Kamati ya maelekezo na msada imetembelea kituo cha kitamaduni cha maelekezo na maendeleo katika mkoa wa Nainawa/ wilaya ya Sanjaar.

Maoni katika picha
Kamati ya maelekezo na msaada chini ya kitengo cha Dini katika Atabatu Abbasiyya, imetembelea vituo vilivyopo katika mji wa Mosul kusaidia Hashdi Shaábi kweye kambi za opresheni ya Mosul, kituo cha kitamaduni cha kuelekeza na kusaidia katika Mkoa wa Nainawa/ Wilaya ya Sanjaar kilianzishwa mwaka (2018m) na Atabatu Abbasiyya tukufu.

Ziara hii imefanywa kwa ajili ya kuangalia harakati muhimu zinazo fanywa na kituo cha utamaduni maarifa na maendeleo, na kazi wanazo fanya katika mji wenye idadi kubwa ya wafuasi wa Ahlulbait (a.s), na kuangalia hali yao baada ya matatizo na mitihani iliyo ikumba Iraq mwaka wa 2014m, ambapo mji huo na mingine ilipata mtihani mkubwa baada ya kutekwa na magaidi wa Daesh.

Ugeni umepokelewa na mkuu wa kituo Mheshimiwa Sayyid Aáraji pamoja na jopo la viongozi wa mji huo, wamewasilisha salamu za kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi alizo watumia watu wa Sanjaar, akawasifu wasimamizi wa kituo kwa kuitumikia madhehebu ya Ahlulbait (a.s), na akawahimiza waendelee kufundisha akhlaq na mwenendo wa Imamu Hussein (a.s) katika mji huo uliopo mpakani mwa Iraq na Sirya, upande wa Magharibi ya mkoa wa Nainawa, asilimia kubwa ya wakazi wa mji huu ni Aizidiyya na Wakristo, pamoja na wafuasi wa Ahlulbait (a.s) wachache.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: