Muhimu: Chini ya saa 48 Atabatu Abbasiyya imefanikiwa kusafirisha asilimia kubwa ya majeruhi na maiti za watu waliopata ajali nchini Sirya

Maoni katika picha
Alfajiri ya leo Jumanne ya mwezi (14 Rajabu 1441h) sawa na (10 Machi 2020m) miili ya mazuwaru wa bibi Zainabu (a.s) wa kiiraq, waliokufa kwenye ajali iliyo tokea pembezoni mwa mji wa Damaskas imewasili katika uwanja wa ndege wa Najafu.

Kumbukua kua Mheshimiwa kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya Sayyid Ahmadi Swafi baada ya kupata habari hii ya kuhuzunisha aliunda kamati mara moja itakayo fuatilia hali za majeruhi na kufanya mchakato wa kuwasafirisha pamoja na kugharamia matibabu ya majeruhi wote.

Atabatu Abbasiyya ilitangaza kua asubuhi ya Jumatatu mwezi (13 Rajabu 1441h) sawa na (9 Machi 2020m) majeruhi waliwasiri katika hospitali ya rufaa Alkafeel, jumla ya majeruhi thelathini waliwasiri Iraq kutoka Sirya na kuwagawa kwenye mikoa mitatu (Bagdad, Muthanna na Karbala), kuna wenye majeraha madogo, ya saizi ya kati na makubwa.

Kuna majeruhi wengine wanne madaktari wameshauri waendelee kutibiwa katika hospitali za Sirya, kutoka na hali zao za afya haziruhusu kusafirishwa kwa sasa.

Mchakato wa kuwasafirisha haujachukua zaidi ya saa 48, umefanywa kwa ushirikiano wa ofisi ya waziri mkuu na uongozi wa muungano wa opresheni za kijeshi pamoja na wizara ya ulinzi ambayo ilitoa ndege ya kivita, bila kusahau wizara ya mambo ya nje ya Iraq pamoja na ubalozi wa Iraq nchini Sirya sambamba na serikali ya mkoa wa Karbala na idara ya afya ya mkoa huo, kwa pamoja walikamilisha mahitaji yote ya kidaktari.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: