Marjaa dini mkuu: Kuishi kwa amani kunahitaji kufuata misingi ya maelewano na maongezi katika kutatua matatizo na mizozo…

Maoni katika picha
Marjaa dini mkuu ameendelea kubainisha misingi ya kua raia mwema, kupitia mimbari ya swala ya Ijumaa na katika ulimi wa mwakilishi wake Shekh Abdulmahdi Karbalai, ambaye ameeleza kua: Hakika raia mwema anatakiwa afuate misingi ya mazungumzo na maelewano katika kutatua migogoro.

Amesema: “Kutatua mizozo na migogoro inatakiwa iwe kwa kutumia mazungumzo na maelewano hata kama utatuzi utakawia. Raia mwema hujiepusha na kutumia nguvu na kushambulia anapokua na matatizo na watu wengine, ndugu zangu nitakapo kua na tatizo na mtu mwingine yanipasa nitafute njia za amani katika kutatua tatizo hilo, kama vile kuanzisha naye mazungumzo, kama isipo wezekana naweza kutumia watu wengine wenye hekima na busara na wanao heshimika katika jamii kwa ajili ya kutatua tofauti zetu kwa amani, ikishindikana tunaenda katika utaratibu wa kisheria..

Kwa bahati mbaya, mara nyingi imetokea mizozo kwa mambo madogo madogo na watu hukimbilia kushutumiana na kutumia nguvu kila mmoja anataka kuonyesha nguvu zake katika kutatua jambo hilo.

Misingi ya raia mwema, yatupasa tuitumie katika nyumba zetu na katika familia zetu kisha tuitumie sokoni, barabarani, shuleni na kila sehemu sawa liwe ni tatizo la mtu na mtu au jamii na jamii nyingine. Wakati mwingine hutokea mizozo baina ya makabila, watu wengi wameripoti kutokea mizozo katika baadhi ya mikoa, kuna watu waligombania kipande cha aridhi na wakauawa watu wanne, jambo hili linaingia akilini? Je haya ndio mafundisho ya uislamu? Ugonvi wa aridhi ndogo tu watu mnauana!!? Uislamu uko mbali na mambo hayo..

Akasisitiza kua: “Linapo tokea tatizo baina yangu na mtu mwingine sitakiwi kutumia nguvu katika kutatua tatizo hilo.. naweza kutumia kuongea kwa utulivu na upole na tatizo likaisha, badala ya kutumia hasira na ugongi ambao husababisha kuumizana na kuuana na kuleta migogoro isiyo isha.

Raia mwema anatakiwa kutumia njia ya mazungumzo na maelewano katika kutatua migogoro na mizozo.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: