Siku ya tatu mfululizo: kazi ya kupuliza dawa inaendelea

Maoni katika picha
Kamati ya kupambana na majanga katika Atabatu Abbasiyya inaendelea na kazi ya kupuliza dawa maeneo yanayo zunguka Ataba na majengo ya shule kwa siku ya tatu mfululizo.

Dokta Yusufu Twalibu Mahadi kutoka idara ya madaktari amesema kua: Atabatu Abbasiyya imepuliza dawa sehemu zote zinazo izunguka pamoja na majengo ya shule, kwa kushirikiana na kitengo cha usimamizi wa kihandisi chini ya usimamizi wa jopo la madaktari na kamati maalum iliyo undwa na Ataba tukufu.

Kiongozi wa mambo ya kibinadamu chini ya kitengo cha usimamizi wa kihandisi ustadh Hassan Ali Abdulhussein akasema kua: “Miongoni mwa hatua za kujikinga na maambukizi ya virusi vya Korona zilizofanywa na Atabatu Abbasiyya, ni kuunda kamati ya wataalam ambayo imekua ikipuliza dawa kwa siku ya tatu mfululizo, imepuliza sehemu yote ya Ataba pamoja na majengo ya shule”.

Kumbuka kua Atabatu Abbasiyya imeshachukua hatua kadhaa za kujikinga na maambukizi ya virusi vya Korona, na inafuata kwa ukamilifu maelekezo yanayo tolewa na vituo vya afya, katika Ataba, mji na mkoa kwa ujumla.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: