Kufungua milango ya ushirikiano na kufanya kazi pamoja: Ujumbe kutoka kituo cha turathi za Karbala watembelea taasisi ya Kaashiful-Ghitwaa…

Maoni katika picha
Ujumbe kutoka kituo cha turathi za Karbala chini ya kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinadamu katika Atabatu Abbasiyya tukufu, wajadiliana na taasisi ya Kaashiful-Ghitwaa namna ya kushirikiana na kufanya kazi kwa pamoja katika sekta ya turathi pamoja na mambo mengine.

Ujumbe huo uliongozwa na mkuu wa kituo cha turathi za Karbala dokta Ihsaan Gharifi na walikuna na naibu katibu mkuu wa taasisi hiyo Shekh Ahmadi Kaashiful-Ghitwaa na wakabadilishana mawazo, walianza kwa kutoa utambulisho wa kituo na harakazi zake pamoja na pendekezo la kufungua mlango wa kusaidiana na kufanya kwazi kwa kushirikiana katika kila jambo linalo husiana na turathi za mji wa Karbala.

Ujumbe huo ulipata fursa ya kutembelea korido za taasisi na vitengo vyake mbalimbali na kusikiliza maelezo kwa ufupi kuhusu kila kitengo na kazi inayo fanywa na taasisi ya kukusanya na kuhifadhi turathi na nakala kale.

Mwishoni mwa ziara ujumbe ulitoa pongezi kwa kazi zinazo fanywa na taasisi hii za kielimu na kitamaduni, naye Shekhe Ahmadi Kaashiful-Ghitaa alisifu juhudi nzuri inayo fanywa na kituo cha turathi za Karbala ya kuhifadhi turathi za Ahlulbait (a.s) na kuzitunza kwa ajili ya vizazi vijavyo, na akaonyesha utayali wake wakusaidiana na kufanya kazi kwa kushirikiana na kituo hicho.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: