Chuo kikuu cha Al-Ameed kinatumia njia ya ufundishaji kwa njia ya mtandao (masafa).

Maoni katika picha
Chuo kikuu cha Al-Ameed kimeanza kutoa masomo kwa njia ya mtandao (masafa) tangu siku za kwamza za kufungwa rasmi kwa shule, kwa sababu ya maambukizi ya Korona.

Tumeongea na mkuu wa chuo hicho kuhusu swala hili amesema kua: “Chuo chetu kimeanza kutoa elimu ya masafa kwa ajili ya kuwawezesha wanafunzi kuendelea na masomo wakati wa likizo, ili wasipoteze mwaka wa masomo, kutokana na tatizo la virusi vya Korona, amesisitiza umuhimu wa program hiyo kwa wanafunzi”.

Wanafunzi pamoja na wazazi wao wamefurahia sana program hiyo, kwani itawafanya wasipoteze muda wala mada za masomo kama zilivyo pangwa kwenye selebasi.

Kumbuka kua chuo kikuu cha Al-Ameed kinatumia program ya (Moodle) kufundishia kwa miaka miwili takriban, program hiyo humpa nafasi mwanafunzi kuangalia somo lolote kwenye mtandao kulingana na nafasi yake.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: