Mtandao wa Alkafeel wafanya ziara za kwa niaba zaidi ya elfu 24 katika kipindi cha ziara ya Arubaini, na idara yatenga zawadi kwa mazuwaru kumi…

Maoni katika picha
Idara inayo fanya ziara kwa niaba chini ya ofisi ya mtandao wa kimataifa Alkafeel, imesema kua; idadi ya watu waliofanyiwa ziara kwa niaba katika kipindi cha ziara ya Arubaini imefika (24500) kutoka nchi mbalimbali na kupitia mitandao yake yote (Kiarabu, Kiengereza, Kiurdu, Kituruki, Kifarsi, Kijerumani, Kiswahili na Kifaransa), walifanyiwa ziara ya Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s) pamoja na swala ya rakaa mbili na dua.

Asilimia kubwa ya watu walio jisajili katika ziara hii iliyo fungua milango ya usajili siku (10) kabla ya siku ya ziara, wanatoka katika nchi zifuatazo: (Iraq, Baharain, Saudia, Yemen, Qatar, Kuwait, Sirya, Lebanon, Tunisia, Misri, Morocco, Oman, Swiden, Denmak, Norway, Austria, Marekani, Kanada, Finland, Jodan, Landan, Krashia, Czech, Afughanistan, India, Pakistan, Uturuki, Iran) pamoja na nchi zingine.

Idara ya mtandao wa kimataifa Alkafeel imeandaa zawadi ya tabaruku kutoka katika malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) kwa mazuwaru kumi walio jisajili, itafanyika kura ya kuchagua majina hayo kisha yatatangazwa.

Kumbuka kua ziara kwa niaba ni miongoni mwa huduma zinazo tolewa na mtandao wa Alkafeel, (ambao ni mtandao rasmi wa Atabatu Abbasiyya tukufu) kwa wafuasi wote wa Ahlulbait (a.s) na wapenzi wao, unamilango mingi inayo fundisha mambo ya kitamaduni na kiutumishi na unamsaidia kila mwenye kutafuta haki.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: