Opresheni kubwa ya kupulizia dawa maeneo yanayo zunguka Atabatu Abbasiyya na mji mkongwe

Maoni katika picha
Watumishi wa kamati ya kujikinga na majanga iliyo undwa na Atabatu Abbasiyya, wameanza kazi ya kupuliza dawa maeneo yanayozunguka haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s) na barabara zinazo elekea kwenye haram hiyo, pamoja na mji mkongwe, kwa ajili ya kujilinda na virusi vya Korona, ili kuimarisha usalama wa mazuwaru pamoja na kuondoa hatari ya kuambukizwa kwao.

Kiongozi wa idara ya tiba Dokta Osama Abdulhussein ameuambia mtandao wa Alkafeel kua: “Miongoni mwa shughuli za kujikinga zinazofanywa na kamati iliyo undwa na Atabatu Abbasiyya tukufu, pamoja na juhudi kubwa inayofanywa na kitengo cha usimamizi wa kihandisi chini ya usimamizi wa madaktari, tumefanya kazi ya kupuliza dawa maeneo yote yanayozunguka haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s) pamoja na sehemu za kutunzia amana (vitu) vya mazuwaru, sehemu za kuvulia viatu, sehemu za kuhifadhi mabeji, milango pamoja na ukuta wa haram kwa nje”.

Akaongeza kua: “Aidha tumepuliza dawa kwenye barabara zinazoelekea haram pamoja na mji mkongwe, sehemu za biashara, sehemu za kupumzika, sehemu za chakula (migahawa), majengo ya vyoo na sehemu zingine.

Akafafanua kua: “Vifaa vilivyo tumika katika kazi hii vinatengenezwa na shirika la Khairul-Juud na vinauwezo mkubwa wa kuzuwia virusi vya Korona”.

Kiongozi wa idara ya uzalishaji katika kitengo cha usimamizi wa kihandisi bwana Hassan Ali Abdulhussein amesema kua: “Kutokana na kuenea kwa virusi vya Korona kazi ya kupuliza dawa imefanywa chini ya idara ya madaktari, tayali kuna kamati maalum iliyo pewa jukumu hilo, itakayo fanya kazi hiyo mara kwa mara kama itakavyo swauriwa na wataalam wa afya”.

Kumbuka kua Atabatu Abbasiyya imesha chukua hatua nyingi za kujikinga na maambukizi ya virusi vya Korona, na inafanyia kazi maelekezo mbalimbali yanayo tolewa na idara ya afya.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: