Umoja wa mataifa umeingiza miradi ya maktaba na Daru Makhtutwaat katika ramani ya kimataifa

Maoni katika picha
Umoja wa mataifa umeingiza miradi ya maktaba na Daru Makhtutwaat ya Atabatu Abbasiyya tukufu katika ramani ya kimataifa, pamoja na nchi zinazo saidia kutekeleza malengo ya maendeleo endelevu ya mwaka 2015m, yaliyo sainiwa na nchi (96) duniani ikiwepo Iraq.

Mkuu wa kituo cha faharasi na kupangilia maalumaat Ustadh Hasanain Mussawi ameuambia mtandao wa Alkafeel kua: “Tumepokea ujumbe kutoka umoja wa mataifa kupitia barua pepe, ukituambia tuingize miradi yetu yenye malengo ya maendeleo endelevu ya mwaka (2020 / 2030m) katika ramani ya kimataifa.

Akaongeza kua: “Tukapewa na ufungua (neno la siri) la kuingia kwenye mtandao wao, tumeingiza miradi mitano ya maktaba na Daru Makhtutwaat ya Atabatu Abbasiyya tukufu, ambayo ni:

  • 1- Mpangango kazi wa kuhifadhi turathi za Iraq kwa namba ulio andaliwa katika maktaba ya taifa.
  • 2- Nadwa maalum kuhusu maktaba na tiba iliyo fanywa katika chuo kikuu cha Al-Ameed chini ya Atabatu Abbasiyya.
  • 3- Nadwa maalum ya kutekeleza malengo ya maendeleo endelevu ya maktaba za Iraq iliyo fanywa ndani ya Atabatu Abbasiyya.
  • 4- Nadwa ya namna ya kuhifadhi maoni na barua za vyuo vikuu katika kutekeleza malengo ya maendeleo endelevu, ilifanywa kwa kushirikiana na chuo kikuu cha Mosul.
  • 5- Nadwa za hatua ya kwanza na ya pili katika chuo kikuu cha Mustanswiriyya/ kitivo cha adabu/ kitengo cha maktaba na maalumaat katika utekelezaji wa malengo ya maendeleo endelevu katika usomaji bora.

Miradi yote ilihudhuriwa na wawakilishi kutoka wizara ya mipango ya Iraq na muwakilishi rasmi kutoka umoja wa mataifa nchini Iraq, pamoja na rais wa umoja wa maktaba za kiarabu.

Tambua kua umoja wa mataifa uliweka misingi ya maendeleo endelevu kumi na saba, yenye malengo 64 yanayo takiwa kutekelezwa na maktaba, kwani umoja wa mataifa unazingatia kua ni sehemu muhimu inayo onganisha jamii na taifa.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: