Maahadi ya Quráni inafanya semina ya usomaji (Maqamaat) za kiiraq.

Maoni katika picha
Maahadi ya Quráni tukufu/ tawi la Najafu inaendesha semina ya usomaji wa Quráni kwa mahadhi ya kiiraq, ambayo huchukuliwa kua ni njia nzuri ya usomaji wa Quráni hapa Iraq, pia ni sehemu ya kuendeleza harakati zake katika fani za Quráni.

Semina hii ni sehemu ya mkakati wa mwaka 2020m, wakufunzi wa semina ni walimu waliobobea katika sauti na mahadhi (maqamaat), mabingwa wa usomaji wa kiiraq, wanauwezo mkubwa wa kumfikisha mwanafunzi katika hali ya juu ya usomaji wa Quráni, kama vile msomaji na haafidh Khaliil Ismaili na Walidi Faluji na wengine miongoni mwa wasomaji wakubwa.

Tambua kua Maahadi ya Quráni tukufu inaendeleza harakati za kufundisha kitabu kitakatifu cha Mwenyezi Mungu na mafundisho ya kizaki kitakaswa, vitu ambavyo tumeusiwa na Mtume Muhammad (s.a.w.w) tushikamane navyo ili tusipotee.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: