Idara ya mapambo na miti katika kitengo cha eneo la katikati ya haram mbili tukufu imeanza kazi ya kusafisha na kuchambulia mitende iliyopo katika eneo hilo, sambamba na kupuliza dawa ya kuuwa wadudu wanaodhuru.
Kiongozi wa idara hiyo Ustadh Haatim Abdulkarim ameuambia mtandao wa Alkafeel kua: “Kazi hii huanza katikati ya mwezi wa Machi, chini ya ratiba ya uchambuliaji, kila mtende huchambuliwa mara moja au mara mbili, kazi hiyo hufanywa na wataalam wa sekta hiyo, kila mtende huchambuliwa kulingana na matawi yake pamoja na upambaji wake na kuhakikisha unapamba vizuri na unakua na matunda mazuri”.
Akaongeza kua: “Kazi huendelea hadi mwezi wa sita kipindi cha kukomaa kwa tende, kazi humaliziwa katika mwezi huo kwa kukagua mikungu ya tende iliyopamba na uwezo wa mikungu hiyo katika kubeba matunda, mitende hiyo hupandikizwa aina bora zaidi, kama vile Wardiy na Samismiy na hutoka kwa wahisani, halafu hukaguliwa kama haina maradhi, kama vile maradhi ya Khiyasi na Twalaá”.
Kumbuka kua mitende iliyo pandwa katika eneo la katikati ya haram mbili tukufu ni moja ya miti muhimu inayo weka muonekano wa kijani kibichi katika eneo hilo, pamoja na umuhimu wake kwenye eneo hilo, kuna mitende ipatayo (57) inaashiria umri wa Imamu Hussein (a.s) siku ya kuuwawa kwake katika vita ya Twafu.