Atabatu Abbasiyya inachukua tahadhari ya kujilinda na virusi vya Korona

Maoni katika picha
Atabatu Abbasiyya tukufu imechukua tahadhari kadhaa kwa ajili ya kujilinda na virusi vya (Korona) kwa wafanyakazi wa Ataba na mazuwaru.

Kwa mujibu wa maelezo ya kiongozi wa idara ya madaktari katika Ataba tukufu Dokta Usama Abdulhassan Kaadhim: “Kutokana na kuwepo kwa maambukizi ya virusi vya Korona katika nchi mbalimbali duniani hususan nchi jirani, kwa usalama wa mazuwaru na wafanyakazi tumechukua tahadhari kadhaa za kiafya na kimatibabu kwa ajili ya kujilinda na virusi hivyo kama vikitokea hapa Iraq –Allah atuepushie- ikiwa ni sehemu ya kufanyia kazi kauli isemayo (kinga ni bora kuliko tiba)”.

Akabainisha kua: “Miongoni mwa hatua hizo ni kuimarisha huduma za afya hasa kwa wale wanaofanya kazi moja kwa moja na mazuwaru, kama vile kitengo cha mgahawa, utumishi, mahusiano na ukaguzi sambamba na kuchukua ripoti kila simu katika maeneo hayo”.

Akaongeza kua: “Kazi haijaishia hapo bali kuna mambo mengine yatafanyika kulingana na mahitaji, ikiwa ni pamoja na kutoa maelekezo hukusu maradhi hayo”.

Kumbuka kua Marjaa Dini mkuu alitoa wito wa kujikinda na virusi vya Korona katika khutuba ya Ijumaa iliyopita.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: