Ukarabati wa vifaa kale katika makumbusho ya Alkafeel

Maoni katika picha
Kikosi cha watalamu wa nakala na vifaa kale katika makumbusho ya Alkafeel chini ya Atabatu Abbasiyya, kina uzowefu mkubwa katika fani ya makumbusho na vifaa kale, kikosi hicho hufanya marekebisho ya vifaa kale, na kutoa fursa ya kushuhudiwa vifaa hivyo na mazuwaru watukufu, sambamba na kuweka mabango yenye picha za vifaa kale katika barabara ya Swahibu Zamaan (a.f), kazi hiyo inahitaji ujuzi maalum.

Mtalam wa michoro Ustadh Kamali Basha amesema kua: “Kuna mambo matatu ya msingi katika jambo hili, nayo ni ukarabati, upakaji rangi na uchoraji”.

Akaongeza kua: “Makumbusho ya Alkafeel inamabango mengi ya picha za turathi yaliyo tolewa zawadi katika haram, kwa nafasi yangu hubaini umri wa bango kisha hulifanyia marekebisho kwa kutumia njia mbalimbali, na baada ya kukamilika huliweka katika maonyesho ya makumbusho”.

Akasema: “Sehemu ya pili hua napokea kopi ya nakala kale na mimi huzifanyia marekebisho, kulingana na kitu husika pamoja na kubainisha alama za asili katika kitu hicho, kisha huwekwa kwenye maonyesho”.

Akaendelea kusema: “Jambo la mwisho hua ni kuandaa mabango ya picha za zamani za mji mtukufu wa Karbala na eneo la katikati ya haram mbili sambamba na mabango mengine”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: