Marjaa Dini mkuu amesisitiza kua kuwatibu wagonjwa na kuwahudumia ni wajibu kifaya kwa kila mwenye uwezo wa kufanya hivyo ambao ni madaktari, wauguzi na wengineo, serikali inatakiwa iwape vifaa vyote vinavyo hitajika kwa ajili ya kuwalinda na maambukizi, wala haitakiwi kutoa udhuru katika hilo, atakaejitolea maisha yake kwa ajili ya kumhudumia mgonjwa ataandikiwa thawabu za shahidi.
Hayo yapo kwenye jibu la Mheshimiwa Marjaa Dini mkuu Ayatullah Sayyid Hussein Sistani la swali lililotumwa kwenye ofisi yake.
Tazama pisha iliyo ambatana na habari hii kuona jibu kamili.