Kitengo cha Maqaam ya Imamu Mahadi (a.f) ni utowaji endelevu wa neema za mwenye ukarimu

Maoni katika picha
Watumishi wa kitengo cha Maqaam ya Imamu Mahadi (a.f) chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu wanaendelea kuboresha mazingira ya mazuwaru, kwa kudumisha usafi katika Maqaam pamoja na mazingira yanayo izunguka, likiwemo soko la Imamu Swadiq (a.s).

Rais wa kitengo cha Imamu Mahadi (a.f) Adnani Ni’mah Dhaifu, ameuambia mtandao wa Alkafeel kuhusu kazi zao, amesema kua: “Miongoni mwa vipaombele vya kazi yetu ni kuboresha mazingira ya mazuwaru wanaokuja katika Maqaam ya Imamu Mahadi (a.f), na kudumisha usafi kwa kuosha mazulia, na sehemu zote za Maqaam pamoja na kupuliza manukato”.

Akaongeza kua: “Hali kadhalika huwa tunasafisha mto kila baada ya muda fulani kwa kushirikiana na idara ya mito ya Karbala, pamoja na kusafisha daraja maalum la mto wa Husseiniyya, sehemu inayo pendwa sana na mazuwaru watukufu, kwa sababu maji ya sehemu hiyo yanahusiana na mnyweshaji wenye kiu Karbala (Saaqi Atwasha Karbala) Abulfadhil Abbasi (a.s).

Akaendelea kusema kua: “Miongoni mwa huduma tunazotoa kwa wakazi wa eneo hilo ni kusafisha soko la Imamu Swadiq (a.s) kila siku asubuhi na jioni, kwa kutumia gari maalum la usafi, huwa tunashirikiana na wafanya biashara wa soko hilo”.

Akamaliza kwa kusema: “Miongoni mwa baraka za mwezi wa bani Hashim (a.s) tumefanikiwa kuweka maji safi ya kunywa sokoni na katika shule zilizo karibu na Maqaam tukufu kwa kutumia gari maalum la kusambaza maji”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: