Alasiri ya Jumanne (25 Februari 2020m) vimehitimishwa vikao vya uwasilishaji wa mada za kitafiti katika kongamano la Imamu Baaqir (a.s) awamu ya sita, lililofanywa chini ya kauli mbiu isemayo: (Imamu Baaqir –a.s- ni muendelezaji wa mafundisho ya utume na hazina ya uimamu).
Kulikua na jumla ya mada tatu, ya kwanza imetolewa na mkufunzi wa chuo kikuu Karbala Dokta Karimah Numasi Madani, mada yake ilihusu: (Hutuba za Imamu Baaqir (a.s).. baina ya muundo na athari zake na kisomo katika udhu na ufasaha), akafafanua neno la (Balagha Jamhuri) ambayo huchukuliwa kama hadithi ya kuingia katika uwanja wa kiarabu, akaingiza baadhi ya kauli na khutuba za Imamu Baaqir (a.s) kuhusu msamiati wa Balagha Jamhuri, kuonyesha kua kauli zake na za maimamu wengine (a.s) ni ujumbe endelevu kwa umma, kulikua na watu maalum wanasikiliza kauli zao na kuzifanyia kazi.
Mada ya pili ilitolewa na Dokta Daudi Salmani Khalfu Zubaidi chini ya anuani isemayo: (Upokezi wa Imamu Baaqir (a.s) katika kitabu cha Faraja baada ya dhiki – cha Qadhi Tanukhi), mtoa mada alifafanua riwaya kadhaa za Imamu Baaqir (a.s), aidha akahimiza kushikamana na Quráni tukufu pamoja na Mtume Muhammad (s.a.w.w) na watu wa nyumbani kwake watakatifu (a.s), akataja dua zilizo pokewa kutoka kwao.
Mada ya mwisho ikatolewa na Ustadh Muhammad Hussein Abudi kutoka chuo kikuu cha Karbala, ilikua inasema: (Mafuhumu na mahusiano ya kijamii katika fikra za Imamu Baaqir –a.s-), akaeleza mafuhumu mbili, kwanza mafuhumu ya mahusiano katika mtazamo wa sheria na sunna za Mtume Muhammad (s.a.w.w) na Ahlubaiti wake watukufu (a.s), akafafanua baadhi ya aya za Quráni na hadithi zinazo eleza umuhimu wa jambo hilo, pili akazungumza kuhusu mafuhumu ya uhusiano wa kijamii katika fikra ya Imamu Baaqir (a.s), hapo akaangazia hadithi na riwaya za Imamu kuhusu umuhimu wa mtu na nafsi yake, mtu na familia yake, na mtu na jamii.