Mwezi kumi Rajabu.. kuzaliwa mwezi wa tisa miongoni mwa maimamu wa Ahlulbait Imamu Muhammad Aljawaad (a.s).

Maoni katika picha
Mwezi kumi Rajabu wa kila mwaka, wafuasi wa Ahlulbait (a.s) hufanya kumbukumbu ya kuzaliwa kwa nuru ya tisa miongoni mwa nuru za Uimamu, ambae ni Imamu Muhammad Aljawaad (a.s) aliyezaliwa mwaka wa (195h).

Imamu Aljawaad ni Muhammad bun Ali bun Mussa bun Jafari bun Muhammad bun Ali bun Hussein bun Ali bun Abu Twalib (a.s). Mama yake ni bibi Sakina Marsiyya na inasemekana ni Khaizarani, na mke wake ni bibi Sumana kutoka Moroko, Imamu alikua kimbilio la wafuasi wake kwa upole na ukarim.

Kuhusu kuzaliwa kwake bibi Hakima mtoto wa Abu Hassan Mussa bun Jafari (a.s) anasimulia karama zilizo tokea, anasema: wakati alipo pata uchungu mama Abu Jafari (a.s), Imamu Ridhwa (a.s) aliniita akasema: (Ewe Hakima hudhuria kujifungua kwake) akaniingiza ndani (a.s) na akatuwashia taa na kutufungia mlango, alipo karibia kujifungua taa likazimika, alikua ameshika chombo, mimi nikashughulika na kuwasha taa, ghafla Abu Jafari (a.s) akazaliwa akiwa na kitu laini kimemfunika mwili wake kama nguo na kinatoa mwanga mkali ulio angazia nyumba yote.

Imamu Muhammad Aljawaad (a.s) alikulia katika nyumba ya Utume na Uimamu, nyumba aliyo itukuza Mwenyezi Mungu kwa waislamu, alipata mafundisho bora kutoka kwa baba yake Imamu Ridhwa (a.s) ambaye yeye mwenyewe alisimamia malezi hayo, alikua anafatana naye nyumbani na safarini hadi alipo kua mkubwa (a.s), alipata elimu kubwa kutoka kwa baba yake hadi akaweza kufundisha wanachuoni wakubwa namna ya kufundisha sharia za kiislamu, na akawahimiza kuandika na kutunza anayo wafundisha na yaliyo fundishwa na wazazi wake walio tangulia.

Miongoni mwa laqabu zake (a.s) ni: (Aljawaad, Attaqiyyu, Azzakiyyu, Alqaanii, Almurtadhwa, Almuntajabu) na mashuhuri zaidi ni: (Aljawaad) kutokana na wingi wa kutoa kwake na ukarimu, pia huitwa (Baabu Muraad) baada ya kufa kwake, kutokana na wingi wa kukidhiwa haja za watu kwenye kaburi lake, aliishi miaka (25) na kipindi cha Uimamu wake kilikua miaka (17).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: