Kitengo cha uangalizi wa kihandisi katika Atabatu Abbasiyya tukufu chakamilisha matengenezo ya barabara ya nyuma ya jengo la Alqami kwa ajili ya mazuwaru…

Maoni katika picha
Mafundi wa kitengo cha uangalizi wa kihandisi katika Atabatu Abbasiyya tukufu wamekamilisha hatua mbili za utengenezaji wa barabara ya (Akdi bani Tamim) iliyopo nyuma ya jengo la Alqami kwa ajili ya mazuwaru katika eneo ya (Fariha), hatua ya uwekaji wa mchanga na kokoto, kutokana na maelekezo ya kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya tukufu Sayyid Ahmadi Swafi.

Mradi huu unatekelezwa baada ya kuondoa vizuizi vilivyo kua katika barabara hiyo na kuisawazisha, kisha watalamu wa ujenzi wameweka mchanga wenye ujazo wa senti mita (60) katika eneo leto la barabara, lenye urefu wa mita (500) na upana wa mita (7), kisha wakaweka kokoto iliyo changanywa na lami kwa ujazo wa sinti mita (15) pamoja na kumwagilia maji, kitengo cha uangalizi wa miradi ya kihandisi kimetumia mabomba ya maji kumwagilia pembezoni mwa barabara pia.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: