Siku ya Jumanne jioni (25 Februari 2020m) ndani ya haram tukufu ya Abbasi kilifanyika kikao cha usomaji wa Quráni ambacho ni miongoni mwa vipengele vya kongamano la Imamu Baaqir (a.s) la awamu ya sita, kwa ushiriki wa jopo la wasomaji wa Atabatu Abbasiyya na kuhudhuriwa na mazuwaru.
Kikao kilifunguliwa kwa Quráni iliyo somwa na Ammaar Hiliy, akafuatia Faisal Matwar na mwisho akasoma Muhammad Ridhwa Salmani.
Tumeongea na mjumbe wa kamati ya maandalizi ya kongamano la Imamu Baaqir (a.s), ambae ni makamo rais wa kitengo cha habari na utamaduni katika Atabatu Abbasiyya Ustadh Aqiil Abdulhussein Yaasiri kuhusu kikao hicho, amesema kua: “Tunamshukuru Mwenyezi Mungu mtukufu kwa kufanya kikao cha usomaji wa Quráni ambacho wasomaji wetu wa Ataba wameshiriki, kikao hiki ni sehemu ya maelekezo ya kamati ya Quráni katika Atabatu Abbasiyya tukufu, inayo lenga kueneza utamaduni wa kufuata mafundisho ya Quráni kwa kutumia nafasi ya kusoma Quráni kwenye makongamano na mahafali”.
Akaongeza kua: “Kongamano lijalo (Insha-Allah) tunatarajia kuwa na washiriki wengi zaidi kutoka ndani na nje ya Iraq”.
Kumbuka kua kongamano la Imamu Baaqir (a.s) la awamu ya sita, chini ya usimamizi wa uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya limefanywa siku ya Jumanne (25 Februari 2020m) chini ya kauli mbiu isemayo: (Imamu Baaqir –a.s- ni muendelezaji wa mafundisho ya utume na hazina ya uimamu).