Katika ziara yake kwenye shirika la Khairul-Juud.. Sayyid Swafi: Lazima kufanyia kazi maelekezo ya kidaktari na kulinda ubora wa bidhaa pamoja na kuzuwia ongezeko la bei

Maoni katika picha
Kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya tukufu Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi ametembelea shirika la Khairul-Juud, kuangalia utendaji wa kazi na bidhaa mpya zinazo zalishwa za kinga (maski) na visafishio.

Katika ziara hiyo amefuatana na mkuu wa idara ya afya katika mkoa wa Karbala Dokta Swabahu Husseini na naibu katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya pamoja na wajumbe wa kamati kuu ya uongozi na baadhi ya marais wa vitengo.

Rais wa kitengo cha habari katika Atabatu Abbasiyya Dokta Mushtaqu Muan ameuambia mtandao wa Alkafeel kua: “Ziara hii ni sehemu ya ziara nyingi ambazo hufanywa na Mheshimiwa kiongozi mkuu wa Kisheria katika Atabatu Abbasiyya kwa ajili ya kuangalia huduma za kijamii na viwanda vilivyo chini ya Atabatu Abbasiyya, amesisitiza mambo mengi kuhusu ulazima wa kujilinda na virusi vya Korona katika ziara hii, miongoni mwa aliyo sisitiza ni:

Kwanza: ulazima wa kufuata maelekezo yanayo tolewa na taasisi za afya, hususan maelekezo yanayo tolewa na taasisi za afya za kimataifa.

Pili: kutafsiri maelekezo hayo na kuyatumia katika kuboresha utengenezaji wa vifaa vya kujikinga (maski) na visafishio ili kupambana na kusambaa kwa virusi vya Korona.

Tatu: kuongoza uzalishaji wa vifaa hivyo kwa ajili ya kukidhi mahitaji ya watumiaji, sambamba na kudhibiti ongezeko la bei, tofauti na wale wanaotumia tatizo hili kama fursa ya kupandisha bei bidhaa zao, akasema kua hiyo sio sifa ya wairaq wanaojulikana kwa ukarimu na ubinaadamu pamoja na kusaidiana wakati wa shida, inatakiwa wairaq wote tuungane katika mapambano haya hususan kuzisaidia familia zenye kipato kidogo.

Nne: mapambano ya tatizo hili (virusi vya Korona) yanatakiwa yafanywe kwa umakini na tahadhari kubwa, haifai kutumia vitisho na kujenga hofu, bali inatakiwa kufanyia kazi kauli isemayo (kinga ni bora kuliko tiba).

Dokta Swabahu Husseini akasema kua: “Shirika la Khairul-Juud linatengeneza bidhaa mbalimbali za visafishio na maski zenye ubora mkubwa, sisi kama idara ya afya ya mkoa wa Karbala tuna mawasiliano ya moja kwa moja na taasisi zote zinazo jihusisha na bidhaa zinazo husu afya, bidhaa zote zinazo tengenezwa hukaguliwa ubora wake, na bidhaa za shirika hili zimethibitika kua na ubora mkubwa”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: