Kikosi cha Abbasi kinaendelea kushirikiana na kamati maalum, na jeshi la wananchi linasema kua kikosi cha Abbasi kina nafasi kubwa katika kazi ya kupuliza dawa

Maoni katika picha
Kwa siku ya saba mfululizo wapiganaji wa kikosi cha Abbasi (Liyaau/26 Hashdi Shaábi) wakishirikiana na shirika la Khairul-Juud, wanaendelea kupuliza dawa katika mitaa ya mkoa wa Karbala pamoja na jeshi la wananchi.

Msemaji wa kikosi ameripoti kua; opresheni hiyo imehusisha: mtaa wa Abbasi, Zaharaa, na sehemu za bustani zilizopo maeneo hayo, kikosi cha madaktari kinatumia vipaza sauti kutoa elimu.

Uongozi wa jeshi la wananchi katika mkoa wa Karbala umethibitisha nafasi muhimu ya kikosi cha Abbasi katika kupambana na virusi vya Korona.

Kiongozi wa jeshi la wananchi katika mkoa wa Karbala Kapteni Twaahir Hamiid amesema kua: Sehemu kubwa imepulizwa dawa kuanzia barabara viwanja vya wazi hadi katikati ya mji.

Akabainisha kua: “Vikundi vyote vinashirikiana katika kazi hii kwa nguvu na ari kubwa, hapa lazima tuseme haki kuhusi majemedari wa kikosi cha Abbasi (a.s), wana nafasi kubwa katika zamu za asubuhi na jioni, kuna wapiganaji zaidi ya (50) wanafanya kazi kubwa sana”.

Akasisitiza kua: “Kazi inaendelea hadi litakapo tolewa tangazo la kwamba mkoa wa Karbala uko salama kutokana na maambukizi ya virusi vya Korona”.

Tambua kua kikosi cha Abbasi (a.s) cha wapiganaji (Liwaau/26 Hashdi Shaábi) kwa kushirikiana na shirika la Khairul-Juud kilianza opresheni ya kupuliza dawa katika mitaa ya Karbala tangu siku ya Jumatatu (16 Machi 2020m) na bado kinaendelea hadi leo.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: