Mbele ya malalo ya burudisho la macho yake Abulfadhil Abbasi (a.s) tunaombeleza kifo chake

Maoni katika picha
Mawakibu za kuomboleza zimeanza kuingia katika malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) mapema asubuhi ya leo Jumamosi (13 Jamadal-Aakhar 2020m) sawa na (8 Februari 2020m), kutoka ndani na nje ya mkoa wa Karbala, kwa ajili ya kumpa pole kwa kufiwa na mama yake mtakatifu, mama wa uaminifu na kujitolea Ummul-Banina (a.s), hakika yeye ndio muhusika mkuu wa msiba huu.

Mawakibu zimezowea kufanya hivyo katika kuomboleza msiba huu, kwa mujibu wa maelezo ya rais wa maadhimisho na mawakibu Husseiniyya katika Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya bwana Riyadhi Niímah Salmaan, ambae ameongea na mtandao wa Alkafeel kuhusu mawakibu hizo: “Mawakibu za kuomboleza kifo cha Ummul-Banina (a.s) zilianza kuwasili kabla ya siku mbili na zinaendelea kuwasili, kilele chake hua ni siku ya mwezi kumi na tatu, siku hiyo malalo ya Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s) hujaa mawakibu za kuomboleza kutoka ndani na nje ya mkoa wa Karbala”.

Akaongeza kua: “Hiyo ndio desturi ya uombolezaji iliyozoweleka tangu zamani, watumishi wa kitengo chetu huratibu matembezi yao, mawakibu huingia kupitia mlango wa Kibla katika malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s), baada ya kumpa pole huelekea katika malalo ya Abu Abdillahi Hussein (a.s), wakipitia katika uwanja wa katikati na haram mbili tukufu, huku kundi kubwa la mazuwaru likishiriki kwenye matembezi hayo”.

Kumbuka kua matembezi ya mawakibu hizo huanzia barabara ya Kibla ya haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s), kisha hufanya majlisi mbele ya kaburi la Abulfadhil Abbasi (a.s) na hujikumbusha msimamo wake (Ummul-Banina) katika siku ya Ashura, kabla yake na baada yake, huku wakisema: Mwenyezi Mungu ayakuze malipo yako ewe mwenye msiba ewe Abulfadhil Abbasi (a.s), halafu mawakibu huelekea katika haram ya Imamu Hussein (a.s) kumpa pole mbele ya kaburi lake takatifu wakipitia katika uwanja wa katikati ya haram mbili tukufu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: