Kitengo cha miradi katika Atabatu Abbasiyya tukufu kimetangaza kudhibiti maji ya ardhini katika mradi wa Saaqi

Maoni katika picha
Watumishi wa kitengo cha miradi ya kihandisi katika Atabatu Abbasiyya tukufu, wametangaza kudhibiti kiwango kikubwa cha maji ya ardhini na kuyahifadhi, kwa kutumia njia za kisasa.

Rais wa kitengo cha miradi ya kihandisi Mhandisi Dhiyaau Swaaigh ameuambia mtandao wa Alkafeel kua: “Mradi wa Saaqi unategemea visima (52) vinavyo lisha maji kwenye mradi huo”.

Akaongeza kua: “Kudhibiti maji ya visima kunategemea hatua kadhaa zinazo tuwezesha kutambua uwepo wa maji na kiwango chake, kwa ajili ya kulinda rasilimali hiyo tukufu katika kilimo”.

Akafafanua kua: “Kitengo cha miradi ya kihandisi chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu huchunguza kiwango cha maji sehemu ya kuchimba kisima, kwa kushirikiana na idara ya visima ya mkoa wa Karbala ambayo inamamlaka ya kuangalia kiwango cha maji ya aridhini na maji ya mvua na kuangalia tofauti iliyopo katika rasilimali hizo muhimu”.

Akaendelea kusema: “Tumepata mafanikio makubwa ya kutunza maji na kuyatumia kwa matumizi chanya”.

Mradi wa Saaqi wa kilimo unatekelezwa magharibi ya mkoa wa Karbala ni miongoni mwa miradi mikubwa inayo simamiwa na kitengo cha miradi ya kihandisi katika Atabatu Abbasiyya tukufu, mradi huo unategemea maji ya visima.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: