiasa katika matumizi sahihi ya fani za lugha”.

Wahudhuriaji walipata nafasi ya kuuliza maswali na kutoa michango yao, na watoa mada walijibu maswali na kutoa ufafanuzi zaidi.

Kumbuka kua jumla ya tafiti zilizo wasilishwa katika kamati ya maandalizi zilikua (68), na zilizo pasishwa kuwasilishwa katika kongamano hili ni tafiti (50), tafiti (24) kiti ya hizo zimeandikwa kwa lugha ya kiarabu na (26) kwa lugha ya kiengereza, tafiti (34) zimefanywa na wairaq na (16) zimefanywa na washiriki kutoka katika nchi za: (Lebanon, Oman, Aljeria, Iran, Uingereza, Kanada, Italia na India).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: