Kifo cha Aqiilah Ahlulbait wahyi na Utume (a.s)

Maoni katika picha
Wapenzi na wafuasi wa Ahlulbait (a.s) mashariki na magharibi (dunia nzima) katika siku kama ya leo mwezi kumi na tano Rajabu, wanaomboleza kifo cha Aqiilah Twalibina bibi Zainabu Kubra (a.s), ambaye alikufa mwaka wa 62 hijiriyya na inasemekana mwaka wa 65 Hijiriyya, akiwa na umri wa miaka 60, ambayo aliitumia kupigana jihadi katika njia ya Mwenyezi Mungu, kwani alizaliwa mwaka wa tano hijiriyya katika nyumba ya Utume, akaishi chini ya malezi ya babu yake Mtume wa mwisho pamoja na baba yake bwana wa mawasii na mama yake mbora wa wanawake wa ulimwenguni, na ndugu zake Hassanaini wapenzi wa Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w).

Bibi Zainabu aliishi katika mazingira ya Imani ndani ya nyumba ya mama yake pande la nyama ya Mtume mtukufu Fatuma Faharaa (a.s), akakua pamoja na kaka zake mabwana wa vijana wa peponi, akasoma kwa baba yake mlango wa mji wa elimu, alifuzu mafunzo ya nyumba hiyo na alionyesha ujemedari wake, amani iwe juu yake siku aliyozaliwa na siku aliyo kufa na siku atakayo fufuliwa na kua muombezi katika watu wa nyumba ya Mtume (a.s).

Bibi Zainabu (a.s) alikua ni wa pili baada ya mama yake Swidiqah Zaharaa (a.s) katika kufanya ibada, tahajudi na dhikri, alikua mwingi wa kufunga mwingi wa kuswali mwingi wa kusoma dua, sehemu kubwa ya usiku alikua anaswali na kusoma Quráni, hakuacha kufanya hivyo hata katika usiku mgumu zaidi kwake, nao ni usiku wa mwezi kumi na moja Muharam, imepokewa kutoka kwa Fadhili Nainiy Burjudi kua: “Hussein (a.s) alipomuaga dada yake kwa mara ya mwisho alisema: Ewe dada yangu usinisahau katika sunna za usiku”.

Alikua (a.s) anapigiwa mfano katika kujihifadhi, Yahya Mazini anasema: Nilikua jirani na kiongozi wa waumini (a.s) katika mji wa Madina kwa muda mrefu, tena karibu na nyumba aliyokua anaishi binti yake Zainabu, namuapa Mwenyezi Mungu sikuwahi kumuona na kijana wala kusikia sauti yake, alikua anapotaka kwenda kuzuru kaburi la babu yake Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w), anaenda usiku Hassan akiwa kuliani kwake na Hussein kushotoni kwake na kiongozi wa waumini mbele yake, wakikaribia kaburi tukufu anatangulia baba yake kiongozi wa waumini (a.s) na anapunguza mwanga wa taa, Hassan akamuuliza kuhusu jambo hilo, akasema: Naogopa watu wasimuone dada yako Zainabu. Imamu Hussein (a.s) alikua anapotembelewa na Zainabu anasimama kuonyesha heshima kwake, na alikua anamkaribisha kwenye kiti chake.

Bibi Zainabu (a.s) alishuhudia mambo yote yaliyojiri Karbala, alishuhudia kuuwawa kwa watoto wake, ndugu zake miezi ya bani Hashim, lakini aliendelea kufanya subira na kumtegemea Mwenyezi Mungu, nafasi yake ilionekana katika kuwasimamia wanawake na watoto, ushujaa wake ulionekana sehemu nyingi.

Bibi Zainabu (a.s) alifariki mwezi (15 Rajabu) katika mji wa Damaskas Sham, wanahistoria wametofautiana mwaka aliokufa, asilimia kubwa wanasema alikufa mwaka wa (62) hijiriyya, huku wengine wakisema kua alikufa mwaka wa (65) hijiriyya, na alizikwa pembezoni mwa mji wa Damaskas katika kijiji kiitwacho Rawiyah, amejengewa mazaru inayo endana na utukufu wake, kuna kauli dhaifu inayo sema kua alizikwa Misri, katika nchi hiyo pia ana maqaam (sehemu) ambayo watu huenda kuizuru na kutabaruku.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: