Haya ndio aliyo usia Marjaa dini mkuu kwa wahadhiri na mubalighina katika mwezi wa Muharam 1438 hijiriyya..

Maoni katika picha
Unatujia mwezi mtukufu wa Muharam, ambao hua tunafanya kumbukumbu ya harakati kubwa iliyo ongozwa na watu waliokua na hima ya kurekebisha jamii na kuufanya umma uishi katika mazingira mazuri, ambayo ni harakati tukufu ya Imamu Hussein (a.s), kwa kukumbuka harakati hiyo tukufu, kunatupa jukumu kubwa sisi wafuasi wa imamu Hussein bun Ali (a.s), nalo ni jukumu la kulinda muendelezo wa harakati hiyo, na kurithisha athari na malengo yake katika nyoyo za watu.

Hili ni jukumu la kila mtu, sawa awe ni msomi wa dini au msomi wa mambo mengine miongoni mwa elimu za kibinadamu, kila mmoja miongoni mwetu anajukumu la kulinda harakati tukufu ya imamu Hussein (a.s) kwa kurekebisha nafsi yake na familia yake, pamoja na kuielezea jamii inayo mzunguka kuhusu umuhimu wa harakatu tukufu ya Imamu Hussein (a.s), lakini wahadhiri wanajukumu kubwa zaidi katika swala hili kwani wao ndio watengenezaji wa picha ya harakati tukufu ya Ashura iliyo ongozwa na imamu Hussein (a.s), hapa tunahitaji kujadili kidogo:

Je mimbari za Husseiniyya zinaendana na wakati katika kutekeleza jukumu hili, kiasi ambacho zinaleta athari tarajiwa katika nyoyo za watu?

Kutokana na nukta hiyo, tunatoa baadhi ya nasaha na maelekezo kwa kila atakaye panda katika mimbari ya Sayyid Shuhadaau (a.s):

  • 1- Kuzungumzia maudhui mbalimbali, hakika jamii inahitaji maudhui za kiroho, kimalezi na kihistoria, hivyo mzungumzaji anatakiwa aguse sehemu zote, ili aweze kukata kiu ya wasikilizaji.
  • 2- Muhadhiri anatakiwa atambue mambo yaliyopo katika zama zake, aweze kutambua utata mbalimbali unaotokea wa ki-aqida na mambo mengine ambayo huzuka katika kila jamii, atakapo zungumzia mambo yaliyopo katika jamii watu watavutika zaidi na kumsikiliza na maneno yake yatakua na athari kubwa.
  • 3- Muhadhiri anatakiwa kua makini anapo nukuu aya, hadithi au kisa, na anukuu kutoka katika vitabu vinavyo kubalika, kwani unapo kosea kusoma aya au hadithi au ukanukuu kisa kimakosa, itasababisha kupunguza uzito wa mimbari ya Husseiniyya na kupunguza uaminifu kwa wasikilizaji.
  • 4- Ajiepushe kutaja visa vya kubuni (paukwa pakawa) au vya kufikirika, kwani vinapunguza heshima ya mimbari ya Husseiniyya na kufanya idharaulike na kupuuzwa na wasikilizaji.
  • 5- Maandalizi mazuri, muhadhiri anatakiwa kuipangilia mada yake, na achague maneno na namna nzuri ya uwasilishaji, itakayo vutia wasikilizaji. Hakika muhadhara ulio pangiliwa na ukawasilishwa vizuru huvutia watu wengi.
  • 6- Hakika Ahlulbait (a.s) wanaturathi nyingi sana, na zote ni nzuri, inategemea uwezo wa mzungumzaji kukusanya hadithi zitakazo endana na watu anao wahutubia, na kuifanyia kazi kauli yao (a.s) isemayo (Hakika watu lau wangejua mazuri yetu wangetufuata), mazuri hayo ni turathi zao, zinazo zungumzia matukufu ya binadamu na kumvutia kila mtu bila kujali tofauti za mila wala dini.
  • 7- Kutaja matatizo yaliyopo katika jamii na kuelekeza tiba yake, sio vizuri mzungumzaji kukwepa kutaja matatizo yaliyopo katika jamii inayo mzunguka, kama vile matatizo wa familia, au tabaka la vijana na wazee, au matatizo ya talaka na mengineyo, hii itasaidia kutatua matatizo yaliyopo katika jamii, hivyo mhadhiri anaweza kuomba ushauri kwa wazee na watu wenye hekima anapo taka kuzungumzia matatizo yaliyopo, ili wajadili utatuzi wa matatizo hayo kwa pamoja, jambo hili litaifanya mimbari ya Husseiniyya kua hai na kuchukua nafasi ya uongozi na kurekebisha jamii.
  • 8- Ajiepushe na kuzungumzia tofauti za kimitazamo zilizopo, kwani kuzungumzia tofauti huleta mpasuko na huvunja maelewano, pia husababisha ugomvi baina ya waislamu, wakati mimbari ya Husseiniyya ni kielelezo cha umoja na mshikamano hasa kwa wapenzi wa Sayyid Shuhadaa (a.s).
  • 9- Kuyapa umuhimu mas-ala ya kifiqhi, hasa katika sekta ya ibada na kuyaelezea kwa ufasaha kiasi watu wahisi wanaishi katika mazingira halisi ya mimbari ya Husseiniyya.
  • 10- Kutilia mkazo swala la utii wa Marjaiyyah na umuhimu wa hauza (masomo ya dini) hakika hiyo ndio siri ya nguvu ya madhehebu ya Imamiyya.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: