Kitengo cha meno katika chuo kikuu cha Alkafeel kinachukua tahadhari ya kupambana na virusi vya Korona

Maoni katika picha
Chuo kikuu cha Alkafeel chini ya kamati ya malezi na elimu ya juu katika Atabatu Abbasiyya tukufu kinachukua hatua kadhaa za kujilinda na maambukizi ya virusi vya Korona katika vitengo na idara zake.

Maeneo yote muhimu yamepulizwa dawa kwa kutumia vifaa maalum (CBRN), kazi hiyo imefanywa kwa kushirikiana na mkuu wa kikosi kwa namna ambayo inaendana na eneo husika.

Tambua kua chuo kikuu cha Alkafeel ni sawa na taasisi zingine za elimu zilizo chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu, kinatekeleza majukumu yote kinayo pewa na kamati maalum iliyo undwa na Ataba tukufu, au kutoka kwenye kamati ya mkoa wa Najafu, yanayo tokana na maagizo ya wizara ya afya.

Kumbuka kua Atabatu Abbasiyya tukufu inatekeleza opresheni ya kupuliza dawa maeneo yote yanayo zunguka haram tukufu pamoja na mji mkongwe chini ya kamati maalum iliyo undwa.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: