Kufuatia kuzaliwa kwa Mtume mtukufu, Atabatu Abbasiyya tukufu kwa kushirikiana na chuo kikuu cha Qadisiyya yafanya kongamano la mnasaba huu…

Maoni katika picha
Chini ya usimamizi wa uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu, chuo kikuu cha Qadisiyya kimefanya kongamano la kusherehekea kuzaliwa Mtume wa ubinadamu Muhammad (s.a.w.w), huu ni muendelezo wa makongamano yanayo fanywa na kituo cha masomo na utafiti Al-Ameed kilicho chini ya kitengo cha habari na utamaduni katika Atabatu Abbasiyya tukufu kwa kushirikiana na vyuo vikuu vya Iraq.

Kongamano hili lilifunguliwa kwa Qur’an tukufu, kisha ikasomwa surta Fat-ha kwa ajili ya kuwarehemu mashahidi wa Iraq, halafu ikaonyeshwa filamu inayo elezea kuzaliwa kwa Mtume (s.a.w.w) na sehemu ya maisha yake.

Ukafuata ujumbe wa uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu, ulio wasilishwa na dokta Aadil Nadhiir, miongoni mwa aliyo sema ni: “Bila shaka! Kukutana kwetu leo wingu la rehma ya Mwenyezi Mungu limetufunika, kwa sababu kukutana kwetu huku tunatekeleza agizo la Ahlulbait (a.s) walipo sema (Huisheni mambo yetu, Mwenyezi Mungu amrehem atakaye huisha mambo yetu), tumekutana kwa ajili ya jambo gani? Jambo gani kubwa tunalo huisha? Hakika ni kuzaliwa kwa mtume mtukufu (s.a.w.w), na sisi wote hapa tunadhihirisha furaha zetu kwa maimamu watakasifu (a.s), hususan Imamu Swahibu Zamaan (a.f), na kwa maraajii watukufu wa umma wa kiislamu, tunamuomba Mwenyezi Mungu akubali ibada zetu katika siku hii tukufu, pongezi kwenu wote kwa huu uzawa mtukufu.

Hakika kuhuisha tukio hili enyi ndugu zangu, hakutakua na faida bila naia ya kweli na ikhlasi itakayo tafsiriwa na kufuata mwenendo wa Mtume (s.a.w.w) katika nyanja mbalimbali za maisha yetu, kuna haja kubwa katika jamii za waislamu kufuata maelekezo ya Mtume, Atabatu Abbasiyya tukufu imekua ikihuisha daiama, kila tukio lenye uhusiano na Mtume Muhammad (s.a.w.w), kwa kutumia njia mbalimbali za kijamii na kielimu, kutokana na umuhimu wa kunufaika na wasomi wa kisekula na wa kidini katika zama zetu, Ataba Tukufu ilianzisha kituo cha masomo na utafiti Al-Ameed na kuunda kitengo maalumu cha Daru Rasuulul-Aadham (s.a.w.w) kwa ajili ya kuandika matukuio hayo kielimu”.

Kisha ukafuatia ujumbe wa kamati ya maandalizi ya kongamano hili, ulio wasilishwa na dokta Sarhaan Jafaat, alisema kua: “Bila shaka ushirikiano wa vyuo na Ataba mbalimbali unajenga moyo kwa wanafunzi wa vyuo, Atabatu Abbasiyya tukufu kupitia kiongozi wake mkuu wa kisheria Sayyid Ahmadi Swafi imeweka msisitizo katika kujenga ushirikiano mzuri na wanafunzi wa vyuo, tunaamini uwepo wa jukumu la ulezi wa ubaba katika maeneo haya matukufu, hakika malezi ya kiroho yatazaa matunda mazuri kwa wanafunzi wa vyuo, kwa sababu makuzi ya kiroho kwa mwanadamu hufungamana na makuzi ya kielimu, kitamaduni na kimaadili, hakika vijana wa kiume na wa kike wanapo kua katika malezi ya kuipenda sheria na kufuata utaratibu huwaandaa kua watu wema kama walivyo kua wanafunzi wa zamani”.

Mwisho wa kongamano hili yakasomwa mashairi na kaswida zilizo onyesha mapenzi kwa Mtume na watu wa nyumbani kwake (a.s), kisha zikatolewa zawadi kwa wanafunzi waliovaa majoho ya kiislamu, na mwisho kabisa wale walio changia kufanikisha kwa kongamano hili wakapewa vyeti vya ushiriki.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: