Mwezi mosi Rajabu alizaliwa Baaqirul-Uluumu Almuhammadiyya taa liangazalo.

Maoni katika picha
Siku ya kwanza ya mwezi wa Rajabu ni siku ya kukumbuka kuzaliwa kwa Imamu wa tano Muhammad bun Ali Albaaqir (a.s), Baaqirul-Uluumul-Awwalina wal-Aakhirina, aliyezaliwa mwaka wa (57h), watu wa nyumba ya Mtume walimpokea kwa shangwe na furaha kubwa kwani walikua wanasubiri kwa ham kuzaliwa kwake kulikobashiriwa na Mtume (s.a.w.w), Imamu anayetokana na kizazi kitakasifu kikamilifu.

Imamu Muhammad Baaqir (a.s) ni Imamu wa kwanza maasum aliyetokana na kizazi cha maimamu wawili watakasifu ambao ni Imamu Ali Zainul-Aabidina bun Imamu Hussein bun Ali bun Abu Twalib (a.s) hiyo ndio nasaba yake upande wa baba.

Mama yake ni bibi Fatuma mtoto wa Imamu Hassan bun Ali bun Abu Twalib (a.s), jina lake la kunia anaitwa (Ummu Abdillahi), alikua ni mwanamke mtukufu wa bani Hashim, Imamu Zainul-Aabidina (a.s) alikua anamwita Swidiiqah, Imamu Swaqiq (a.s) anasema: (Kulikua hakuna mwanamke bora kama yeye katika watoto wa Hassan), yatosha fahari kwake kua ametokana na wajukuu wawili wa Mtume (s.a.w.w), na amekulia katika nyumba ambayo Mwenyezi Mungu ameamrisha zitukuzwe na litajwe jina lake, miguu yake mitakatifu ndio iliyomlea Imamu Baaqir (a.s).

Kuniya yake: (Abu Jafari) hana kuniya nyingine zaidi ya hiyo.. laqabu zake (majina ya sifa) ni: (Al-Aminu, Ashabiha –alikua anafanana sana na Mtume (s.a.w.w)-, Shaakiru, Haadi, Swaabir, Shaahid, Baaqir –hiyo ndio laqabu mashuhuri zaidi-) yeye na mwanae Swadiq pia huitwa kwa laqabu ya (Baaqiraini) na (Swaadiqaini).

Imamu Baaqir (a.s) aliishi na babu yake Imamu Hussein (a.s) miaka mitatu na nusu na alishuhudia vita ya Karbala, na ameishi na baba yake miaka thelathini na nane, kipindi chote alijifunza utukufu kutoka kwa baba yake, kipindi cha uimamu wake kilikaribia miaka ishirini.

Imamu Baaqir (a.s) alichota elimu na maarifa kutoka kwa baba yake Imamu Zainul-Aabidina (a.s) hadi akawa bingwa wa fani zote, alikua sawa na alivyotajwa na babu yake Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w) alipo mpa jina la Baaqir, alisema: (Hakika atapata elimu kwa haraka), Imamu alijulikana kwa maneno mazuri, hoja madhubuti za fiqhi, aqida na hukufu za kisheria, maisha yake yote aliishi katika mji wa Madina, akisimamia shughuli za waja wema na kuendeleza mafundisho ya Mtume (s.a.w.w), alilelewa na Imamu Ali kisha akalelewa na maimamu wawili watakasifu, Imamu Hassan na Hussein (a.s), halafu akalelewa na baba yake Ali bun Hussein (a.s) aliye mfundisha matukufu yote.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: