Zaidi ya sahani za chakula (7000) hugawiwa kila siku ya Alkhamisi na usiku wa Ijumaa.

Maoni katika picha
Mgahawa (mudhifu) wa Atabatu Abbasiyya hutoa huduma ya chakula kwa mazuwaru kila siku, idadi ya mazuwaru huongezeka kila siku ya Alkhamisi na usiku wa Ijumaa katika kila wiki, Karbala hushuhudia ongezeko kubwa la mazuwaru, maandalizi ya kuwapokea huanza mapema.

Watumishi wa kitengo cha mgahawa Alkhamisi ya kila wiki huandaa maelfu ya sahani za chakula, huandaa zaidi ya sahani (7000) za chakula pamoja na vinyaji na matunda na hugawa kupitia madirisha ya nje ya haram tukufu, mazuwaru husimama kwenye mstari kwa ajili ya kuchukua chakula, hua kuna mstari wa wanaume na mstari wa wanawake.

Chakula hugawiwa kwa kufuata muda, muda wa kwanza huwa ni chakula cha mchana ambacho hutolewa baada ya Dhuhuraini, hutolewa chakula hicho sambamba na huduma zinazo tolewa ndani ya ukumbi wa mgahawa kwa mazuwaru waliopata koponi za kuingia ndani ya ukumbi huo.

Wakati wa jioni hutolewa juisi, matunda na vitafunwa.

Baada ya swala ya Magharibaini hufunguliwa madirisha ya nje kwa mara nyingine kwa ajili ya kugawa chakula cha usiku kwa mazuwaru.

Tambua kua watumishi wa kitengo cha mgahawa katika Atabatu Abbasiyya wanafanya kazi kila siku ya kugawa chakula kwa mazuwaru wa mwezi wa bani Hashim (a.s) wanaokuja kutoka miji tofauti na mataifa mbalimbali.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: