Toleo jipya la jarida la (Turathi za Karbala)

Maoni katika picha
Hivi karibuni kituo cha turathi za Karbala chini ya kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu katika Atabatu Abbasiyya tukufu kimetoa awamu ya tatu (21) katika jarida la sita la (Turathi za Karbala) linalo andika turathi za Karbala kwa kibali cha wizara ya elimu ya juu na tafiti za kielimu.

Jarida hilo limejaa tafiti na hakiki za masomo mbalimbali, zinazo saidia kuhuisha turathi za wanachuoni wetu watukufu wa Karbala, ikiwa kama sehemu ya kuwaenzi kwa kuwatendea wema, hili ni jambo dogo sana kwao ukilinganisha na kazi walizo fanya.

Katika jarida hilo kuna mambo yafuatayo:

  • - Dalili za kiswarafu katika kitabu cha Tibiyani cha tafsiri ya Gharibul-Quráni cha Shaharistani (aliyekufa 1344h).
  • - Dalili za dhwawahiru na namna ya kuzifanyia kazi kwa mwenye uhakika.
  • - Dalili ya nafasi za mashairi ya Shekh Muhsin Abi Hubbi Alkabiir (Karbala na mifano yake).
  • - Sayyid Muhammad bun Maásuum Musawi Qatwifi (aliyekufa 1269h) na faharasi ya vitabu vyake vya lugha.
  • - Turathi za Karbala katika jarida la turathi mpya za kishia, chini ya utafiti wa jiolojia.
  • - Dalili za hoja kuhusu habari za Aahaadi kwa mujibu wa Abduswamadu Hamadani Alhaairiy (aliyekufa 1216h).

Pamoja na utafiti ulioandikwa kwa lunga ya kiengereza:

(The Frequency of Lexical Collocation and Grammatical Collocation Patterns in the Extracts of AL- Shehristani).
kumbuka kua jarida la (Turathi za Karbala) ni moja ya majarida yanayotolewa na vituo vya Atabatu Abbasiyya tukufu, linakubalika na wizara ya elimu ya juu na utafiti wa kielimu, linakibali cha Darul-Kutubi wal-wathaaiq Iraaqiyya limesajiliwa kimataifa kwa namba (5489-2312 ISSN).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: