Katika huzuni ya kumbukumbu ya kifo chake haram ya mtumishi wake imewekwa mapambo meusi

Maoni katika picha
Haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s) imewekwa mapambo meusi yanayo ashiria huzuni, kwa ajili ya kumbukumbu ya kifo cha Aqilah Twalibina na jabali wa subira mama wa misiba bibi Zainabu binti Ali (a.s), ambaye tarehe ya kifo chake inasadifu Jumatano ya kesho mwezi (15 Rajabu 1441) sawa na (11 Machi 2020m).

Kutokana na tukio hilo tumeandaa ratiba maalum ya maombolezo yenye vipengele vingi, miongoni mwa vipengele hivyo ni:

Kwanza: kufanya mihadhara ya kidini ndani ya haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s) kwa ajili ya kuongea historia ya maisha ya mwanamke huyu mtukufu.

Pili: kujiandaa kupokea mawakibu za waombolezaji zinazo kuja kumpa pole Abulfadhil Abbasi (a.s) kutokana na msiba huu.

Tatu: kuwasha taa nyekundu zinazo ashiria huzuni ndani ya haram tukufu na kupandisha pendera nyeusi zinazo ashiria msiba.

Nne: kufanya majlisi ya kuomboleza ndani ya ukumbi wa utawala katika Atabatu Abbasiyya na kutoa mihadhara wa kidini na mashairi kuhusu utukufu wa bibi Zainabu (a.s).

Tano: kufanya matembezi ya pamoja kati ya wafanyakazi wa Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya kwa ajili ya kumpa pole Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s) yatakayoanzia ndani ya Atabatu Abbasiyya tukufu.

Sita: kuandaa vipindi maalum vya kumzungumzia mama huyu mtakatifu katika redio ya wanawake Alkafeel ambayo ipo chini ya kitengo cha habari na utamaduni cha Atabatu Abbasiyya tukufu.

Saba: kufungua mlango wa kujisajili ziara kwa niaba katika mtandao wa kimataifa Alkafeel kupitia link ifuatayo: https://alkafeel.net/zyara/ kwa lugha zote zilizopo kwenye mtandao huo, ili kuwafanyia ziara kwa niaba watakao jisajili kwenye malalo yake tukufu katika mji mkuu wa Sirya Damaskas.

Kumbuka kua bibi Zainabu (a.s) alikufa na kupumzika matatizo ya duniani mwezi (15 Rajabu 62h), baada ya jina lake kuandikwa kwa nuru katika orodha ya wanawake bora, wapenzi na wafuasi wa Ahlulbait (a.s) hufanya majlisi za kuomboleza kila mwaka katika tarehe ya kifo chake.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: