Pamoja na kupambana na virusi vya Korona.. Marjaa Dini mkuu: Kuwatibu wagonjwa na kuwahudumia ni wajibu kifaya kwa kila mwenye uwezo na jambo hilo.

Maoni katika picha
Marjaa Dini mkuu amesisitiza kua; kuwatibu na kuwahudumia wagonjwa wa Korona ni wajibu kifaya kwa kila mwenye uwezo wa kufanya hivyo, miongoni mwa madaktari, wauguzi na wengineo.

Hayo yapo katika jibu la Mheshimiwa Marjaa Dini mkuu Sayyid Ali Husseini Sistani la swali lililotumwa ofisini kwake, kuhusu hatari ya maambukizi waliyo nayo madaktari, wauguzi na wasaidizi katika hospitali na vituo vya afya wanapo wahudumia watu walioambukizwa virusi vya Korona, ifuatayo ni nakala ya jibu hilo:

(Hakika kutibu wagonjwa na kuwahudumia ni wajibu kifaya kwa kila anaeweza kufanya hivyo, miongoni mwa madaktari, wauguzi na wengineo).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: