Hivi ndio walivyo aga watumishi wa Kaafil malalo ya Aqilah Hashimiyyiin (a.s)

Maoni katika picha
Baada ya safari iliyodumu zaidi ya siku tano na iliyokua na vitu vingi, ikiwa ni pamoja na kufunga paa la taji la dirisha la malalo ya bibi Zainabu (a.s) katika mji mkuu wa Sirya Damaskas, lililo tengenezwa na kitengo cha kutengeneza madirisha na milango ya makaburi matukufu chini ya Atabatu Abbasiyya, leo watumishi wa Abulfadhil Abbasi (a.s) wamehitimisha safari yao katika malalo ya Aqiilah bani Hashim bibi Zainabu (a.s).

Hitimisho la safari hiyo limefanywa kwa kuweka majlisi ndani ya haram tukufu karibu na dirisha lake takatifu, majlisi ilikua na vipengele vingi na imefanywa katika usiku mtukufu wa Ijumaa.

Majlisi hiyo ilihudhuriwa na wageni kutoka Atabatu Abbasiyya pamoja na mazuwaru na watumishi wa malalo ya bibi Zainabu (a.s), ilifunguliwa kwa kusoma dua Kumail (r.a) iliyo pokewa kutoka kwa Imamu Ali (a.s), iliyo somwa na makamu rais wa kitengo cha Dini katika Atabatu Abbasiyya Shekh Aadil Wakiil, akafuata bwana Ahmadi Bawi aliyehamisha hisia za wahudhuriaji na kuwawapeleka Karbala tukufu katika kaburi la Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s) kwa kusoma Ziaratu-Ashuraa, na mwisho ikasomwa kaswida ya huzuni na Sayyid Bahaau Mussawi.

Baada ya hapo watu wote wakasimama na kumuomba Mwenyezi Mungu kwa utukufu wa ambaye wamesimama karibu yake, awape amani na utulivu waislamu wa mashariki na magharibi (dunia nzima) na awalinde na kila aina ya balaa.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: